Biashara ya Chakula (mama wa biashara zote)

Biashara ya Chakula (mama wa biashara zote)

Mtaji wa ndoo 1 hutakiwi kuwa hata na mfanyakazi mkuu

kwann uliweka mfanyakazi biashara changa kiasi hicho?

Kwa biashara yako kilichokuangusha n MATUMIZI yalikua

makubwa kuliko kilichokua kinapatikana,kwa uono wangu.
Sawa sawa nmekupata....nliweka mfanyakaz ili niibie ujuz mana nlikua cjui kuchoma chips wala mishkak....lakn ndo hvo mtaji ukaungua kabla cjasimama effective
 
Tena unamlipa mfanyakazi 8000 asee mkuu zunguka hebu

mtu anauza magunia na magunia ila analipa wafanyakazi 5000

yani wewe ulikua boss mzuri sana,huyo mfanyakazi hatokaa akusahau.
hili pia nahs lilikua tatzo....
 
ndio mkuu wateja walikuepo ila wachache sana mana nlikua nkiuza ndoo MOJA TU. kwa sku na sku nyngne chips znalala. japo hata zle sku ambazo chips zlikuwa znaisha bado nkipiga hesabu nakula shoti.
Ulikosea kitu kimoja... Kupata strategic location yenye potential. Chips ukiipatia sehem nzuri faida huwa inaonekana mapema tu!

Sinza pale Mori Kuna jamaa anawalipa wafanyakazi wake 5 elfu 10 kila siku jumla elfu 50, analipa umeme elfu 30 kila siku, pango anachangia elfu 10 kila siku, kwa wastani anatumia 100,000 kwa matumizi ya kawaida tu afu baadae anapata faida yake vizuri tu. Huu mwaka wa tano Sasa.
 
Nikikumbuka jamaa aliwekeza Bonge la biashara la kisasa BBQ anauza chips na vikorombwezo vyote na wali supu MENU imekamilika location inavutia wafanyakazi Tshirt Marketing mpaka group la whatsApp na Agent jamaa alifanya ubunifu wa Deliver maana wateja wanachuo sasa kule wanapopita sana wanachuo akaweka kibanda ambacho Mobile wanakipeleka na kukirudisha eti baadae akashindwa biashara hakuna faida aisee.
 
umewezaje kusavaiv mda wote asee.,,??

mm nliwah fungua biashara ya chips pale manzese sinza uzuri.kuna hotel inaitwa vienna hotel,nlifungua kwa pembeni. cha ajabu sasa unakuta nanunua ndoo moja ya viaz,nyama ya mishkak na viungo vingne. ila kufika jion napiga hesabu nakuta either imerud hela ile ile au nmekula shot kabsa.sku ya pili tena nkachukua pesa pemben nkaweka kla ktu mpaka kuku lakn kufika jion napiga hesabu nakuta shoti tena. nlikua mm na jamaa mngne lakn sidhan kama alikua ananiibia mana kuna sku naamua mm ndo npokee pesa zote kwa wateja lakn nakuta yale yale. kiukweli nilitumia mtaji wote mpaka pesa ikakata. nakumbka sku ya mwisho baada ya kuona sasa sna pesa ya kuendelea kuongeza, nkafunga, niliondoka na shilingi elfu 3.

mpaka leo nikikaa huwa najiuliza nlikuwa nakosea wapi ila sjawah kupata jbu.
Kuna mzee mmoja Yuko pale nyuma ya kanisa la St Peter's anauza chipsi za kuanzia 200 kwa watoto wa shule Hadi watu wazima kuanzia 1000. Lakini anasomesha watoto na kuendesha familia yake vizuri tu.

