Biashara ya Chakula (mama wa biashara zote)

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,935
22,919
Biashara ya chakula ni moja ya biashara nzuri na yenye faida na inayoweza kukutoa from zero to hero ndani ya mwaka wako mmoja tu ukikomaa ipasavyo kazini kwako, lakini ili ikutoe kama inavyotoa wengine ni lazima biashara yako iguse wateja wote bila kubagua.

Biashara nyingi sana hapa mjini zinafeli kwasababu 1 kuu ambayo ni ubaguzi wa wateja. Acha niwape mfano 1 : Zamani kidogo nilitamani kufanya biashara flani hivi,baaada ya kufanya research zangu za ile biashara ninayotaka kuifanya nikagundua kuwa wauzaji wengine wengi wanauza vitu feki ambavyo si original,nikajisemea moyoni mimi nitakua tofauti na wao nitauza vitu OG tuu.

Basi nikafungua ofisi, nikaipendezesha kimuonekano, Weka mabango ya kisasa kabisa biashara ikaanza kweli nilikua nauza vitu OG OG kama mbele mzee na bei ya vitu OG nadhani mnazijua jamani kitu ya bei chee pale ilikua ni ya 25k ila vingine vyote bei zake ni za moto.

Picha linaanza Day 1 nimeuza hakuna, Day 2 nkauza Desh, Day 3 nkauza Empty mpk kukatika wiki ya kwanza nilikua nauza maneno na kusifia product zangu, nikawa najipa moyo labda sababu ofisi bado mpya ila wapi ikakatka miezi,nikaona hali inazd kua mbaya nikasema Huu ungedere HAPANA siuwezi.

Nikaagiza mzigo ule ule niliokua nauza ORIGINAL nikaagiza FEKI zake sasa, kisha nika brand duka tena upya, matangazo nikaweka upya kazi ikaanza tena yani Mauzo yake siwezi andika hapa ila amini amini nawambia sikuamini macho yangu kwa hesabu niliyofunga Day 1 tu.

Hii maana yake nini? Sio kwamba wateja hawakuepo? Wala si kwamba nilikosea eneo la kufungua hyo biashara ila kosa langu kubwa lilikua ni KUTENGA WATEJA (ubaguzi) niliwabagua wateja nikawa nimeegemea upande mmoja wa wateja wenye nazo nikawasahau hawa wenzangu namimi wenye uwezo wa kati na wachini kabisa ambao kiuhalisia ndio wengi wengi wengi kuliko hawa wengine.

Turudi kwenye Mada yetu ya Biashara ya chakula;

Nimesema biashara ya chakula ili ikupe faida na matokeo chanya ni lazima iguse wateja wote (usiwe m'baguzi) maana jamii tunayoishi imejaa wateja wa aina zote na ni lazima tuwaguse wote.

Leo nataka kumshauri mtu anaetaka kufanya biashara ya chakula kwa kufata IDEA yangu nitakayoichambua hapa chini mwanzo mpk mwisho wa thread hii.

KUUZA CHIPS

Hii ni biashara ya chakula tofauti na vyakula vingine ambayo naipenda kwa sababu ni biashara unayoweza ifanya kuanzia asubuhi saa 1 kamili na ukaenda nayo 24hrs watu wakala bila kuchoka.

Chipsi ni chakula kinacholika na kupendwa na rika zote, chipsi ni chakula kisicho na muda maalum kulika ndio maana ukiingia Kariakoo asubuhi saa 1 utakuta raia wanagonga chai maziwa na chips zege hii ni kwa sababu chipsi inasimama kote kote yani kama kitafunwa, kama mlo mkuu, kama Bites NK yani kama ni chakula kisicho na jinsia basi ni CHIPSI.

Sasa hii chips unauzaje ili uguse wateja wote? Kipimo cha chipsi kavu kwa wakazi wa Dar sio chini ya 1500 na sehemu chache chache sana huko ndan ndani ndio unaweza ukaomba ukapimiwa hata za 1000 ila hapo ni uombe sana au uwe member unaejulikana na umkute muuzaji yupo kwenye mood hiyo siku.

