Mifano ni matajiri wengi tunaowajua kina Mo, Bakhresa, GSM, ni biashara za familia na ndugu wa karibu, ni team work.
Pia kwa upande wetu watanzania wa asili ukienda kwenye masoko makubwa utawakuta wengi wanaofanikiwa ni biashara za familia na ndugu wa karibu wanapambana pamoja, ukienda ofisi zao ukichunguza vizuri kuna watu kadhaa ni wanafamilia na ndugu wa karibu.
Ni team work wanafamilia na ndugu wa karibu wana maduka Mbeya, Iringa, Moro, Dar, wakitaka kujumua mzigo wanakusanya pesa wanaagiza mzigo mkubwa kwa discount kubwa, wewe unaeagiza mwenyewe utaendelea kulalamika faida ni ndogo, bidhaa mnayouza wote elf 5 wewe unapata faida ya jero wao elf 2, wakipunguza bei unaanza kulalamika wanataka kukumaliza
Kwenye matatizo / changamoto wanafamilia na watu wa karibu inakuwa rahisi kuji organize kuyatatua ila wewe ukitaka kuvunja chawa kwa kidole kimoja utateseka mno,
Damu ni nzito kuliko maji, kufanya biashara kwa kuungana na marafiki muda wowote mambo hubadilika (kuzulumiana, kugeukana, kukosa msimamo wa malengo, n.k)