Means anapata faida consistently sababu ana muda mrefu anapush ile idea smoothly.
 
kila sku nlikua natoa pesa pemben ili kununua viaz na mahtaji mengne pamoja na kumlipa mfanyakaz 8000 per day (hapo kumbka tunafanya kaz wote but yy jion lazma aondoke na hela). nlijipa moyo kwamba mfanyabiashara unatakiwa kuwa mvumiliv but hela iliniishia nikafunga tu.
Nahisi kuna siku ulitamani wewe ndo uwe mfanyakazi uiipate ile 8,000
 
Unamlipa 8000 kwa startup business na tena watendaji ni wote mbona naona faida ya 2000 ulikuwa unampa yeye ungemlipa 5000-6000 kwa Startup kwanza hii inaonesha na sehemu nyengine umefeli kimahesabu.Hi

Hivi mkuu ndoo moja ni sahani ngapi anatoa na yule anaeingiza 200K anaweza akawa anaPush ndoo ngapi.
Ndoo inategemea na upimaji mkuu kila mtu na upimaji wake,anae ingiza 200k

hana kipimo maalum pia maana inategemea ktk zile chips kauza nyingi chips yai

au kauza sana kavu,chipsi yenye hela n chips yai mkuu ndio ishu,kavu sio kivileee.
 
umewezaje kusavaiv mda wote asee.,,??

mm nliwah fungua biashara ya chips pale manzese sinza uzuri.kuna hotel inaitwa vienna hotel,nlifungua kwa pembeni. cha ajabu sasa unakuta nanunua ndoo moja ya viaz,nyama ya mishkak na viungo vingne. ila kufika jion napiga hesabu nakuta either imerud hela ile ile au nmekula shot kabsa.sku ya pili tena nkachukua pesa pemben nkaweka kla ktu mpaka kuku lakn kufika jion napiga hesabu nakuta shoti tena. nlikua mm na jamaa mngne lakn sidhan kama alikua ananiibia mana kuna sku naamua mm ndo npokee pesa zote kwa wateja lakn nakuta yale yale. kiukweli nilitumia mtaji wote mpaka pesa ikakata. nakumbka sku ya mwisho baada ya kuona sasa sna pesa ya kuendelea kuongeza, nkafunga, niliondoka na shilingi elfu 3.

mpaka leo nikikaa huwa najiuliza nlikuwa nakosea wapi ila sjawah kupata jbu.
Makosa yako mkuu yalikuwa haya
1; location
2; matumizi makubwa kuliko unachoingiza, 8000 per day ni nyingi kwa mfanyakaz
3, hukuwa na ujuzi wowote kuhusu chips
4, hukusoma mchezo kiufasaha kabla ya kuingia. Ulikurupuka
 
sawa sawa nmekupata....nliweka mfanyakaz ili niibie ujuz mana nlikua cjui kuchoma chips wala mishkak....lakn ndo hvo mtaji ukaungua kabla cjasimama effective
Next time ukitaka kupata ujuzi wa kitu,kubali kuajiriwa mkuu

sio dhambi wala sio kosa kuajiriwa ili kwenda kujifunza mkuu

tatizo watu wakiskia ujasiriamali wanafkiri ndio hatakiwi kuajiriwa

yawezekana ukaajiriwa vizuri na ukawa mjasiriamali,usirudie makosa tena chief.
 
Hat
Next time ukitaka kupata ujuzi wa kitu,kubali kuajiriwa mkuu

sio dhambi wala sio kosa kuajiriwa ili kwenda kujifunza mkuu

tatizo watu wakiskia ujasiriamali wanafkiri ndio hatakiwi kuajiriwa

yawezekana ukaajiriwa vizuri na ukawa mjasiriamali,usirudie makosa tena chief.
Hata Kujitolea.
 
Barikiwa
Biashara ya chakula ni moja ya biashara nzuri na yenye faida na inayoweza kukutoa from zero to hero ndani ya mwaka wako mmoja tu ukikomaa ipasavyo kazini kwako,lakini ili ikutoe kama inavyotoa wengine ni lazima biashara yako iguse wateja wote bila kubagua.

Biashara nyingi sana hapa mjini zinafeli kwasababu 1 kuuu ambayo ni ubaguzi wa wateja,Acha niwape mfano 1 : Zamani kidogo nilitamani kufanya biashara flani hivi,baaada ya kufanya research zangu za ile biashara ninayotaka kuifanya nikagundua kuwa wauzaji wengine wengi wanauza vitu feki ambavyo si original,nikajisemea moyoni mimi nitakua tofauti na wao nitauza vitu OG tuu.

