Biashara ya Chakula (mama wa biashara zote)

Biashara ya Chakula (mama wa biashara zote)

Nakupa Topography ya Dsm Makonda alikuwa anasema ina shape ya kiganja sisi watu wa Geography tunaita Centripetal pattern...watu wana flow kutoka sehemu kuu 6 kwenda katikati ya mji na kurudi jioni movement hiyo ndio inatengeneza Centre kuu kama tano Dsm kutokea kila balabala.

1)Karikooo (Cantre Kuu 1)
2)Makumbusho (Centre Kuu 2)
2Mbagala Rangitatu (Kilwa Road)
3)Gongo La Mboto (Pugu Road)
4)Mbezi Mwisho (Morogoro Road)
5)Tegeta (Bagamoyo Road)
6)Kigamboni Ferry (Non Road)

Centre Zingine
_Tandika Sokoni
_Magomeni Mapipa
_Buguruni

Ukitaka kuwa na BBQ 3...4...5 sehemu hizi ndio sahihi kama hapo MBAGALA RANGI TATU wanauza masaa 24.
Nimekupata vizuri Sana. Asante kwa ufafanuzi yakinifu. Nitaufanyia kazi.
 
Kuna banda la chips hapa Sinza Mori karibia na La chaaz linaitwa Dubai Hawa jamaa kwa siku kuanzia ijumaa wanauwezo wa kuingiza zaidi ya milion 1 kwa siku Kama net profit hiyo wametoa gharama zote za uendeshaji.

Maisha ya biashara ndogo ndogo sijawahi kuyaelewa kabisaa.
Biashara yenye uwezo wa kuingiza faida ya milion moja kwa siku unafikiri mtaji wake ni shilingi ngapi? Usiangalie tu faida
 
Biashara yenye uwezo wa kuingiza faida ya milion moja kwa siku unafikiri mtaji wake ni shilingi ngapi? Usiangalie tu faida
Pale wafanyakazi wakiendaga wanapewa hiyo obligation kwamba wikiendi kuanzia ijumaa net profit ya 1 milion ipatikane mezani asubuhi tu.

Kwa biashara ya chipsi, supu, kongoro na nyama choma haizidi laki 6 Kama standing capital. Kinachombeba jamaa anapata faida kubwa Yuko location sahihi la Chaaz pale ikioperates whole night Hadi asubuhi milion Kama net profit inapatikana mapema tu.

Kuna jamaa yangu kainvest yeye milion 10 kununua gari iwe Uber na kwa siku analaza profit ndogo saana while invested capital ni kubwa.

While huyu wa chipsi yeye analaza milion kwa standing capital ya laki 6.

Nilichogundua faida kubwa sio mtaji Bali Haina ya biashara. Kuna jamaa jirani anachoma mahindi kwa capital ya elfu 40 na anapata faida Hadi elfu 18 kwa siku.

Chagua biashara sahihi ndogo ndogo then multiply your hustle. Then boom.
 
Pale wafanyakazi wakiendaga wanapewa hiyo obligation kwamba wikiendi kuanzia ijumaa net profit ya 1 milion ipatikane mezani asubuhi tu.

Kwa biashara ya chipsi, supu, kongoro na nyama choma haizidi laki 6 Kama standing capital. Kinachombeba jamaa anapata faida kubwa Yuko location sahihi la Chaaz pale ikioperates whole night Hadi asubuhi milion Kama net profit inapatikana mapema tu.

Kuna jamaa yangu kainvest yeye milion 10 kununua gari iwe Uber na kwa siku analaza profit ndogo saana while invested capital ni kubwa.

While huyu wa chipsi yeye analaza milion kwa standing capital ya laki 6.

Nilichogundua faida kubwa sio mtaji Bali Haina ya biashara. Kuna jamaa jirani anachoma mahindi kwa capital ya elfu 40 na anapata faida Hadi elfu 18 kwa siku.

Chagua biashara sahihi ndogo ndogo then multiply your hustle. Then boom.
Unamaanisha million 1 au labda ngoja nimsubiri Controla.
 
Unamaanisha million 1 au labda ngoja nimsubiri Controla.
Mkuu 1M ni hela ndogo sana kwenye biashara ya chakula kama

ikitokea ukalenga sehemu sahihi inayoteremsha wateja 24hrs

Biashara ya chakula ikikukubalia nakwambia utaona wafanya biashara

wengine kama wanapoteza tu muda wao kwenye biashara zao acha tu mkuu.
 
Biashara ya chakula ni moja ya biashara nzuri na yenye faida na inayoweza kukutoa from zero to hero ndani ya mwaka wako mmoja tu ukikomaa ipasavyo kazini kwako,lakini ili ikutoe kama inavyotoa wengine ni lazima biashara yako iguse wateja wote bila kubagua.

