Benjamin William Mkapa nimjuaye... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benjamin William Mkapa nimjuaye...

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Kaniki1974, Jul 2, 2009.

 1. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Rais bora wa TZ next to Mwl. J. Nyerere

  Aliingia madarakani kwa haki bila rushwa wala kununua vyombo vya habari. Alikuwa na hoja na alieleza WAZI nia yake ya kugombea urais.

  Alianza kazi kwa kasi hakungoja wiki mbili au zaidi kupanga baraza la mawaziri.

  Aliunda serikali ndogo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.


  Alikuwa na falsafa binafsi, dira na msomi aliyependa kusoma na kujifunza.

  Akapambana kijemedari kwelikweli na misukosuko ya Reli, MV Bukoba, Elnino na majanga mengine. Akapunguza mfumuko wa bei toka 48% 1994 na kubakia single digit enzi zote za utawala wake.

  Akaboresha utumishi wa umma; kapunguza wafanyakazi hewa na kuboresha maslahi.


  Akapunguza deni la nje na kuipa Tanzania heshima.

  Akajenga miundo mbinu hususan barabara kwa kasi kubwa


  Akavutia wawekezaji wenye tija kama TBL, NBC n.k


  Akajenga EPZ alipanga zijengwe 22 nchi nzima


  Akaimarisha majeshi yetu kwa kuwapatia motisha vitendea kazi na makazi.


  Akajenga Uwanja wa Taifa

  Akajenga Benki kuu Twin towers na kule Zanzibar. Twin Towers kama Bank of Canada, Toronto (kwa wanaojua)


  Alikuwa na hoja zenye mashiko.

  Alikuwa kiongozi kweli jasiri, mwenye kujiamini na hakuogopa mihadhara: iwe ya vyama vya siasa, vyuo vikuu au kimataifa. Alikuwa full of substance.


  Ujasiri wake hata vita ingetokea enzi zake angetuongoza vyema sana kumshinda adui.


  Hakuwa mwongo katika kauli na ahadi zake.

  Alikuwa na maadili na na hekima na aliheshimu mamlaka na taratibu zilizopo.

  Akawapa nguvu na haki zaidi wanawake.

  Alipigania utandawazi kuwanufaisha wengi.

  Alikuwa mchapakazi hakuwa mvivu.

  Alikuwa makini na alipinga na kukwepa sana matumizi yasiyo lazima ya serikali.

  Alisafiri ng’ambo pale tu ilipobidi. Alikaa ofisini na kufanya kazi.

  Alijiheshimu hakuwa Fataki.

  Hakuwa ombaomba, bali alipenda kujenga uwezo, kujitegemea na kuwasaidia ombaomba.

  Akanunua ndege bora ya Rais, mafisadi wakaipinga.

  Akanunua rada ya nguvu, mafisadi wakaipinga.

  Alikuwa na vyeti vya nguvu na alifuzu vyema masomo yake. Alionyesha uwezo. Alikuwa na speech za kisomi.

  Alihakikisha nchi inakaribia kupaa ndio akaikabidhi kwa JK. Tukadhani itapaa.

  Na mengine mengi.

  Huyo ndiye Benjamin William Mkapa, Rais ninayemkubali na kumrank second. Angekuwepo mpaka leo Tanzania ingekuwa emerging economy I am sure.


  Mnaomsema vibaya mshindwe ka kulegea. Hamna shukrani. Ni kiongozi ambaye wanaokumbuka, tunamshukuru sana.
   
 2. S

  Siao Member

  #2
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani kosa ni lako basi...!

  Hujui mwanga kama hujaona giza. kwenye shairi lako hukumalizia vizuri, kuwa ulishawahi kula chakula cha mchana kwake...!

  Pale umaandika njaaaaa tu mshikaji...!

  Unahitaji fimbo kama mtoto wa shule,
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Shairi ungeanza:-

  ALiuza mashirika yote ya Tanzania.

  Akajipa mgodi wa Kiwira.

  Akajipa nyumba za serikali.

  Akawapa Wazungu migodi yetu na ardhi ya bure wachimbe madini.

  Akauza Kilimanjaro Hotel mara tatu na huku sasa twalipa fidia wale wawili wa mwanzo.

  Akawapa Wajanja kiwanja cha ndege cha KIA kwa bei ya dola 1,000/ kwa mwaka.
  aka-EPA hela zetu bale BoT.

  Aka DEEPGREEN hela zetu.

  Aka MEREMETA hela zetu na madini.

  Kama hiyo haitoshi, akaanza kushirikiana na wajanja wachache kuuza silaha ili majirani zetu wachinjane huku akilitumia JWTZ na usalama wa Taifa. Akitumia JWTZ, alinunua RADAR kwa bei ya juu kuliko inavyotakiwa. Akajinunulia na dege bofu bofu.

  Alim-fisadisha Mzindakaya ili a-shut up.

