Ni wakati wa kutafakari wewe binafsi umefanya nini na utafanya nini kusaidia Nchi yetu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,754
Mawazo zaidi ya kibinafsi hasa kwa vijana kutoka moyoni.

Mimi kama Mtanzania ambaye ni diaspora najaribu sana kujitafakari na kuhakikisha najua nilikotoka na sisahau nilikotoka. Lakini swali kubwa kubwa sana ambalo kila Mtanzania anatakiwa kujiuliza ni je leo ukienda mbele ya haki kwa Mungu akakuuliza je umefanya kila kitu kwa uwezo wako wote kusaidia jamii yako na wale ambao hawajabahatika na wenye shida? sina uhakika kama nimefana kila kitu kwa uwezo wangu.

Tumekuwa wepesi wa kukaa pembeni na kusubiria wengine wafanya kazi zetu kwenye kupiga kura, kupuuza unyanyasaji, kupuuza rushwa, umasikini ambao tunauona kila siku na matabaka makubwa sana ambayo yapo kwenye jamii zetu

Kwanza nimeamua kusema ukweli hata kama kwenye mitandao. Jamii yetu ya Watanzania ambayo wengi sana 80% ni chini ya miaka 30 inahitaji mawazo na kujua ukweli badala ya kuwadanganya kila siku

Nashauri tujitolee zaidi kusaidia jamii zetu na sio kila siku kugombana kwenye mitandao kuhusu wanasiasa. Wakati mwingine tuongelee mbinu za kupata kazi, kuwashauri vijana wetu wasome nini kwa nyakati hizi za dunia na kupeana deals badala ya kuongelea wasanii pekee na wanasiasa.

Vijana zetu niwaambie ukweli pesa pekee na kuwa na kazi nzuri, nyumba, na hata wazazi wako kuwa sehemu nzuri havitoshi kukupa furaha kama unavyofikiria. Furaha ya kudumu utapata pale ambapo unasaidia au kufanya kitu cha kusaidia mfano huyu jamaa aliyeanzisha mtandao anafuraha kuona jinsi ambayo anasaidia jamii hata kama ni biashara. Mengi kama mnakumbuka alikuwa anasaidia jamii ndiyo inampa furaha, Bill gates baada ya kupata pesa nyingi sasa anapata furaha kusaidia watu masikini hata maraisi wastaafu baada ya muda wanagundua vyeo pekee havijaweza kuwafurahisha

Niwape mfano wangu binafsi wa ukweli. Bahati mbaya mke wangu mpenzi aliumwa ugojwa ambao haukuweza kupona. Kwasababu ya kazi yangu na sikuwa na tatizo lolote la pesa na nipo US sikuweza kukubali hili kirahisi. Nilitafuta team na tulikuwa na madaktari mabigwa na team zao wasio pungua kumi, teknologia ambayo hata nyingine zilikuwepo US tu, kampuni yangu ya bima ya afya iliniambia watatumia kiasi chochote kile kujaribu kuokoa maisha ya mke wangu.

Tulifanya opereshi zaidi ya tano ya kwanza tu ilikuwa kubwa na kugharimu $250,000 lakini kama nilivyosema pesa haikuwa tatizo kwasababu kampuni yangu ya kazi ilinitafutia bima ya juu kabisa. tumepigana kwa kila njia kwa maka zaidi ya miwili na zaidi ya $4M ilitumika na kila aina ya teknologia ambayo inajulikana tulitumia. Niliomba misa karibu kila wiki mbili zaidi ya makanisa 3.

Niliambiwa nitoe pesa za watoto wa madrasa huko Bagamoyo kuwafutarisha nilifanya hivyo kwa watoto zaidi ya 15 kwa mwezi mtukufu. Nilitoa kila aina ya sadaka na kuomba kila siku. Baada ya miaka miwili na nusu mkwe wangu alifariki. Nilijiuliza sana sana Mungu unaaka nifanya nini, nikupe nini tena. Nilimshukuru Mungu kwa kunipa uwezo wa kujitegemea lakini magari na nyumba na hapa pesa bank hazinipi furaha, furaha yangu ilikuwa napata nikiwa na mke wangu, tunasafiri pamoja, tunapanga vitu pamoja na kuchekeshana.