Basi nikafungua ofisi,nikaipendezesha kimuonekano,Weka mabango ya kisasa kbsa biashara ikaanza kweli nilikua nauza vitu OG OG kama mbele mzee,na bei ya vitu OG nadhani mnazijua jamani Kitu ya bei chee pale ilikua ni ya 25k ila vingine vyote bei zake N za moto.

Picha linaanza Day 1 nimeuza hakuna,Day 2 nkauza Desh,Day 3 nkauza Empty mpk kukatika wiki ya kwanza nilikua nauza maneno na kusifia product zangu,nikawa najipa moyo labda sababu ofisi bado mpya ila wapi ikakatka miezi,nikaona hali inazd kua mbaya nikasema Huu ungedere HAPANA siuwezi.

Nikaagiza mzigo ule ule niliokua nauza ORIGINAL nikaagiza FEKI zake sasa,kisha nika brand duka tena upya,matangazo nikaweka upya Kazi ikaanza tena,yani Mauzo yake siwezi andika hapa ila amini amini nawambia Sikuamini macho yangu kwa hesabu niliyofunga Day 1 tu.

Hii maana yake nini? sio kwamba wateja hawakuepo? wala si kwamba nilikosea eneo la kufungua hyo biashara ila kosa langu kubwa lilikua ni KUTENGA WATEJA (ubaguzi) niliwabagua wateja nikawa nime egemea upande mmoja wa wateja wenye nazo nikawasahau hawa wenzangu namimi wenye uwezo wa kati na wachini kbsa ambao kiuhalisia ndio wengi wengi wengi kuliko hawa wengine.

Turudi kwenye Mada yetu ya Biashara ya chakula ;

Nimesema biashara ya chakula ili ikupe faida na matokeo chanya n lazima iguse wateja wote (usiwe m'baguzi) maana jamii tunayoishi imejaa wateja wa aina zote na ni lazima tuwaguse wote.

Leo nataka kumshauri mtu anaetaka kufanya biashara ya chakula kwa kufata IDEA yangu nitakayoichambua hapa chini mwanzo mpk mwisho wa thread hii.

KUUZA CHIPS

Hii ni biashara ya chakula tofauti na vyakula vingine ambayo naipenda kwasababu ni biashara unayoweza ifanya kuanzia asubuhi saa 1 kamili na ukaenda nayo 24hrs watu wakala bila kuchoka,Chipsi ni chakula kinacholika na kupendwa na rika zote,chipsi ni chakula kisicho na muda maalum kulika ndio maana ukiingia k.koo asubuhi saa 1 utakuta raia wanagonga chai maziwa na chips zege hii n kwasababu chipsi inasimama kote kote yani kama kitafunwa,kama mlo mkuu,kama Bites,NK yani kama n chakula kischo na jinsia basi ni CHIPSI.

Sasa hii chips unauzaje ili uguse wateja wote? kipimo cha chipsi kavu kwa wakazi wa dar sio chini ya 1500 na sehemu chache chache sana huko ndan ndani ndio unaweza ukaomba ukapmiwa hata za 1000 ila hapo n uombe na uwe member na umkute muuzaji yupo kwenye mood.

Sasa basi ktk biashara yetu hii ya chipsi tukisema twende kwa bei kipimo 1500/1000 bado tutasurvive kwa muda mchache sana lakni mwisho tutaanguka kabisa kwasababu kiuhalisia buku au buku jero bado n pesa wachache sana wanaimudu (ukweli ndio huu) anaweza imudu kwa leo lakini hatoweza imudu kwa kesho,kesho kutwa,ijumaa,jmos na kuendelea.