  Na hii yote na yote uliyoandika na yale yote hatukuyaandika, ALILIPWA MSHAHARA WA WALIPA KODI. Makonde siku moja atakiona cha ntema kuni njomba.
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Alikuwa Amiri jeshi mkuu wa majeshi na wapiganaji aliyeongoza kwa ufanisi mkubwa mauwaji ya raia wasiokuwa na hatia Januari 26/27/2001, kule kisiwani Pemba, huku vikosi vyake vya Polisi vikitembeza bakora,vigongo na mabomu ya kutoa machozi katika mitaa ya Darajani na Mtendeni.

  Mauwaji ya Waislamu wa Mwembechai hayatafuta sifa yake nzuri ya ukatili wa utawala wake.

  Manyanyaso kwa wanataaluma na waandishi wa habari waliotumia haki yao ya kidemokarasi ya uhuru wa kutoa maoni hayatasahaulika hasa madhila ya kutaabishwa katika nchi yao wenyewe akina Jenerali Ulimwengu na Mar. Adam Mwaibabile Mwana R.I.P.
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  ni raisi mstaafu wa tanzania ambaye atakufa na laana ya watanzania kama hato omba/kutubu dhambi zake akiwa hai
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kaniki,
  Ungemalizia kwa kibwagizo kuwa huyu ni kuku aliyekula mayai yake mwenyewe.
  Hapo ungeeleweka.
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono kuhusu uwezo alioonesha Benjamin Mkapa katika utawala wake, hasa kurudisha sifa ya Tanzania nje. Alijaribu na kufanikiwa kutupaka mafuta. Alihubiri demokrasia, alihubiri uwazi na uwajibikaji, alihubiri kuchukia rushwa na aliweza kudhibiti mfumuko wa bei.

  Lakini miaka michache ya uongozi wake alionesha udhaifu mkubwa wa uenyekiti wa chama, urais na alituvuruga sana na kutuwekea matatizo ambayo mpaka sasa tunaendelea nayo. Under his watch Tanzania imepata uongozi wa ajabu sana, sasa hivi tunakuwa kama watoto. Kwa hiyo lazima tumuangalie kwa pande zote.

  Kwake kupambana na ufisadi kulilenga zaidi kupambana na rushwa wanayopokea mahakimu, au rushwa ndogondogo lakini ufisadi ni kama aliubariki.
   
 8. Laibon

  Laibon Member

  #8
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaniki,

  Kwanini unapenda kujiunganisha kwenye laana ya Watanzania dhidi ya Mkapa? Hututakuhukumu kwa sasa, inaonekana wewe hauishi TZ kabisa.

  Kama Nyerere alivyosema, ikulu ni mahali patakatifu- Mkapa alipafisadi pale! Angalia mawaziri na maofisa wa serikali yake, wako mahakamani! Hata hizo statistics unazotoa, mfano inflation- aliyekuwa anazitoa si Balali? Zimepikwa tu kuwadanganya wananchi.

  Mkapa has a case to answer, hakuna immunity hapa!
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Inawezekana huyu mtoa aliwahi kula lunch ya huyu jamaa, yaani madudu yote ya che Nkapa hayaoni? Simulazimishi kuyaona ila mzee angalia hata mahali pa kutetea,sikulaumu kama ambavyo simlaumu mbunge wa Kgm mjini alivyomtetea jana bungeni. Mkapa ana mambo mengi ya kujibu.
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Jul 3, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,566
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Good post kaniki.

  Unajua ninachofurahi ni kuwa huyu jamaa anayelaumia yupo, anaishi, anadunda, vongozi waliokuwa wamkamat kaa amekosea wapo nao wanaishi!

  Tutaendelea kulalamika na kulaumu tu hapa, TUNA RAIS YUPOYUPO TU KAMA SANAMU, watu watasubiri kumlaumu akitoka kwenye uongozi.

  JK huwazi ku-mquote kila siku anatoa pumba
  JK hana unaloweza kujivunia kuwa tuna kiongozi

  IQ ya JK is remotely far lower than BMW.

  KWA MIMI MTANZANIA MMOJA, NINAPOONA KUWA WATANZANIA WENZANGU WALIMWEKA JK! then MTU AKANIPA NAFASI YA KU-COMPARE KATI YA HAWA WAWILI, MKAPA KWAMWACHA MBALI SANA JK!

  Kuhusu kuuzwa viwanda kosa lilifanyika na akina Mwinyi kukubali globalisation!

  BWM alikuwa mkweli , mchapakazi na ailsimamia maamuzi yake hii ndio sifa ya kiongozi, hatukuona ujinga wa kujadili mahakama ya kadhi au ya kikristo hakuwa ana muda huo

  Tutatukana na kusema lolote, tukubali kuwa sisi wenyewe watanzania ndio tuna makosa SASA KAMA MTU ALIONA MKAPA ANA MATATIZO NDIO MKAMKWEKA JK KUREKEBISHA?????????????????????LOL!

