Benki ya Dunia yaisifu Tanzania kusimamia Uchumi kwa umahiri

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
BENKI ya Dunia imeimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayopata fedha kutoka kwenye taasisi hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi za Afrika.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania, unaoongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwenye Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Dkt. Ngaruko, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya Dunia katika ukanda huo, alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa sera za uchumi na fedha ambapo licha ya changamoto za UVIKO 19 na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine, tathimini ya Benki hiyo inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika.

“Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano kwa usimamizi mahili wa masuala ya uchumi mpana, si tu kwa nchi za Afrika Mashariki, bali kwa nchi za Afrika, ambapo kiwango cha ukuaji uchumi cha wastani wa asilimia 5.4 ni cha juu, na ninawapongeza sana” alisema Dkt. Ngaruko

Aidha, alipongeza uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia na kuahidi kuwa Benki yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kukuza uchumi na kuwaondolea umasikini wananchi wake kwa kusaidia fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii pamoja na kutoa misaada ya kiufundi.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alimweleza Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika, Dkt. Floribert Ngaruko, kwamba uchumi wa Tanzania unazidi kuimarika na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua muhimu kuhakikisha uchumi unazidi kuimarika na kuleta ahueni kwa wananchi.

Alifafanua kuwa katika kipindi cha robo tatu robo ya mwaka 2022/2023 uchumi umekua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.8 katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliotangulia 2021/2022 na kwamba kutokana na mipango kabambe iliyowekwa na Serikali uchumi utakua zaidi hadi kufikia wastani wa zaidi ya asilimia 6.3 miaka michache ijayo.

“Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi makini wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, tunaahidi kuwa tutasimamia na tutatumia fedha hizo kwa umakini ili kufikia malengo yaliyokusudiwa Alisema Dkt. Nchemba

Mpaka sasa Benki ya Dunia imewekeza zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 7.2, sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 16.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi zaidi ya 29 nchini Tanzania ambapo kati ya miradi hiyo, 24 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 6.41 ni ya kitaifa na mingine 5 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 0.75 ni ya kikanda.

Truth must told, huu ndio ukweli halisi Tanzania inafanya vizuri sana achilia mbali na washenzi wezi wanaohujumu taifa hili, wezi kila mahali huwa hawakosekani, tuwadhibiti kwa vitendo ili taifa letu liwe mfano bora zaidi.
 
Kuna watu hii nchi wameifanya mali yao.hawana huruma watoto wanasomea taa za barabarani mijitu ipo tu kukusanya na kuweka mabilioni nje ya nchi.
 
Hawa nao wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa hili tujisahau na tujipendekeze watupige na kitu kizito kichwan kwa kutukopesha mikopo isiyo na sura wala miguu
 
Kama Tanzania ni nchi ya kupigia mfano kwa matumizi bora ya fedha, basi Afrika imeoza!
Hata hizo Japan, Hong Kong wapigaji wapo Isipokuwa wanashughulikiwa ipasavyo, lakini kwa tanzania kuwajibishana ni tatizo labda Dr Samia alianzishe hili.
 
BENKI ya Dunia imeimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayopata fedha kutoka kwenye taasisi hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi za Afrika.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania, unaoongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwenye Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Dkt. Ngaruko, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya Dunia katika ukanda huo, alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa sera za uchumi na fedha ambapo licha ya changamoto za UVIKO 19 na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine, tathimini ya Benki hiyo inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika.

“Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano kwa usimamizi mahili wa masuala ya uchumi mpana, si tu kwa nchi za Afrika Mashariki, bali kwa nchi za Afrika, ambapo kiwango cha ukuaji uchumi cha wastani wa asilimia 5.4 ni cha juu, na ninawapongeza sana” alisema Dkt. Ngaruko

Aidha, alipongeza uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia na kuahidi kuwa Benki yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kukuza uchumi na kuwaondolea umasikini wananchi wake kwa kusaidia fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii pamoja na kutoa misaada ya kiufundi.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alimweleza Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika, Dkt. Floribert Ngaruko, kwamba uchumi wa Tanzania unazidi kuimarika na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua muhimu kuhakikisha uchumi unazidi kuimarika na kuleta ahueni kwa wananchi.

