Bi dada... Utafanya nini? Mmeo anatembea na binti wa Salon...!

uondoke uende wapi,kwanza mapungufu yaliyosemwa wewe mwenyewe unakiri ni ya kweli,cha kufanya ni kuyafanyia kazi mapungu mr huenda akajirekebisha!!!

Inategemea na mapungufu yanayoongelewa, kama wanasema nimepigwa pasi, narekebishaje hapo?
 
nyie ndo mnaokewa mitego na kunasa kirahisi
ni nadra sana kwa mashangingi ya mjini watembee na mtu wasimjue mkewe
inawezekana hiyo ni set up.....ili uvunje ndoa wajisogeze....

nilikwenda salon siku moja mdada akafanya hivyo baada ya mwenye mume kuondoka akasema nimemrusha roho nia yake hasa ilikuwa kuvuruga ndoa yao.......mara nyingi wanafanya hivyo wakiwa na uhakika muhusika yupo hapo
 
jamani Mbu si lazima kila kitu ushirikishe wazee.....unadeal nao tu hao............


......kwakuwa mke amethibitisha sauti, maneno na ukweli uliodhahiri
Anavyoaibishwa na mumewe, hana budi kuita "wazee wa busara" kulizungumza
Hili mbele ya mumewe. Huyo mume amechemka mbaya.
 
Last edited by a moderator:
Ila kwa kweli, sina uhakika na reaction yangu itakuwaje, maana kuna vitu unajikuta unafanya unakuja kujutia baadaye. Kama nitajikuta na ujasiri, basi nitaendelea kuusikilizia msuko (kama nilikuwa nasuka) mpaka nisikie mwisho wa hizo hadithi.
 
Upo Salon, mumeo anajadiliwa na wasichana waliopo hapo Salon... Hawajui kama wewe ndo mkewe...

Mmoja wao anatembea nae... full vicheko, full kumpigia simu na kuweka loud speaker. Unamsikia mumeo anajiachia tu... Hajui kama kawekwa kwenye loud speaker... Wanakata simu wanacheka mbaya! Mbaya zaidi, wanasema jamaa anamponda mke wake ile mbaya, wanataja na mapungufu yako
ambayo kwa asilimia kubwa ni ya kweli....

Je..? Utafanya nini kama ni wewe...?


kwanza hapo kwenye red itabidi pafanyiwe kazi inawezekana ikawa sababu kwa mume kwenda huko
 
.........wanasema when your enemies makes mistakes, don't interrupt them..........


yaani hao mbona unawatafutia dawa tamu tu?

tena wanawake wamepewa moyo wa uvumilivu.....unavumilia na mume unamchekea huku ukimuandalia dawa.....ukimalizana nae hatothubutu kurudia huo ujinga....na huyo mwanamke ukimalizana nae hatothubutu kuiba hadharani............



 
Huo si ushahidi tosha?

Sidhani kama nitaweza endelea fanya nilichokuwa nafanya hapo salon.
Nitarudi home na kujipanga kuondoka, sitakuwa hata na muda wa kumuuliza
ni kuend hiyo ndoa tu. Saana nitaishare hiyo incident humu with a new ID
ofcourse.

Au with the same ID ila unaanza,"kuna rafiki yangu yamemkuta ...."
 
Nakubaliana na wewe Kaunga....

Tatizo ni kwamba watu wanasahau kanuni za kutembea nje ya ndoa...

Wataalamu wanasema kuwa ni mwiko kuongea habari za mke wako mbele ya hawara na pia huyo mtu wa nje hana ruhusa kuwasaliana na wife. Akikaidi hayo, lazima alimwe red card bila huruma...

Inapofikia mwanamume anamwaga kila kitu cha mke wake kwa hawara basi kapoteza sifa zote za kuwa mume...

Babu DC!!
Asprin Likes This......!!
 
Japo nina masharubu lakini nachangia hivi Huyo dada anayetamba na mume wa mtu anamapungufu ni mshamba na malaya wa kiwango cha chini, sio mstaarabu na hajui kula na kipofu, na huyo mume anayemponda mkewe namwita *****, limbukeni wa mapenzi na mambo ya mapenzi ya nje hayajui, Namshauri huyo mwenye mume amdharau huyo dada pale pale na angeamua kupiga simu pale pale salooni na yeye aweke loud speaker nakuongea na mumewe na kumbembeleza aje hapo saloon,ili kumuumbua mumewe ili watu wote waliokuwa pale wauone ushamba wa pande zote mbili
 
Mkwara kote kote unasaidia

Fikiria unagombana na mumeo tu. Unadhani ataenda ku share varangati ulompa na kimada wake. Thubuthu! Aonekane dhaifu?

Matokeo yake nyie ndani kunawaka moto, mwenzenu anapiga miluzi. Na mumeo hamuachi ng'o; kwani miugomvi yenu ya ndani yeye wala hana habari nayo. Sana sana ndio anazidisha mapenzi...unaachwa jumla. Maana mume akifika ndani moto...akienda nje..'darling achana na huyo kichaa'. Utakumbukwa wewe? Lazima moto uwe kote kote ili achuzi (achague). Na ni obvious atachagua kuiokoa ndoa yake.