Sasa basi katika biashara yetu hii ya chipsi tukisema twende kwa bei kipimo 1500/1000 bado tutasurvive kwa muda mchache sana lakini mwisho tutaanguka kabisa kwa sababu kiuhalisia buku au buku jero bado ni pesa wachache sana wanaimudu (ukweli ndio huu) anaweza imudu kwa leo lakini hatoweza imudu kwa kesho, kesho kutwa, Ijumaa, Jumamosi na kuendelea.

Sasa kwanini tufanye biashara ambayo uhakika ni mpaka mteja mfuko uwe vzuri ndio aje? Hamna sababu hiyo. Tufanyeje sasa? Katika biashara yetu ya chipsi ambayo muda wa kufungua n saa 1 kamili asubuhi kabati limeshapendeza tutakua tunauza
  • Chips
  • Mihogo/viazi vitamu (utachagua uweke kipi)
  • Ndizi mzuzu (za jero na za 200)
  • Mishkaki (ya buku,ya jero, ya 200 na ya 100)
  • Kuku (firigisi/shingo/miguu/vichwa)
  • Soseji
  • Viazii vya kacholi

Katika vitu vyetu hivyo hapo juu sio lazima ununue gunia la viazi kwa sababu ndio tunaanza unaweza ukaaanza na ndoo mbili tu kubwa za viazi au hata 1 kutegemea na uwezo wako.

Kwenye mihogo hapa napo muhimu chukua mihogo ya 15,000 au hata 20,000 kutegemea na eneo ulipo, ndizi mzuzu hizi nazo unaweza ukafata mkungu wenye ndizi ndogo ndogo kabisa au

Ukaenda kununua zile za mafungu ndogo ndogo utakazouza 200 na ukanunua na zile mzuzu kubwa utakazoweza uza 500.

Mishkaki nunua kulingana na mfuko wako muhimu uweze kujua kuikata kwa kipimo finyango za buku za jero, 200 na 100 na vitu vingine upendavyo kama hizo kacholi kama unaweza tengeneza usiache hakikisha unaziweka hata kama huwezi tafuta mtu anaeweza Muajiri atengeneze kachori utakazouza sh.100 kwa moja.

Hivi vitu nilivyotaja vinaweza kuonekana ni vingi na kweli ni vingi kwa sababu nataka tuwe tofauti na wauza chipsi wengine wote eneo tutakalofungua na lengo la kuweka vitu vingi hivi ni ili kuweza pata watu aina zote.

Nilisema hapo awali kwamba Hapa Dar na sehemu nyingi sana ili weze kupata mlo wa mchana au usiku ni lazima kila mlo usiwe na chini ya 1000 maana yake ni kwamba mchana 1000 usiku 1000, sasa kwenye hii ofisi yetu nataka Wale wenye jero jero zao nao wakitaka kula wale washibe.

Mteja akija na jero akataka mihogo ambayo sisi tunauza sh.200 tutampa mihogo miwili, ile sh 100 tutampa kacholi 1 na tutamuwekea chipsi chombeza ile sahani yake ukiweka na kachumbari zetu atapokea sahani ina mlima atakula atashushia na maji yetu ya kandoro ya bure ya mezani Ataondoka kashiba vizuri kabisa,

Huyu mteja kurudi tena kwetu sio ombi ni lazima tu Maana hamna mahali pengine popote atakapoenda na jero akala akashiba tofauti na kwetu.

MIHOGO.2.JPG

wakija wateja V.I.P wale wanaotaka mshkaki wa buku,kidari cha 2500 soseji mayai nao tunaenda nao sawa vile vile hii biashara yetu haina uchawi hta uwe uchochoro gani biashara lazima utusue na ufanye vizuri tu.

Mihogo sio asubuhi tu mihogo kazin kwetu itapatkana muda wote ofisi itakapokua wazi,ndizi kadhalika,kacholi kadhalika hatuanzi na nguvu ya soda speed hii hii tutaenda nayo hadi mwisho.

Mtaji wa hii biashara yetu kwa makadirio ya chini kbsa kwa mtu mwenye vyombo vyote ni kama 300,000 na kwa mtu aasie na vyombo maana yake gharama itapanda zaidi lakini Ukiwa na 500,000 - 600,000 unaweza ukaianza hii biashara kibishi bishi mpk utakapoimarika kabisa.

Faida utakayoipata kwenye biashara hii kama upo sehemu nzuri umelenga na ukaiweka biashara kama mimi ninavyoipigia picha huku kichwani kwangu kukunja faida ya 100,000k per day ni jambo la kawaida kbsa,ambapo ukitoa matumizi ukalipa wafanyakazi wako wewe kubaki na 40,000 - 50,000 ni jambo la kawaida sanaaaaaaaa.
maxresdefault.jpg

Kuna watu wanasemaga hizi ni theory hazina uhalisia SAWA SAWA kbsa acha sisi wazee wa theory tuthiorike ila mfano wa biashara hii ya chips ipo Magomeni usalama na nyingine ipo K.koo Aggrey na likoma opposite na POSTAL BANK kuna chaliii ya R chuga iko pale inajua biashara mpk inaboa,akikupmia chipsi ya buku unaweza sema kateleza mkono jinsi anavyomwagia kwenye hiyo sahani.

Hela haweki kwenye epron Hela anatupia kwenye ndoo kubwa Jioni hesabu anayofunga,wewe na duka lako unaweza ukaipata kwa wiki nzima ila mtu anaikunja kwa siku 1.

Kama upo Dar na una mtaji Nakuhakikishia hii biashara ipo siku 1 utakuja toa ushuhuda.Usiache ifanya.Funga macho ifanye Hutojutia nakuhakikishia.

I dedicate this thread kwa watafutaji wote wasiochoka na wenye malengo na wasioridhika na biashara moja kiufupi kwa wapiganaji wote waliopo ndani ya JF amu MAMA nakuaminia sana sana,najua huchokagi wala hujawahi kuchoka,ongezea na hiii.
 
Makala murua Sana hi muhimu watu waisome na waitafakari.

Unapatikana wapi tukutane tunywe hata juice leo hii.

Maana nimebakiza 600,000/= nahitaji kuiweka sehemu nikae mwenyewe nife nayo. Inabidi tukae tubrain storm Location nzuri ya kuitupa hii laki 6 yangu.

Mimi nakaa Sinza Mori.
 
🖒🖒🖒umeigusa kabisa business yangu na mwanangu Zero IQ hongera mleta mada

Nimeifanya hii business since 2015 almost ulichoongea ni ukweli 98%

Ila nili copy hii idea kwa msanii @SHETTA

Nilimskia anasema yeye ana vibanda 10 vya chips hapa mjini

Mi nkasema ngoja nitest nikaanza maeneo ya kawe ukwamani

Hakika.
 
Asante sana mkuu. Undefeated kwenye masuala ya small business
Asante kwa kushukuru mkuu na siku zote amini amini

nakwambia biashara ndogo ndogo ndizo zenye pesa

Mfano halisi wa biashara kubwa yenye faida ya kiduanzi

ni GESI,unanunua mtungi mdogo 16,000 halafu unauza 17k -18k

Faida ya mtungi mmoja ni 1000,2000-3000,wakati mtaji wa 16,000

nikienda sokoni nikanunua mihongo ya 10,000 Nikauza yote Faida skosi 15,000.

Hapo mtu akimuona muuza mitungi ya gesi anamuona ni Boss kuliko muuza mihogo

wakati kiuhalisia muuza gesi ana hali mbaya leo kesho anatamani Siku ya unyakuo ifike anyakuliwe tu.
 
Anyways, Mimi ni mgeni Dar ndio maana nikaanzisha thread ya kuuliza sehemu yenye center nzuri kwa ajili ya kufanyia biashara kwenye Uzi huu hapa Maeneo/Miji/Centers zinazokua kibiashara kwa kasi sana hapa Dar es Salaam

Lakini Kama kawaida response imekuwa ya kurithisha ingawaje sikuwa specific na biashara ninayotaka kufungua.

Ila kwa Sasa nataka nikomae kwenye chips niwe na mabanda almost 5 hapa mjini niyaweke sehemu potential yenye mzunguko mkubwa wa watu then nitoe quality service afu nipenetrate market kwa strategy ya price.

Kwa kuwa Ni mgeni naomba mnisaidie kunipa location zenye watu kibao.. nikakomae nao fasta. Nahitaji ndani ya mwezi huu niwe nimelaunch hizi small scale investment hata moja nikisoma upepo wa kuzivurumusha zingine.

Asante.
 