Alifafanua kuwa katika kipindi cha robo tatu robo ya mwaka 2022/2023 uchumi umekua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.8 katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliotangulia 2021/2022 na kwamba kutokana na mipango kabambe iliyowekwa na Serikali uchumi utakua zaidi hadi kufikia wastani wa zaidi ya asilimia 6.3 miaka michache ijayo.

“Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi makini wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, tunaahidi kuwa tutasimamia na tutatumia fedha hizo kwa umakini ili kufikia malengo yaliyokusudiwa Alisema Dkt. Nchemba

Mpaka sasa Benki ya Dunia imewekeza zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 7.2, sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 16.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi zaidi ya 29 nchini Tanzania ambapo kati ya miradi hiyo, 24 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 6.41 ni ya kitaifa na mingine 5 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 0.75 ni ya kikanda.

View attachment 2584395
Safi sana Tanzania inazidi kusonga mbele kiuchumi chini ya Rais Samia Suluhu
 
Rais Samia akisimamia uchumi kwa umahiri🐒🐒🐒
 
Safi sana Tanzania inazidi kusonga mbele kiuchumi chini ya Rais Samia Suluhu
Hii siyosafi, wenziyo wanataka maridhiano yaaniCCM wakiri kwamba watu wametrswa sana tunataka tume huru na truth and reconciliation. Aidha, wanaamini kuwa chawa na wapumbafu kazi yao kupigia makofi Rais ana madaraka mengi mno apunguziwe na RPC na Askofu eapigiwe kura na Kabila zao hatitaki Wazenj sisi.
 
BENKI ya Dunia imeimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayopata fedha kutoka kwenye taasisi hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi za Afrika.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania, unaoongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwenye Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Dkt. Ngaruko, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya Dunia katika ukanda huo, alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa sera za uchumi na fedha ambapo licha ya changamoto za UVIKO 19 na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine, tathimini ya Benki hiyo inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika.

“Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano kwa usimamizi mahili wa masuala ya uchumi mpana, si tu kwa nchi za Afrika Mashariki, bali kwa nchi za Afrika, ambapo kiwango cha ukuaji uchumi cha wastani wa asilimia 5.4 ni cha juu, na ninawapongeza sana” alisema Dkt. Ngaruko

Aidha, alipongeza uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia na kuahidi kuwa Benki yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kukuza uchumi na kuwaondolea umasikini wananchi wake kwa kusaidia fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii pamoja na kutoa misaada ya kiufundi.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alimweleza Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika, Dkt. Floribert Ngaruko, kwamba uchumi wa Tanzania unazidi kuimarika na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua muhimu kuhakikisha uchumi unazidi kuimarika na kuleta ahueni kwa wananchi.

Alifafanua kuwa katika kipindi cha robo tatu robo ya mwaka 2022/2023 uchumi umekua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.8 katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliotangulia 2021/2022 na kwamba kutokana na mipango kabambe iliyowekwa na Serikali uchumi utakua zaidi hadi kufikia wastani wa zaidi ya asilimia 6.3 miaka michache ijayo.

“Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi makini wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, tunaahidi kuwa tutasimamia na tutatumia fedha hizo kwa umakini ili kufikia malengo yaliyokusudiwa Alisema Dkt. Nchemba

Mpaka sasa Benki ya Dunia imewekeza zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 7.2, sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 16.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi zaidi ya 29 nchini Tanzania ambapo kati ya miradi hiyo, 24 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 6.41 ni ya kitaifa na mingine 5 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 0.75 ni ya kikanda.

View attachment 2584395
Halafu kuna shoga anasema upotevu wa 30 Trillion ni propoganda? Hao ni world bank tu bado China wametia hela kibao nchini.
 
Back
Top Bottom