Sakata la viroba: Mselia wa Dodoma ajipiga risasi na kufa

Sakata la viroba: Mselia wa Dodoma ajipiga risasi na kufa

Mwanakili90

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,568
Reaction score
246
Mfanyabiashara mkubwa wa vinywaji kwa jumla pia na rejareja mjini Dodoma ndugu Wense almaarufu Mselia amejipiga risasi kwa kile kinachoaminiwa ni ghadhabu ya shehena yake ya viroba iliyokamatwa na serikali hivyo kumpelekea kuchukua hatua hiyo.
Bwana ametoa,Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.



Tukio ilo limetokea jana akiwa shambani kwake.

Chanzo cha kifo inasemekana ni biashara ya viroba iliyopigwa marufuku. Yasemekana alikua ameomba mkopo mkubwa sana bank na kununua mzigo huo lakini polisi wamekamata mzigo wote. Ndio imepelekea kifo cha marehemu mselia.

Rest in peace.....tuliokua na vibaa vyetu tutakukumbuka maana hata mzigo wa mali kauli ulikua unatupa.


=====UPDATE=======

Mzigo ulikua ni tani 1.5 ya viroba vyenye thamani ya mil.600 ambao umekamatwa na polisi

Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limekamata shehena ya pombe kali za viroba zilizopigwa marufuku zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa wakala mkuu wa uagizaji na usambazaji wa pombe hizo Dodoma Mselia Enterprises huku mmiliki wake Festo Mselia akijiua baada ya zoezi hilo kwa kujipiga risasi kichwani kwa kile kinachodaiwa ni msongo wa mawazo kutokana na mkopo aliochukua benki kwa ajili ya kuendesha biashara hiyo.

Msako huo wa pombe hizo zilizopigwa marufuku umeongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa ambaye aliongozana na maofisa wengine wa jeshi hilo na kukuta zaidi ya katoni 1400 za viroba katika moja ya stoo za mfanyabiashara huyo na kufanya nae mahojiano na kisha kumtaka aendelee na shughuli zake na kisha kamanda huyo akaamuru shehena hiyo isiuzwe wala kutumika akisubiri maelekezo.

Kufuatia msako huo wa polisi ambao awali ulitanguliwa na maofisa wa mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA inadaiwa kuwa mfanyabishara huyo aliamua kujiua kwa kupiga risasi kichwani ambapo kabla ya umauti kumkuta kamera ya ITV ilinasa mazungumzo yake na maofisa wa TFDA akidai kuwa amesitisha uuzaji akisubiri maelekezo kutoka kwenye mamlaka husika kuhusu nini cha kufanya juu ya pombe hizo.

Kufuatia tukio hilo baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma wamekuwa na maoni tofauti kuhusu operation ya kuondoa pombe hizo ambapo wanasema licha ya kufanyika kwa nia ya kunusuru taifa na janga la ulevi lakini wangetoa muda kwa wafanyabishara kumaliza bidhaa zao kwani awali ilikuwa ikiendeshwa kihaliali ikiwemo kulipiwa kodi na tozo mbalimbali.

Katika tukio jingine jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu wanne raia wa Ethiopia na watanzania idadi kama hiyo ambao wanadaiwa kuhusika na kuwa safirisha wahamiaji hao ambapo wote kwa pamoja wanatarajiwa kupandishwa mahakamani.

Chanzo: ITV

=====

Mapya yaibuka kifo bilionea wa viroba

WAKATI mwili wa bilionea na mfanyabiashara maarufu wa vinywaji Festo Mselia (58), ukitarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Umbwe Unana mkoani Kilimanjaro, mambo mapya yameibuka kuhusiana na kifo chake kinachodaiwa kutokana na kujipiga risasi.

Kamanda%20wa%20Polisi%20mkoani%20Dodoma%2C%20Lazaro%20Mambosasa.jpg

KAMANDA WA POLISI MKOANI DODOMA, LAZARO MAMBOSASA.


Mambo mapya yaliyoibuka yakihusishwa na chanzo cha kifo hicho ni pamoja na usumbufu alioupata polisi, kutuma ujumbe wa kumuaga mkewe na kumpigia simu mdogo wake mara tisa bila kupokewa muda mfupi kabla ya umauti kumfika.

Akizungumza na Nipashe jana, mdogo wa marehemu huyo, Anthony Mselia alisema mwili wa marehemu baada ya kufanyiwa uchunguzi, umekutwa na matundu matatu ya risasi kwenye maeneo ya chini ya kidevu.