Sasa kwann tufanye biashara ambayo uhakika n mpk mteja mfuko uwe vzuri ndio aje? Hamna sababu hiyo,Tufanyeje sasa? Katika biashara yetu ya chipsi ambayo muda wakufungua n saa 1 kamili asubuhi kabati limeshapendeza tutakua tunauza

  • chips
  • mihogo/viazi vitamu (utachagua uweke kipi)
  • ndizi mzuzu (za jero na za 200)
  • mishkaki (ya buku,ya jero, ya 200 na ya 100)
  • Kuku (firigisi/shingo/miguu/vichwa)
  • soseji
  • viazii vya kacholi

Katika vitu vyetu hivyo hapo juu sio lazima ununue gunia la viazi kwasababu ndio tunaanza unaweza ukaaanza na ndoo mbili tu kubwa za viazi au hata 1 kutegemea na uwezo wako,kwenye mihogo hapa napo muhimu chukua mihogo ya 15,000 au hata 20,000 kutegemea na eneo ulipo,ndizi mzuzu hizi nazo unaweza ukafata mkungu wenye ndizi ndogo ndogo kbsa au ukaenda kununua zile za mafungu ndogo ndogo utakazouza 200 na ukanunua na zle mzuzu kubwa utakazoweza uza 500.

Mishkaki nunua kulingana na mfuko wako muhimu uweze kujua kuikata kwa kipimo finyango za buku,za jero,200 na 100 na vitu vingine upendavyo kama hizo kacholi kama unaweza tengeneza usiache hakikisha unaziweka hata kama huwezi tafuta mtu anaeweza Muajiri atengeneze kachori utakazouza sh.100 kwa moja.

Hivi vitu nilivyotaja vinaweza kuonekana ni vingi na kweli n vingi kwasababu nataka tuwe tofauti na wauza chipsi wengine wote eneo tutakalofungua na lengo la kuweka vitu vingi hivi ni ili kuweza pata watu aina zote,Nilisema hapo awali kwamba Hapa Dar na sehemu nyingi sana ili weze kupata mlo wa mchana au usiku n lazima kila mlo usiwe na chini ya 1000 maana yake n kwamba mchana 1000 usiku 1000,sasa kwenye hiii ofisi yetu nataka Wale wenye jero jero zao wakitaka kula wale washibe.

mteja akija na jero akataka mihogo ambayo sisi tunauza sh.200 tutampa mihogo miwili,ile sh 100 tutampa kacholi 1 na tutamuwekea chpsi chombeza ile sahani yake ukiweka na kachumbari zetu atapokea sahani ina mlima atakula atashushia na maji yetu ya kandoro ya bure ya mezani Ataondoka kashiba vizuri kabisa,huyu mteja kurudi tena kwetu sio ombi n lazima tU Maana hamna mahali pengine popote atakapoenda na jero akala akashiba tofauti na kwetu.

View attachment 1526858

wakija wateja V.I.P wale wanaotaka mshkaki wa buku,kidari cha 2500 soseji mayai nao tunaenda nao sawa vile vile hii biashara yetu haina uchawi hta uwe uchochoro gani biashara lazima utusue na ufanye vizuri tu.

Mihogo sio asubuhi tu mihogo kazin kwetu itapatkana muda wote ofisi itakapokua wazi,ndizi kadhalika,kacholi kadhalika hatuanzi na nguvu ya soda speed hii hii tutaenda nayo hat mwisho.

Mtaji wa hii biashara yetu kwa makadirio ya chini kbsa kwa mtu mwenye vyombo vyote ni kama 300,000 na kwa mtu aasie na vyombo maana yake gharama itapanda zaidi lakini Ukiwa na 500,000 - 600,000 unaweza ukaianza hii biashara kibishi bishi mpk utakapoimarika kabisa.

Faida utakayoipata kwenye biashara hii kama upo sehemu nzuri umelenga na ukaiweka biashara kama mimi ninavyoipigia picha huku kichwani kwangu kukunja faida ya 100,000k per day ni jambo la kawaida kbsa,ambapo ukitoa matumizi ukalipa wafanyakazi wako wewe kubaki na 40,000 - 50,000 ni jambo la kawaida sanaaaaaaaa.View attachment 1526867

Kuna watu wanasemaga hizi ni theory hazina uhalisia SAWA SAWA kbsa acha sisi wazee wa thery tuthiorike ila mfano wa biashara hii ya chips ipo Magomeni usalama na nyingine ipo K.koo Aggrey na likoma opposite na POSTAL BANK kuna chaliii ya R chuga iko pale inajua biashara mpk inaboa,akikupmia chipsi ya buku unaweza sema kateleza mkono jinsi anavyomwagia kwenye hiyo sahani.