Biashara nyingi sana hapa mjini zinafeli kwasababu 1 kuuu ambayo ni ubaguzi wa wateja,Acha niwape mfano 1 : Zamani kidogo nilitamani kufanya biashara flani hivi,baaada ya kufanya research zangu za ile biashara ninayotaka kuifanya nikagundua kuwa wauzaji wengine wengi wanauza vitu feki ambavyo si original,nikajisemea moyoni mimi nitakua tofauti na wao nitauza vitu OG tuu.

Basi nikafungua ofisi,nikaipendezesha kimuonekano,Weka mabango ya kisasa kbsa biashara ikaanza kweli nilikua nauza vitu OG OG kama mbele mzee,na bei ya vitu OG nadhani mnazijua jamani Kitu ya bei chee pale ilikua ni ya 25k ila vingine vyote bei zake N za moto.

Picha linaanza Day 1 nimeuza hakuna,Day 2 nkauza Desh,Day 3 nkauza Empty mpk kukatika wiki ya kwanza nilikua nauza maneno na kusifia product zangu,nikawa najipa moyo labda sababu ofisi bado mpya ila wapi ikakatka miezi,nikaona hali inazd kua mbaya nikasema Huu ungedere HAPANA siuwezi.

Nikaagiza mzigo ule ule niliokua nauza ORIGINAL nikaagiza FEKI zake sasa,kisha nika brand duka tena upya,matangazo nikaweka upya Kazi ikaanza tena,yani Mauzo yake siwezi andika hapa ila amini amini nawambia Sikuamini macho yangu kwa hesabu niliyofunga Day 1 tu.

Hii maana yake nini? sio kwamba wateja hawakuepo? wala si kwamba nilikosea eneo la kufungua hyo biashara ila kosa langu kubwa lilikua ni KUTENGA WATEJA (ubaguzi) niliwabagua wateja nikawa nime egemea upande mmoja wa wateja wenye nazo nikawasahau hawa wenzangu namimi wenye uwezo wa kati na wachini kbsa ambao kiuhalisia ndio wengi wengi wengi kuliko hawa wengine.

Turudi kwenye Mada yetu ya Biashara ya chakula ;

Nimesema biashara ya chakula ili ikupe faida na matokeo chanya n lazima iguse wateja wote (usiwe m'baguzi) maana jamii tunayoishi imejaa wateja wa aina zote na ni lazima tuwaguse wote.

Leo nataka kumshauri mtu anaetaka kufanya biashara ya chakula kwa kufata IDEA yangu nitakayoichambua hapa chini mwanzo mpk mwisho wa thread hii.

KUUZA CHIPS

Hii ni biashara ya chakula tofauti na vyakula vingine ambayo naipenda kwasababu ni biashara unayoweza ifanya kuanzia asubuhi saa 1 kamili na ukaenda nayo 24hrs watu wakala bila kuchoka,Chipsi ni chakula kinacholika na kupendwa na rika zote,chipsi ni chakula kisicho na muda maalum kulika ndio maana ukiingia k.koo asubuhi saa 1 utakuta raia wanagonga chai maziwa na chips zege hii n kwasababu chipsi inasimama kote kote yani kama kitafunwa,kama mlo mkuu,kama Bites,NK yani kama n chakula kischo na jinsia basi ni CHIPSI.

Sasa hii chips unauzaje ili uguse wateja wote? kipimo cha chipsi kavu kwa wakazi wa dar sio chini ya 1500 na sehemu chache chache sana huko ndan ndani ndio unaweza ukaomba ukapmiwa hata za 1000 ila hapo n uombe na uwe member na umkute muuzaji yupo kwenye mood.

Sasa basi ktk biashara yetu hii ya chipsi tukisema twende kwa bei kipimo 1500/1000 bado tutasurvive kwa muda mchache sana lakni mwisho tutaanguka kabisa kwasababu kiuhalisia buku au buku jero bado n pesa wachache sana wanaimudu (ukweli ndio huu) anaweza imudu kwa leo lakini hatoweza imudu kwa kesho,kesho kutwa,ijumaa,jmos na kuendelea.

Sasa kwann tufanye biashara ambayo uhakika n mpk mteja mfuko uwe vzuri ndio aje? Hamna sababu hiyo,Tufanyeje sasa? Katika biashara yetu ya chipsi ambayo muda wakufungua n saa 1 kamili asubuhi kabati limeshapendeza tutakua tunauza

  • chips
  • mihogo/viazi vitamu (utachagua uweke kipi)
  • ndizi mzuzu (za jero na za 200)
  • mishkaki (ya buku,ya jero, ya 200 na ya 100)
  • Kuku (firigisi/shingo/miguu/vichwa)
  • soseji
  • viazii vya kacholi

Katika vitu vyetu hivyo hapo juu sio lazima ununue gunia la viazi kwasababu ndio tunaanza unaweza ukaaanza na ndoo mbili tu kubwa za viazi au hata 1 kutegemea na uwezo wako,kwenye mihogo hapa napo muhimu chukua mihogo ya 15,000 au hata 20,000 kutegemea na eneo ulipo,ndizi mzuzu hizi nazo unaweza ukafata mkungu wenye ndizi ndogo ndogo kbsa au ukaenda kununua zile za mafungu ndogo ndogo utakazouza 200 na ukanunua na zle mzuzu kubwa utakazoweza uza 500.

Mishkaki nunua kulingana na mfuko wako muhimu uweze kujua kuikata kwa kipimo finyango za buku,za jero,200 na 100 na vitu vingine upendavyo kama hizo kacholi kama unaweza tengeneza usiache hakikisha unaziweka hata kama huwezi tafuta mtu anaeweza Muajiri atengeneze kachori utakazouza sh.100 kwa moja.

Hivi vitu nilivyotaja vinaweza kuonekana ni vingi na kweli n vingi kwasababu nataka tuwe tofauti na wauza chipsi wengine wote eneo tutakalofungua na lengo la kuweka vitu vingi hivi ni ili kuweza pata watu aina zote,Nilisema hapo awali kwamba Hapa Dar na sehemu nyingi sana ili weze kupata mlo wa mchana au usiku n lazima kila mlo usiwe na chini ya 1000 maana yake n kwamba mchana 1000 usiku 1000,sasa kwenye hiii ofisi yetu nataka Wale wenye jero jero zao wakitaka kula wale washibe.

mteja akija na jero akataka mihogo ambayo sisi tunauza sh.200 tutampa mihogo miwili,ile sh 100 tutampa kacholi 1 na tutamuwekea chpsi chombeza ile sahani yake ukiweka na kachumbari zetu atapokea sahani ina mlima atakula atashushia na maji yetu ya kandoro ya bure ya mezani Ataondoka kashiba vizuri kabisa,huyu mteja kurudi tena kwetu sio ombi n lazima tU Maana hamna mahali pengine popote atakapoenda na jero akala akashiba tofauti na kwetu.

View attachment 1526858

wakija wateja V.I.P wale wanaotaka mshkaki wa buku,kidari cha 2500 soseji mayai nao tunaenda nao sawa vile vile hii biashara yetu haina uchawi hta uwe uchochoro gani biashara lazima utusue na ufanye vizuri tu.

Mihogo sio asubuhi tu mihogo kazin kwetu itapatkana muda wote ofisi itakapokua wazi,ndizi kadhalika,kacholi kadhalika hatuanzi na nguvu ya soda speed hii hii tutaenda nayo hat mwisho.

Mtaji wa hii biashara yetu kwa makadirio ya chini kbsa kwa mtu mwenye vyombo vyote ni kama 300,000 na kwa mtu aasie na vyombo maana yake gharama itapanda zaidi lakini Ukiwa na 500,000 - 600,000 unaweza ukaianza hii biashara kibishi bishi mpk utakapoimarika kabisa.

Faida utakayoipata kwenye biashara hii kama upo sehemu nzuri umelenga na ukaiweka biashara kama mimi ninavyoipigia picha huku kichwani kwangu kukunja faida ya 100,000k per day ni jambo la kawaida kbsa,ambapo ukitoa matumizi ukalipa wafanyakazi wako wewe kubaki na 40,000 - 50,000 ni jambo la kawaida sanaaaaaaaa.View attachment 1526867

Kuna watu wanasemaga hizi ni theory hazina uhalisia SAWA SAWA kbsa acha sisi wazee wa thery tuthiorike ila mfano wa biashara hii ya chips ipo Magomeni usalama na nyingine ipo K.koo Aggrey na likoma opposite na POSTAL BANK kuna chaliii ya R chuga iko pale inajua biashara mpk inaboa,akikupmia chipsi ya buku unaweza sema kateleza mkono jinsi anavyomwagia kwenye hiyo sahani.

Hela haweki kwenye epron Hela anatupia kwenye ndoo kubwa Jioni hesabu anayofunga,wewe na duka lako unaweza ukaipata kwa wiki nzima ila mtu anaikunja kwa siku 1.

Kama upo Dar na una mtaji Nakuhakikishia hii biashara ipo siku 1 utakuja toa ushuhuda.Usiache ifanya.Funga macho ifanye Hutojutia nakuhakikishia.

I dedicate this thread kwa watafutaji wote wasiochoka na wenye malengo na wasioridhika na biashara moja kiufupi kwa wapiganaji wote waliopo ndani ya JF amu MAMA nakuaminia sana sana,najua huchokagi wala hujawahi kuchoka,ongezea na hiii.
Uzi nimeupenda asante ndugu niwachache wanaoweza kuonyesha fuls zenye mafanikio wewe niwapekee.Wengi ni wachoyo kuonyesha wenzao fulsa
 
Uzi nimeupenda asante ndugu niwachache wanaoweza kuonyesha fuls zenye mafanikio wewe niwapekee.Wengi ni wachoyo kuonyesha wenzao fulsa
Asante kwa kushukuru Mkuu,sina uwezo wa kugawa pesa za mitaji

kwa kila mtu ila naamini nina uwezo wa kugawa na kutoa mawazo yangu

ambayo kwa namna moja ama nyingine yatamsaidia mtu walau m1 mahali flani.
 
Kuna banda la chips hapa Sinza Mori karibia na La chaaz linaitwa Dubai Hawa jamaa kwa siku kuanzia ijumaa wanauwezo wa kuingiza zaidi ya milion 1 kwa siku Kama net profit hiyo wametoa gharama zote za uendeshaji.

Maisha ya biashara ndogo ndogo sijawahi kuyaelewa kabisaa.
Hapo ndio utata wa biashara unapokuja,mwenye hardware store yenye mtaji wa milioni 40 haingizi milioni 1 kwa siku halafu unashangaa anayeuza chipsi anaipata hiyo na mkopo wowote wa benki.
Inaleta confusion sana.
 
Wewe hata ukipewa siri za uchimbaji wa mafuta una uwezo wa kuanzisha na kuwa mpinzani?una mtaji bilioni ngapi?
Na

Nafkiri kuchimba mafuta ni Biashara yenye faida mbona inasemwa sana na kilamtu anajua na sio siri.

Technology Startup mbona ndio Biashara zenye mafanikio na zinasemwa mpaka mamayangu aliye kijijini hana simu anajua.

Ulikuwa unamaanisha nini kuuza machungwa baharini au.
 
Mkuu unapokuwa na vibanda 10 vya chipsi unawezaje kuvisimamia vyote kwa ufanisi?
Na je kama nahitaji kuanzisha hizo biashara lakini muda wangu ni mchache nawezaje kusimamia na kuhakikisha hakuna wizi au upotevu wa pesa unaoweza kujitokeza?
🖒🖒🖒umeigusa kabisa business yangu na mwanangu Zero IQ hongera mleta mada

Nimeifanya hii business since 2015 almost ulichoongea ni ukweli 98%

Ila nili copy hii idea kwa msanii @SHETTA

Nilimskia anasema yeye ana vibanda 10 vya chips hapa mjini

Mi nkasema ngoja nitest nikaanza maeneo ya kawe ukwamani

Hakika.
 
Hapo ndio utata wa biashara unapokuja,mwenye hardware store yenye mtaji wa milioni 40 haingizi milioni 1 kwa siku halafu unashangaa anayeuza chipsi anaipata hiyo na mkopo wowote wa benki.
Inaleta confusion sana.
Kuna complex phenomenal moja nlikuwa sijaifahamu hatimae nimeifahamu hivi karibuni.
"Business is easy but not simple" ukielewa hii principle Basi biashara haiwezi kukupa shida.

Hivi karibuni nimejifunza vitu vingi saana.
 
nirushie hizo pdf na mimi niongeze maarifa mkuu
Kuna complex phenomenal moja nlikuwa sijaifahamu hatimae nimeifahamu hivi karibuni.
"Business is easy but not simple" ukielewa hii principle Basi biashara haiwezi kukupa shida.

Hivi karibuni nimejifunza vitu vingi saana.
 
nirushie hizo pdf na mimi niongeze maarifa mkuu
Huzipati kwenye PDF hii ni totally elimu ya mtaa. Elimu inayopatikana kwa experience na kuwa na kiu ya kujifunza. Elimu iliyowatoa darasa la 7 wengi wawe mamilionea bila kusoma pdf.

Tuendelee kujifunza. Juzi kwa mtaji wa elfu 60 nimempa kazi dogo mmoja kwa sharti la kugawana faida ambapo daily anantumia 15 Kama net profit yangu na yeye ajilipe hulo huko therefore target yangu Ni kuingiza 200,000/= kwa siku kwa investment ya kawaida saana.. It's insane! Nataka nimultiply hii idea kwa vijana 15 hapa Dar. After 4 weeks nitakuwa nimemaliza kazi ya kuwasimika sehemu mbalimbali za Dar.

Show inaanza Sasa......
 
Back
Top Bottom