"Mazingira yanaonyeshwa kwamba 'brother' (kaka) hajauliwa na mtu, yaani sielewi ni kitu gani kilichomsibu," alisema.
"Lakini kulikuwa na taharuki kuhusu suala la pombe kali aina za viroba, lakini hakuna kitu alichowahi kuniambia zaidi ya kulalamikia suala hilo.

"Tangu siku ya kwanza alipokamatwa Machi 3, mwaka huu, alinipigia simu na kuniambia kwamba serikali haioni namna yeyote ya kuongeza muda na hii ilitokana na kwamba alikuwa na mzigo mkubwa wa bidhaa hiyo katika stoo zake zaidi ya tatu tofauti wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni moja na viroba ndio vilivyokuwa na mzunguko mkubwa wa biashara na ndivyo vilikuwa vimekamata fedha."

Akisimulia zaidi, mdogo huyo wa marehemu alisema kaka yake aliwapeleka polisi zaidi ya stoo tatu.

Alisema kuwa kabla kaka yake hajafikia uamuzi huo Machi 7, yeye alifika nyumbani kwake na kumuaga kuwa anasafiri kwenda Moshi.

"Nilimsalimia na kumuaga kwa safari na akaniruhusu kuondoka na hakuonekana kuwa na mawazo wala kitu chochote alikuwa 'happy' (na furaha) tu. Nakumbuka aliniambia kwamba mdogo wangu ukienda uwahi kurudi kutoka Moshi kwa kuwa mimi naishi hapa hapa Dodoma," alisema.

Aliendelea kueleza kuwa anaamini kaka yake hajafikia uamuzi huo kutokana na kuwa na madeni aliyokuwa nayo ambayo alidai alikuwa ameshayalipa kwa kiasi kikubwa.

"Kwa mfanyabiashara mkubwa kama Mselia ambaye ana mzunguko mkubwa wa biashara, lazima kutakuwa na watu wanaoleta mizigo lakini siyo kesi ya yeye kufikia hatua hiyo, mimi mpaka sasa hivi akili na aliponipigia simu na kulalamika kilichompelekea kufanya uamuzi ni suala la viroba."

Alieleza kuwa awali polisi, maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) walifika dukani kwa kaka yake kumhoji na kumkagua na kwamba marehemu alitoa ushirikiano na kuwapeleka kwenye stoo zake na kuwaonyesha mzigo wote ambao alizuiwa kuuuza.

Alisema kuwa maofisa hao baada ya kumaliza kukagua, waliweka stika lakini alikuwa bado analalamika kwanini mzigo wenye thamani kubwa ya fedha ufungiwe ndani, jambo ambalo lilikuwa linampa wakati mgumu.

Alisema mzigo huo licha ya kuzuiwa kuuzwa, bado umo kwenye stoo zake.

SIMU MARA TISA
Mdogo huyo wa marehemu aliendelea kusimulia kuwa baada ya kuagana na kaka yake, hakuwasiliana naye lakini baada ya kufika Moshi na kutaka kumjulisha kwamba amefika salama, alibaini kuwa kaka yake alikuwa amempigia simu mara tisa bila kumpokea.

"Muda mfupi baadaye nilipigiwa simu na polisi kwa namba zilizoishia 71 akiuliza kwamba 'wewe unamfahamu Mselia?',

nikamwambia ni kaka yangu, akaniambia mimi ni askari, kaka yako amejipiga risasi, nikamuuliza amejipiga au imemfyatukia bahati mbaya?

"Akasema amejipiga mwenyewe, tafuta watu waende ‘General Hospital’ (Hospitali ya Rufaa ya Mkoa) kwa ajili ya kumpa msaada."
Alibainisha kuwa baada ya taarifa hiyo, alimpigia mke wa marehemu na baadaye wakawapigia marafiki wa karibu wa familia na wakaungana naye, lakini muda mfupi baadaye akapigiwa simu kuwa kaka yake amefariki.

Alidai kuwa marehemu alikuwa anamshirikisha matatizo yote ya kibiashara.

KWAHERI
Mdogo huyo wa marehemu pia alidai kuwa kaka yake alitumia ujumbe mfupi wa maandishi kwa mkewe uliosomeka "kwaheri" muda mfupi kabla ya tukio la risasi, lakini mke wake hakuutilia maanani akidhani alikosea kuutuma kwake badala yake alikuwa anamuaga mtu mwingine.

"Lakini baadaye, baada ya kupata taarifa kuwa amejipiga risasi, aligundua kuwa kumbe alikuwa anamuaga," alisema Mselia.