Hela haweki kwenye epron Hela anatupia kwenye ndoo kubwa Jioni hesabu anayofunga,wewe na duka lako unaweza ukaipata kwa wiki nzima ila mtu anaikunja kwa siku 1.

Kama upo Dar na una mtaji Nakuhakikishia hii biashara ipo siku 1 utakuja toa ushuhuda.Usiache ifanya.Funga macho ifanye Hutojutia nakuhakikishia.

I dedicate this thread kwa watafutaji wote wasiochoka na wenye malengo na wasioridhika na biashara moja kiufupi kwa wapiganaji wote waliopo ndani ya JF amu MAMA nakuaminia sana sana,najua huchokagi wala hujawahi kuchoka,ongezea na hiii.
 
Nahisi kuna siku ulitamani wewe ndo uwe mfanyakazi uiipate ile 8,000
Yaan kila ikifika mda wa kupiga hesabu nakuta shoti nlikuwa namkumbka nataman nompigie smu mzee wa kuuza vihepe Zero IQ nmuulize yy anafanyeje kupata faida?

japo saiz wamemwibia vifaa nampa pole
 
Makosa yako mkuu yalikuwa haya
1; location
2; matumizi makubwa kuliko unachoingiza, 8000 per day ni nyingi kwa mfanyakaz
3, hukuwa na ujuzi wowote kuhusu chips
4, hukusoma mchezo kiufasaha kabla ya kuingia. Ulikurupuka
Sawa
 
Next time ukitaka kupata ujuzi wa kitu,kubali kuajiriwa mkuu

sio dhambi wala sio kosa kuajiriwa ili kwenda kujifunza mkuu

tatizo watu wakiskia ujasiriamali wanafkiri ndio hatakiwi kuajiriwa

yawezekana ukaajiriwa vizuri na ukawa mjasiriamali,usirudie makosa tena chief.
sawa mkuu nmejfunza
 
Huzipati kwenye PDF hii ni totally elimu ya mtaa. Elimu inayopatikana kwa experience na kuwa na kiu ya kujifunza. Elimu iliyowatoa darasa la 7 wengi wawe mamilionea bila kusoma pdf.

Tuendelee kujifunza. Juzi kwa mtaji wa elfu 60 nimempa kazi dogo mmoja kwa sharti la kugawana faida ambapo daily anantumia 15 Kama net profit yangu na yeye ajilipe hulo huko therefore target yangu Ni kuingiza 200,000/= kwa siku kwa investment ya kawaida saana.. It's insane! Nataka nimultiply hii idea kwa vijana 15 hapa Dar. After 4 weeks nitakuwa nimemaliza kazi ya kuwasimika sehemu mbalimbali za Dar.

Show inaanza Sasa......
Umeiva mkuu! Utajiri unakuja kwa ku Multiply hussles!
 
Nikikumbuka jamaa aliwekeza Bonge la biashara la kisasa BBQ anauza chips na vikorombwezo vyote na wali supu MENU imekamilika location inavutia wafanyakazi Tshirt Marketing mpaka group la whatsApp na Agent jamaa alifanya ubunifu wa Deliver maana wateja wanachuo sasa kule wanapopita sana wanachuo akaweka kibanda ambacho Mobile wanakipeleka na kukirudisha eti baadae akashindwa biashara hakuna faida aisee.
Biashara sio kitu cha kila mtu! Kuna watu wana karama tu ya biashara! Hizi biashara za kibongobongo uendeshaji wake una janjajanja nyingi sana wengine wanaendelea sio kama wana product nzuri ila vi mzizizology vinafanya kazi.
 
Back
Top Bottom