BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 2,948
- 6,828
Serikali imewasilisha ombi hilo kupitia Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) unaosimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Dkt. Mwigulu ameiomba WB kuharakisha upatikanaji wa zaidi ya Dola za Marekani Milioni 500 ifikapo Novemba 2023 ili Fedha hizo zisaidie kukabiliana na changamoto ya uhaba wa Dola katika mzunguko wa Fedha hali inayochangia Mfumuko wa Bei na kukwamisha uagizaji wa bidhaa ikiwemo Mafuta.
Aidha, amesema Serikali kupitia Bunge imefanya maboresbo na kupitisha mabadiliko mbalimbali ya Sheria na Kanuni zitakazowezesha kuvutia Uwekezaji wa Mitaji na Teknolojia.
===
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameiambia Benki ya Dunia kwamba Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kuiwezesha sekta binafsi kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwezesha upatikanaji wa fedha za kigeni kupitia uwekezaji wa mitaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Dkt. Nchemba, amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia, ukiongozwa na Mkurugenzi anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bw. Hassan Zaman, katika Ofisi za Hazina Ndogo Jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki hiyo, ikiwemo namna ya kuisadia nchi kukabiliana na athari za upungufu wa dola za Marekani katika mzunguko wa fedha, ili kulinda ukuaji wa uchumi.
Alisema kuwa Serikali kupitia Bunge, limepitisha mabadiliko mbalimbali ya sheria na kanuni zitakazowezesha kuvutia uwekeaji wa mitaji na teknolojia ambapo sheria kadhaa zimefanyiwa marekebisho na sheria nyingine ya masuala ya ununuzi wa umma itajadiliwa bungeni ambapo maboresho ya sheria hiyo yatachochea zaidi uwekezaji.
Aliiomba pia Benki hiyo kuharakisha upatikanaji wa zaidi ya dola za Marekani Milioni 500 ifikapo mwezi Novemba mwaka huu ili fedha hizo zisaidie nchi kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa dola za Marekani katika mzunguko wa fedha nchini hali inayochangia mfumuko wa bei na kukwamisha uagizaji wa bidhaa muhimu kutoka nje ya nchi ikiwemo mafuta.
Aidha, Dkt. Nchemba aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuidhinisha upatikanaji wa fedha kwenye miradi 8 yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2.16 kati ya miradi 26 yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 5 ambayo Serikali imewasilisha kwenye Benki hiyo, na kwamba miradi hiyo itakapokamilika itakuwa na matokeo chanya katika kukuza uchumi na maendeleo ya watu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bw. Hassan Zaman, alipongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Tanzania katika kusimamia na kukuza uchumi wake licha ya uwepo wa changamoto za athari za UVIKO 19 na vita baina ya Urusi na Ukraine na kwamba nchi nyingi za Afrika zinapaswa kujifunza kutoka Tanzania kuhusu usimamizi wa sera za fedha na uchumi.
Alipongeza pia hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini ambapo amesisitiza kuwa hatua hizo zitawavutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza katika sekta muhimu za uzalishaji na hivyo kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Meneja Mkazi wa Benki ya Dunia Bw. Nathan Belete, Meneja Uendeshaji anayesimamia nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe, Bi. Preeti Arora, Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade na maafisa wengine kutoka Tanzania na Benki ya Dunia.