Benki kuu ya Tanzania yapiga marufuku matumizi ya fedha za kigeni kufanya miamala ya ndani

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,992
Reaction score
5,660
Benki kuu ya Tanzania ilisema katika taarifa yake Ijumaa jioni kwamba imepiga marufuku matumizi ya fedha za kigeni kwa miamala na malipo ya ndani.

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesema kwa mujibu wa kanuni zilizotolewa na Serikali mwaka 2025, bei na malipo ya bidhaa na huduma zote nchini lazima yafanywe kwa shilingi za Tanzania.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba, ilisema kanuni hizo pia zinabainisha miamala ambayo inaruhusiwa kufanywa kwa fedha za kigeni.

Ilisema wageni wakiwemo watalii wanatakiwa kubadilisha fedha za kigeni katika benki za biashara au ofisi za kubadilisha fedha nchini Tanzania. Bado wanaweza kulipa kwa kadi za benki au mbinu nyingine za kidijitali.

BOT pia iliwataka wananchi kuripoti ukiukwaji wowote wa kanuni hizi kwa benki kuu kupitia Kitengo cha Ujasusi wa Fedha, polisi au mamlaka nyingine yoyote inayosimamia sheria kwa hatua stahiki
 
Hawana lolote hao,hicho kitengo Cha FIU wanakula mshahara wa Bure tu hapo BOT.
Wachina na wakinga wanauza bidhaa kwa Dola kwa Wageni,Tena kwa bei ya juu kuliko bei iliyotolewa na BOT,Dola watu wanabadilisha tu barabarani tu kama tupo Congo!
Sheria ya maduka ya kubadilisha fedha,inamruhusu mzawa tu kufanya biashara hiyo ila kwa sasa mpaka Wachina wanamiliki bureau de change na utakatishaji wanaofanya unatisha!
Serikali ipo,BOT wapo na FIU wapo,halafu Wanakuja kutoa vistatement humu wakati Kila kitu wanajua!
Wenzetu hawachezi na sekta fedha maana hiyo ndio roho ya Uchumi!
Hatua za haraka zinahitajika kunusuru shilingi yetu,watu wanaichezea sana na hawaipi thamani yake stahiki.
 

Nafikiri BOT wanapaswa kujikita kujua sababu hasa ambazo zinawasukuma watu kutumia fedha za Kigeni kwa miamala ya biashara za Ndani ya nchi badala ya kujikita kwenye kudhibiti Matumizi ya fedha hizo. Ni kwa nini watu hawataki kutumia shilingi ya Tanzania kwa biashara za ndani?

Ukweli halisi ni kwamba, fedha (sarafu) ya Tanzania thamani yake inayumba Sana kupita kiasi mbele ya Dola ya Marekani. Stability ya thamani ya shilingi ipo mashakani Sana, kila siku thamani yake inaporomoka na kwenda chini siku hadi siku Kama vile Fedha ya Zimbabwe.
 
Hizo noti za kitanzania zimechakaa sn huko mtaani.Hasa 10000 na 5000
 
Ni sahihi mkuu lakini unatakiwa kuelewa kwamba shilingi inashuka thamani dhidi ya dola kwa sababu ya uhitaji wa dola kulinganisha na uhitaji wa shilingi.

Hivyo basi, BOT inapopiga marufuku utumiaji wa dola ndani ya nchi, ni kupunguza uhitaji wa dola. Watu hawatataka dola na demand yake itashuka huku uhitaji wa shiling kuongezeka na thamani yake kupanda

Njia ya pili ni kuimarisha uuzaji bidhaa nje ya nchi ili tupate dola zaidi (Kukuza bidhaa za ndani) na kuongeza bidii katika biashara za kutuletea fedha za kigeni kama utalii nk.

Ukiwa na reserve ya kutosha maana yake nchi inaweza kununua bidhaa za muhimu zinazohitaji dola kama mafuta nk bila nchi kuwa na wasiwasi wa upungufu wa dola, hii itafanya dola ionekane kama haina thamani (Supply & Demand)
 


Kushuka kwa Kasi kwa Sarafu ya Fedha katika nchi yoyote ile hasa husababishwa na Hali ya kukosekana kwa Mlingano wa Kibiashara (No Balance of Trade, whereby Import is much higher than Exports).

Aidha, kushuka kwa kasi kwa thamani ya Sarafu au fedha ya Tanzania inaonekana ni kutokana na kuwepo kwa Magendo kwenye Money Supplies katika mzunguko wa fedha.
 
Magufuli alale pema katika Roho zetu Sisi WANYONGE
 
Nafikiri tunazungumza kitu kimoja.

Hivyo utakubaliana na BOT kuwa njia ya kuanza kutatua tatizo hili, ni kupiga marufuku utumiaji wa dola katika miamala ya ndani. Huku tukiendelea kupambana na exports ya bidhaa, huduma n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…