Ningekuwa na uwezo ningetoa chochote kumrudisha mkwe wangu lakini kuna vitu ambayo ni uwezo wa Mungu pekee. Pesa na hata matakwa yetu haviwezi kusaidia. Nimekueleza haya yote kukupa ukweli kama wewe ni mmoja ya wale ambao wanafikiri pesa, nyumba na magari yatakupa furaha.

Kitu ambacho nimejifunza kusaidia ndiyo kutakupa furaha. Matukio ya kufiwa na kupoteza uwapendao huwezi kuzuia hata uwe wapi au uwe na uwezo gani. Lakini kwenye kusaidia usiache kusaidia ndugu na marafiki wa kweli kuna wakati utafika hao ndiyo wataweza kukusaidia. Kwenye misiba ndiyo unajua nani ni rafiki na umuhimu wa ndugu. Usione aibu kufanikiwa kwenye maisha lakini mafanikio yako uyatumie kuinua wengine hii ni pamoja na kusaidia ndugu na jamaa kwenye elimu zao, kusaidia wazazi wako na wapedwa na kutoa sadaka kwa kusaidia wale ambao wana matatizo.

Kwasasa mfano nimeanza mpango wa kuchukuwa watoto yatima wachache nianze kuishi nao kama watoto wangu kabisa. Vilevile vijana imekuwa kama tabia siku hizi kuishi fake life tunakuwa na jamii wa waongo na washabiki. Jaribu kijiendeleza badala ya kulalamika kila siku. Usiogope kutafuta mtu ambaye kafanikiwa na kumuomba awe mshauri wako usimuogope kuna watu wengi sana wanataka kusaidia watu. Hii inaweza ikawa boss hata kama ni kampuni nyingine, wafanyabiashara wenye hekima na wengine wowote ambao wanafanya ambacho unapenda. Jaribu kujua kipaji chako itakusaidia.

Vilevile vijana wengi nawashauri jamii yetu hauwatendei haki wanawake. Tumekuwa na mfumo dume na kuturudisha nyuma sana kama nchi. Ni ngumu kuona kijana wa kiume kumfuata Mama mwenye mafanikio na kwenda kuomba ushauri. Akili haina jinsia kuna wanawake wengi sana ambao wanapenda kitu ambacho na wewe unapenda lakini tumekuwa na utamaduni wa kuangalia sketi pekee.

Kwenye jamii zetu hata kwenye matukio tunajitenga hivyo yule Mama mwenye akili huwezi hata kuongea naye na kumuuliza chochote maana wengi hatuwezi kukutana nao. Hivyo vijana sio kila kitu cha kuiga kutoka kwetu mimi nipo kwenye umri wa kati 40's sasa ni mtu mzima na ndiyo maana nashauri vijana wadogo zaidi.

Kwa wale umlioa kuna ambao wanatamani maisha yako jisaidieni kujiendeleza mfano usiache kumsaidia mke wako au mume wako kujiendeleza kielemu, usiogope kama mwenzako anajua kitu zaidi kama biashara hata kama ni mwanamke badala yake msaidie kwa manufaa ya familia nzima. Msiogope mwanamke kutengeza pesa zaidi kama wote mnajichukulia kama team moja.

Usisikilize maneneo ya mitandao hata nayosema mimi kama moyoni unajua yanapotosha lakini mazuri yachukuwe. Familia yako usikubali iendeshwe na marafiki, wazazi au kujali watu watasema nini! watu wengi hata ndugu wanapenda sana kuona drama kwa wengine hivyo kuwa makini kwao ni kama the comedy show.

Vijana pamoja na kwamba kwa wakati mwingine tunawapiga madongo sana kuwa ni wavivu eleweni nyie ndiyo mtatusaidia kutoa nchi yetu kwenye umasikini. Pingine rushwa, piganieni uhuru wa kila mmoja, pingine unyanyasaji wa kijinsia. Mjue tunawapenda na kuwategemea sana sana kwenye nchi yetu ya Tanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom