Nitarahisisha hili ili kuendeleza mjadala.
Ninajibu swali - Kwa kweli simjui mmiliki wa Kiwira (kwa hakika).
Je wewe unamjua?
Mkapa,Yona na watu wengine kadhaa wana hisa kwenye mgodi huu.
Ushahidi wa kesi za Kimafia unadhihirisha wazi kwamba mkuu Mkapa ni fisadi.
Kumbuka hii si kesi ya mwizi wa kuku ambayo ni lazima tumshike na mnofu kinywani ili kuthibitisha wizi wake, kwani kumshika na kuku wako kwapani kwake bado haitoshi kumpa mvua, pengine alikuwa akijaribu kumrejesha kuku wako alopotea???.!!!!
Sisi tumemtuhumu Mzee Mkapa kuwa ni Fisadi, je wewe unaweza kuleta utetezi wa maana kwamba Nkapa si Al-Fisad?
Kushindwa kwetu kwa namna yeyote kuleta ushahidi wa wazi juu ya Ufisadi wa mkapa hakumuondelei Mzee huyu Wadhifa na heshima hiyo chafu. Rais wa nchi hawezi kudai kwamba hajui wala hahusiki na wizi wa Billion za kulipa madeni nje ya nchi. Suala la kulipa madeni nje ya nchi lilikuwa namba moja kwa Mkapa, ni vipi hakujua account ya EPA inachotwa kwa Machepeo???
Watu wote kabisa wakiwemo mzee Kingunge na Rostam Azizi mpaka wafagizi ikulu wajue kuna wizi wa Mabillioni lakini ina kuwa habari mpya kwa Rasi wa nchi???
Alikuwa akilipa Madeni ya nje au alikuwa akituongezea??
Ndiyo maana Kesi zote za Wizi wa Kimafia zina Mahakama zake na upelelezi wa aina yake.
Huwezi kuwatuma Polisi wakaao kwenye Mabanda ya mabati, shule hakuna, upeo duni, wauaji hawana hamu na nia ya kazi huku wana vibyongo vya njaa kupeleleza wizi wa Kifisadi!!!
Tumemtuhumu mzee huyu kwa Ufisadi, tupe utetezi wako kuthibitisha kauri yako halali " Mkapa sio Fisadi".