Izzi
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 553
- 1,107
Hakuna asiependa pesa (Hapo sasa nimekuwa semaji la binadamu wote), na kama yupo basi ana raha sana. Tutakubaliana pia, hakuna asiependa njia za mkato (shortcuts) za kurahisisha mambo. Njia mojawapo ya mkato ni kutumia uchawi kupata kile unachokitaka.... nimekua katika jamii ambayo inaamini ili utoboe kimaisha ni lazima utumie uchawi. Na mtu yeyote akitajirika basi lazima atahusishwa na uchawi 'bai difoti' (by default). Lakini, ambacho sijawahi kusikia ni kwamba kuna mchawi mmoja amekomba pesa zote kutoka benki fulani. Au yupo sema mimi ndio sikusikia? Kama hayupo, kwanini hizi 'softiwea'(software) za kichawi hazitumiki kubeba pesa kutoka benki?
Kuna ambao wanasema mchawi hawezi kutumia uchawi wake kuvuta pesa kutoka benki, kwasababu benki zenyewe zinalindwa na Uchawi 'Pro Max'/ Majini 'first class'. Kundi jingine kubwa zaidi ni la sisi ambao hatuelewi kwanini wachawi hawawezi kuvuta pesa kutoka benki. Inasemekana pia, mchawi hata akija kwako usiku kukuroga/kukukaba/ kukunyonya damu/ kukuchezea, halafu ukawa umeweka pesa hata pembeni ya kitanda kwa mfano, atafanya vyote lakini hawezi kuchukua ile pesa.
Nilisoma mahali fulani wanasema uchawi sio halisi, ni viinimacho tu - manaake uchawi hauna madhara/matokeo kwa ambae haamini au haogopi uchawi. Kwa lugha rahisi uchawi ni mchezo wa kisaikolojia tu, hauna uhalisia kwa hiyo hauna madhara kwa vitu vinavyoonekana/ kushikika, isipokuwa panapo imani na hofu; Ukiamini basi kitatokea ulichokiamini, na ukiogopa lazima madhara yatokee kwasababu ya hofu yako (Kumbuka: Sio kwasababu ya uchawi!)
Bahati mbaya sijawahi kumpata mchawi anijibu maswali yangu, kukidhi udadidi wangu tu. Lakini tuna jukwaa lililosheheni watu wenye asili tofauti tofauti, watu wenye fikra tunduizi, watu makini kabisa wenye uzoefu na masuala anuai. Naombeni mnisaidie kufahamu, wachawi wanakwama wapi kubeba shekeli zile kutoka benki?
Naomba kuwasilisha.