"Kinachoonekana ni 'harrasment' ya polisi kwa sababu polisi walifika mara ya kwanza, ya pili na ya tatu, Mselia wa watu maskini hapendi kusumbuliwa."

KAULI YA POLISI
Akizungumza na Nipashe kwa simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, alidai maganda ya risasi yaliyokutwa pembeni ya mwa mwili wa marehemu yalitumiwa na marehemu wakati akijaribu kujiua.

“Maganda yale ya risasi aliyatumia kujipiga mwenyewe, unajua alipokuwa akijipiga nadhani hakujilenga vizuri na hii ni kutokana na kupaniki, alijipiga kwenye shigo ikatokea mdomoni, hakufa na yeye alitaka afe sasa kutokana na kujipiga kule alijipiga risasi tano," alidai Kamanda Mambosasa.

Mfanyabiashara huyo alijiua juzi shambani kwake Msalato Manispaa ya Dodoma baada ya kuhojiwa na polisi kuhusu shehena ya viroba aliyokuwa nayo yenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni moja.

Chanzo: Nipashe
 
Du!aisee hii government itapata dhami sana
 
Mfanyabiashara mkubwa wa vinywaji kwa jumla pia na rejareja mjini Dodoma ndugu Wense almaarufu Mselia amejipiga risasi kwa kile kinachoaminiwa ni ghadhabu ya shehena yake ya viroba iliyokamatwa na serikali hivyo kumpelekea kuchukua hatua hiyo.
Bwana ametoa,Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
Mkuu una uthibitisho wa hii taarifa mkuu
 
Mwache ajipige risasi,serikali ilitoa muda wa kutosha alitakiwa atumiwe common sense
Wengine dhamira inawasuta huyo na yule mkulima wa bangi wengine kau Kama kina Makonda, hawana hata mshipa wa aibu.

Kutoa uhai wa mtu (hata kama ni wako mwenyewe) ni dhambi kubwa sana. Naomba wote mnaofikwa na matatizo tafuteni ushauri nasaha na ujue hauko peke yako. Tumieni wanasheria kuwatetea.
 
Me huwa sielewi mtu unajiua vip kwa sababu nya mali. Hamna kitu kibaya kama kushikanisha nafsi yako na mali. Tulikuja duniani tukiwa hatuna chochote na hivyo tutaondoka tukiwa watupu.

Tuwe na ushirika na Mungu na jamii inayotuzunguka. Hii ndiyo furaha kamili. Furaha ya kweli si katika mali bali katika kumuabudu Mungu na wapendwa wako katika familia, mke,mume, watoto, wazazi, na hata marafiki.

Tuache kuabudu mali, hii ndo inapelekea watu kuuana, kulogana, kudhulumiana, kufanya ndugu mandondocha n.k. Laiti tungejua yule unayemuua, au kumdhulumu au kumfanya ndondocha ndiyo furaha yako, mtu asingefanya vile.

Nasaha hizi ziwaendee wote washakamanisha nafsi na mali.
 
Mwache ajipige risasi,serikali ilitoa muda wa kutosha alitakiwa atumiwe common sense
R.I.P Wense. Muda ulikuwa mfupi sana, unapotoa tangazo la namna hiyo hata wanunuzi wa jumla nao wanapunguza kiasi wanachonunua. Mimi nafikiri ingekuwa sawa kama wangepiga marufuku kutengeneza au kuingiza bidhaa hiyo na wangeacha bidhaa iliyoingizwa/iliyozalishwa mpaka iishe yenyewe mtaani. Lakini kwa amri ya kusitisha ghafla namna hii bila sababu ya msingi hainingii akilini. Kutoa amri kusalimisha bidhaa polisi ambazo bado zipo kwenye maghala haisaidii kitu, labda hao polisi wangekuwa wanatoa refund.. Huu mimi naona ni ubabe tu usio kuwa na tija.
 
Mkuu una udhibitisho wa hii taarifa mkuu
Ni kweli amejipiga risasi chini ya kidevu huko shambani kwake Msalato, akakimbizwa Hospital ya mkoa na kufariki saa usiku, viroba kukamatwa ndio chanzo, lkn alivihifadhi na utaratibu ungefanyika wa ku repark kwenye ujazo utakiwao, habari za chini ni deni la Benki na Kodi ukichanganya na udhibiti wa mianya kubanwa kulimchanganya akakksa mshauri, kwani ana majengo mawili ya ghorofa shamba nk ambayo yangefuta kabisa hilo deni la Benk na viroba, 347/milioni
 
Back
Top Bottom