Ukilianzisha kote kote lazima huyo kimada achanganyikiwe ndio pale atakapotaka nae kutunisha kifua na kusahau position yake. Lazima apigwe chini walahi.

Maana ataanza mimi mkeo ananitukana sikubali...ntamtia adabu...mwambie kabisa anikome...au atanijua mimi nani...Hajaachwa tu hapo?
Lazima uwavuruge wote ili uwagonganishe vichwa.





.........wanasema when your enemies makes mistakes, don't interrupt them..........


yaani hao mbona unawatafutia dawa tamu tu?

tena wanawake wamepewa moyo wa uvumilivu.....unavumilia na mume unamchekea huku ukimuandalia dawa.....ukimalizana nae hatothubutu kurudia huo ujinga....na huyo mwanamke ukimalizana nae hatothubutu kuiba hadharani............



 
Upo Salon, mumeo anajadiliwa na wasichana waliopo hapo Salon... Hawajui kama wewe ndo mkewe...

Mmoja wao anatembea nae... full vicheko, full kumpigia simu na kuweka loud speaker. Unamsikia mumeo anajiachia tu... Hajui kama kawekwa kwenye loud speaker... Wanakata simu wanacheka mbaya! Mbaya zaidi, wanasema jamaa anamponda mke wake ile mbaya, wanataja na mapungufu yako ambayo kwa asilimia kubwa ni ya kweli....

Je..? Utafanya nini kama ni wewe...?


Nashauri aripoti abuse kwa moderator wa ndoa yao...labda jamaa atakula ban.
 
Dawa yake huyo unampigia hubby unamwambia gari (kama una lako) imegoma kuwaka aje akuchukue. Afu akifika unamlazimiasha aingie ndani afu unampa tongue kiss ndeeeefu. Kisha mnatoka. Afu mkifika home ndo atajuta kukufahamu. Ile kiss ni action tu kuwa you can have him wherever, and whenever you want.

Siri ya hii mdogo wangu ntakuambia wakati unaingizwa mkoleni. Ila utashangaa, dawa unampigia baba chanji unamuweka loudspeaker unamuambia niko na flani tunapiga stori. Ukirudi home, hata umuambie akufulie vinasa atafua! Halafu ukishamaliza kum-mess up ndo unamuacha!

Hata kama simba inacheza na Chelsea, hukimbii mechi! Unaingia uwanjani unawafanya walau wakafue jezi zao, eboo!

Hizi actions hivi utaweza zifanya? for who?
Wakati moyo wako uko matopeni unagaragazwa, tena na mwanamke asiyejiheshimu??

Mi ndo maana huwa nasema, wanamme waangalie sana watu wanaocheat nao
Maumivu ya kuchitiwa kwa mwanamke decent na mapepe ni tofauti sana.

Kwangu mie, the best option ni kuondoka kama naenda kutema mate
Naenda home kabisa.

Reaction ya kumwonyeshea ya aina yeyote ni ishara tosha kwamba 'ujumbe wa loudspeaker' umekupata kisawa sawa. Kweli uanza shindana na mwanamke anacheat na mmeo?? To me hell no, huwa sijishushi, na hadi kukuoneshea hivyo ujue kuna loop hole ya kukudharau mmeo kaitengeneza.

Kuna mdada anacheat na mme wa mtu, huwa akimuona mke wa huyo baba anaondoka kabisa eneo hilo, sasa huyu anayeweza na kupiga simu, na loudspeaker??? afu na wewe ufanye Actions??
 
Nakuepnda kwa hili
Angalau nimehakiki mie sio kichaa

Eti unamwonyeshea kimada wa mme?? Ili iweje??

huko mtaani zaidi ya kuangaliana kiaina na kushikana mikono tukiwa matembezini na kukimbizana hakuna la ziada. siwezi eti kumkiss vya chumbani ili watu waone............. yule ni mume wangu na kuna heshima mbele za watu. ni kweli watu wakiona watu wanakiss barabarani lazima wajue ni kimada, kama mkeo hamuwezi kufanya hivyo, pamoja na kila kitu kuna element za heshima
 
Kwa hiyo kama mmeo kakushushia heshima, na wewe unaenda imaliza ile ndogo iliyobaki???

Hivi unajua unaweza mfanyia kimada mbwembwe zote
Lakini mwisho wa siku usipate hata hiyo 'Satisfaction'??

Inategemea unachopigania ni nini??
Kama hisia zako zishavurugwa hata undava mie naona hausaidii
Ila kama ni 'material' yaweza saidia labda

Anyway, kila mmoja na fomula yake

Unadhani kulianzisha ni lazima ufunge kibwebwe na kuanza kupigana mtaani kama wafanyavyo wamama wa uswahilini?

Afu kuhusu heshima...kuna heshima gani kwa mtu ambaye anakubonda kwa small house?; kuna heshima gani na ukipita mtaani watu wana kung'ong'a? Hakuna heshima yeyote ni undava undava...na haondoki mtu...kama kuondoka unaondoka kwa convenience yako.

Mwanaume akishaanza kuchukua machangu hakuna heshima ni ugumu tu na kuvaa mask usoni.
 
Back
Top Bottom