CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 6,939
- 22,985
- Thread starter
- #101
Hata Kujitolea.
TRUE STORY
Siku moja nilienda mahali kula chipsi,nikaagiza wakaniletea huwa nikienda kula mahali kiepe nawambiaga waweke kila kitu kasoro mayonaize zao tu.
Basi nikaletewa kiepe kwakweli zile chipsi zilikua safi sana sana zinang'aa lakini zaidi pilipili yao ilikua inawasha haswaaa na ni tamu sio kitoto yani unakula pilipili makamasi yanashuka ila bado unailamba.
tukija kwenye kachumbari ndio usiseme sijui ile kachumbari ilikua inatengenezwaje,kusema ukweli zile chipsi sikuwahi kuzila mahali popote tangu nizaliwe.
Kumbuka hapo nina goli la kuuza chipsi namimi sio kwamba sina
ila chipsi zangu si tamu na nzuri kama zile,nikawa nimetamani kweli zile chips na kila kitu cha pale nikawa najiuliza moyoni namimi nifanyeje ili niweze kutoa chipsi za namna hii?
basi next time nikarudi tena nikaagiza vile vile kiepe ila safari hii nilienda kwa lengo la kukagua zile chipsi na pilipili na kila kitu chao ili namm nikatengeneze kwangu,sikwenda kwasababu nilikua na njaa Hapana.
Nlipofika nikaagiza wakaniletea,nikanawa mikono nikainua kipande cha chipsi nikakisogeza machoni kbsa nikawa nakikagua,hiki n kiazi kweli au kuna uziada uliofanyika hadi kiepe kikang'aa vile? kwenye viazi nikagundua kuwa kuna kitu imeongezwa ambayo n rangi,swali n kwamba Je n rangi gani? (hapo nikapaacha)
nikaja kwenye kwenye pilipili nikatia mdomoni nikawa naskilizia kung'amua viungo vilivyotumika ila Nikatoka kapa,Nikaja kwenye kachumbari napo nikatoka kapa sikuweza gundua chochote.
Nikajiuliza sasa nafanyaje? nikienda kule kwangu nikimtuma mfanyakazi wangu mmoja aje ajitolee hapa kwenye hii ofisi atakubaliwa ataingia ila je Huyu mfanyakazi wangu Nitakua nae miaka yote? Jibu hapana.
Nilichoamua n mimi mwenyewe kwenda kuomba kazi ya kujitolea kwenye ile ofisi,Basi SIKU 1 nikadamka saa 10 usiku nikaenda pale nikaomba kazi japo sikumkuta boss nikawa naomba tu kusaidia nikawa nasaidia,mida mida ikafika boss akaja akanikuta akauliza taarifa zangu akaambiwa najitolea tu kufanya kazi.
hakukataa basi nikawa nafanya kazi,ikafika muda wa kachumbari wakawa wanaandalia ndani mimi nipo nnje namenyeshwa viazi,Lengo langu likawa halijatimia,Day 1 ikaisha sikujua chchte kuhusu pilipili wala kachumbari,Ikaja day 2 nikatoka kapa,Day 3 ndio nikaambiiwa niandae pilipili nikaelekezwa jinsi yakuandaa mpk ikakamilika.
Day 4 nikaandaa tena pilipili kweli ikatoka kama ile niliyokua naila,day 5 nikahamia kwenye kachumbari kiufupi nilifanya kazi ile ofisi kama wiki (siku 7) nikaongeza siku nyingine kama 3 mbele maana nakumbuka nilisingizia naumwa ilikua j4 sikwenda kbsa HAPO n baada ya ku master kila kitu.
Wakawa wananipgia sana simu nirudi kazini boss akasema nirudi atakua ananilipa ila nilisingizia nimesafiri nikirudi ntaenda,walisumbua sana ila mwisho wakanipotezea.
Nikarudi kwenye magoli yangu nikawa nawaandalia mimi kachumbari na pilipili,wateja wakapenda nikafundsha wafanyakazi jinsi ya kuandaa,nikazunguka ofisi zote nikatoa somo likaeleweka basi saivi usijiloge ukaja kula kiepe eneo langu maana ndio utakua umenasa hiyo.
Lengo la kusimulia hii kitu refu hivi ni nini?
wakati mwingine tunapaswa kuingia gharama/kupoteza muda ili kupata kitu kizuri Pesa si kitu kama huna akili za kujua uitumie vipi hiyo pesa.
pesa haiwezi kukupikia chakula kitamu,pesa haiwezi kukutengenezea kachumbari nzuri,pesa si kila kitu linapokuja swala la ubunifu ktk biashara unayofanya ili uweze kufikia malengo yako.
na ktk biashara zinazotaka uwe m'bunifu kila siku iendayo leo n biashara ya chakula maana ukizoesha wateja taste flani kila siku wakiizoea wataaanza kuona chakula chako kibaya wakat chakula n kile kile cha siku zote.
ukizoesha wateja aina flani ya kachumbari ukawa unaiandaa hyo hyo kila siku wakiichoka wataanza iona mbaya wakat kachumbari n ile ile,ndio mana biashara ya chakula inataka ubunifu wa hali ya juu Mfano leo ukipika wali wa nazi,kesho unawapikia wali wa kitunguu,kesho kutwa unawapikia wali wa maua Yani haina kukariri chakula cha ofisi yako kiko vipi.
ukipka chai ya rangi leo unapika unaweka viungo hivi,kesho unaweka viungo vile kesho kutwa unawapkia na mchai chai peke yake,nk nk yani hamna kukaririr taste ya chai wala chochote kinachopikwa ktk ofisi yako.
ila ukisema upike chakula kile kile wali aina ile ile,pilau lile lile,chai ile ile,kachumbari,nk nknk aseee utapata wateja ila hutodumu na hao wateja maana wateja n watu wapenda kubadilisha ladha,na hiyo ipo kwa kila mtu duniani.
Kwahyo tunarudi pale pale kuwa ubunifu ktk biashara ya chakula unahitajika sana na ubunifu huu huwezi kuupata kama huzungki ofisi za wengine,hutembelei wenzako,Ukijiona umekua boss ukiamini huwezi tena kuajiriwa wala kushuka chini basi Biashara haikufai na siku 1 isiyo na jina utaanguka na utaanza singizia biashara bila ndumba haiendi wakati si kweli.