Inasikitisha kuona thread haitembei, Kweli wabongo sio aggressive when it comes to hustling and money making issues.
Kuna thread zinahitaji JAM na kuna thread zinahitaji tafakuri

sio kila thread lazima mtu atie neno mkuu,wengi sana ni wasomaji

amini nakwambia nina ushahidi ktk hilo 100%,wakat mwingine thread inatakiwa ipoe.

kusiwe na kelele mingi mingi maana kuna kelele zingine zinatoa watu nnje ya mada kbsa.
 
Sawa nadhani tushauriane maeneo potential Sasa kwa nyie wenyeji.. wapi Location zinafaa kwa biashara za Namna hi?
 
Anyways, Mimi ni mgeni Dar ndio maana nikaanzisha thread ya kuuliza sehemu yenye center nzuri kwa ajili ya kufanyia biashara kwenye Uzi huu hapa Maeneo/Miji/Centers zinazokua kibiashara kwa kasi sana hapa Dar es Salaam

Lakini Kama kawaida response imekuwa ya kurithisha ingawaje sikuwa specific na biashara ninayotaka kufungua.

Ila kwa Sasa nataka nikomae kwenye chips niwe na mabanda almost 5 hapa mjini niyaweke sehemu potential yenye mzunguko mkubwa wa watu then nitoe quality service afu nipenetrate market kwa strategy ya price.

Kwa kuwa Ni mgeni naomba mnisaidie kunipa location zenye watu kibao.. nikakomae nao fasta. Nahitaji ndani ya mwezi huu niwe nimelaunch hizi small scale investment hata moja nikisoma upepo wa kuzivurumusha zingine.

Asante.
Kwa vile wewe ni mgeni usianze na mabanda ma5 anza moja kwanza ndani ya mwaka then ujiongeze

Afu tembelea maeneo tofaut tofaut we mwenyewe ujue changamoto na potential ya kila eneo
 
Anyways, Mimi ni mgeni Dar ndio maana nikaanzisha thread ya kuuliza sehemu yenye center nzuri kwa ajili ya kufanyia biashara kwenye Uzi huu hapa Maeneo/Miji/Centers zinazokua kibiashara kwa kasi sana hapa Dar es Salaam

Lakini Kama kawaida response imekuwa ya kurithisha ingawaje sikuwa specific na biashara ninayotaka kufungua.

Ila kwa Sasa nataka nikomae kwenye chips niwe na mabanda almost 5 hapa mjini niyaweke sehemu potential yenye mzunguko mkubwa wa watu then nitoe quality service afu nipenetrate market kwa strategy ya price.

Kwa kuwa Ni mgeni naomba mnisaidie kunipa location zenye watu kibao.. nikakomae nao fasta. Nahitaji ndani ya mwezi huu niwe nimelaunch hizi small scale investment hata moja nikisoma upepo wa kuzivurumusha zingine.

Asante.
Nakupa Topography ya Dsm Makonda alikuwa anasema ina shape ya kiganja sisi watu wa Geography tunaita Centripetal pattern...watu wana flow kutoka sehemu kuu 6 kwenda katikati ya mji na kurudi jioni movement hiyo ndio inatengeneza Centre kuu kama tano Dsm kutokea kila balabala.

1)Karikooo (Cantre Kuu 1)
2)Makumbusho (Centre Kuu 2)
2Mbagala Rangitatu (Kilwa Road)
3)Gongo La Mboto (Pugu Road)
4)Mbezi Mwisho (Morogoro Road)
5)Tegeta (Bagamoyo Road)
6)Kigamboni Ferry (Non Road)

Centre Zingine
_Tandika Sokoni
_Magomeni Mapipa
_Buguruni

Ukitaka kuwa na BBQ 3...4...5 sehemu hizi ndio sahihi kama hapo MBAGALA RANGI TATU wanauza masaa 24.
 
Principle kuu.

Biashara yenye mafanikio haisemwi.

Umiza kichwa. Hakuna mfanyabiashara aliefanikiwa kwa kuoneshwa fursa ila Kuitafuta Kwa TAABU hiyo fursa.

Na ukifanikiwa Kwenye hiyo biashara hautanyanyua mdomo kutoa siri nje.

Good evening.
 
Back
Top Bottom