  Tujadili mzizi wa matatizo, system zetu, sheria zetu lakini kwa yeyote mwenye akili BWM hatasahaulika kwa mazuri aliyotenda TZ. Na kama kuna mabaya mimi siamini mpaka aende jela! ndio nitaamini


  VIZAZI VIJAVYO VIKITUULIZA KUWA ETI MKAPA ALIIBA?? TUTASEMA NDIO?? NA WAKITUUULIZA JE WALE VIONGOZI WALIOKUJA BAADA YAKE WALIFANYA NINI walimshtaki?? kimya!!!!! bado mnalaumu wezi

  Mtanzania bila aibu anasema eti aombe msamaha! haya mawazo ya kifisadi pia! eti MKAPA KAMA KWELI ALIIBA AKIOMBA MSAMAHA BASI IS OK! bado tunasema tatizo ni viongozi hapa?? watz siku zote wajuaji tunamuhitaji MKAPA MWINGINE!

  Unaweza ukampa MAXIMO cheo cha urais na akafanya vizuri zaidi kuliko JK!

  Tatizo sisi, mwakani JK anaweza akasema hagombei tunaweza kumpa urais Sofia Simba! sisi!
   
 11. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ben Mkapa,

  Alimkabidi mkewe mama Mkapa aka first lady funguo za ikulu yetu akawaenzi akina Maro, akutuibia kwa kutumia mifuko ya kiserilikali, akawapa nduguze tender za kiwizi, akajenga majumba ya kifahari kwa kodi zetu.

  Mkapa aliwawezesha watanzania kuanzisha madeni hewa ulaya na kujifanya wanalipa madeni kwa kodi zetu.

  Mkapa aliuza mali asili zetu zote.

  Makapa hakuridhika akavunja katiba akafungua kampuni yake binafsi Kiwira akiwa ikulu akishindana na wavuja jasho.
   
 12. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  mnaniliza jamani naihurumia nchi yangu......
   
 13. Radical

  Radical JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 374
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wan JF makubwa/mazuri aliyoyafanya ni wajibu wake na kiongozi yeyote, so mazuri yake haya-justify ubaya alio ufanya baadae. He should be held accountable for his misconduct.
   
 14. S

  Stephano Member

  #14
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. hata wewe unaeona mapungufu una pande mbili ya maisha yako. una mazuri na mabaya. kabla hujasemea boriti katika jicho la mwenzio toa kibanzi kilichoko katika jicho lako.

  aiseeee jamaa wameandika kwa mahasira. inaelekea jamaa wanaishi maisha ya shida sana maana kuwa na maisha ya kuangalia vitu vibaya tu lazima uwe na negative perceptional mind.

  mtunzi angemalizi kwa kusema hakuna aliye kamili alipopotosha tuparekebishe na tujifunze kutokana na makosa ya mwenzetu tusiyarudie.
   
 15. a

  adobe JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Jamani tuache yote ila mkapa huwezi kumlinganisha na JK.Alifanya mambo yaliyoonekena.Ingawa ana mapungufu yake ila hayazidi mazuri alofanya.Hata ndani ya familia baba hawezi kufanya yote mazuri.Mkapa ndo mwanga tulionao sasa wa TZ
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  mimi nasema hv

  mkapa ni mwanaume mtake msitake.
  huwez kumlinganisha na huyu kikwete.

  hv jk angechukua baada ya mwinyi ingekuwaje? huyu jk amekuta nchi pazuri lakini anaharibu tu.
  mkapa safi sana na hata ninyi mnaopinga hapa kipiondi kile mliona heri tubadili katiba ili BWM aendelee. hata mambo ya msingi mnatia question mark!!!?
   
 17. A

  August JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Mkapa ajuta

  • Ahuzunishwa wageni kuhodhi uchumi

  na Mwandishi Wetu

  RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, amesema anajutia kitendo chake cha kuliingiza taifa katika ubinafsishaji wa rasilimali bila ya kujiandaa kikamilifu na mabadiliko hayo.

  Mkapa alitoa majuto hayo katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) uliofanyika Zanzibar wiki iliyopita katika Hoteli ya Zamani Kempinski na kuhudhuriwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki.

  Mbali ya Mbeki, viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale - Mwiru.

  Mmoja ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo ambaye alizungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa sharti la kutokutajwa jina lake, alisema Mkapa alikiri kuwa sera ya ubinafsishaji haijamsaidia kwa kiwango kilichotarajiwa Mtanzania na badala yake wamegeuka wageni katika rasilimali zao.

  Chanzo hicho kilidokeza kuwa Mkapa alibainisha kuwa kukubali kwake sera hiyo kulikuwa na lengo zuri la kuwafanya Watanzania waondokane na lindi la umaskini kupitia uwekezaji utakaofanywa katika rasilimali zao.

  “Alituambia sera ya ubinafsishaji inamuumiza mno, kwani alipoikubali hakutarajia kama ingeweza kuwafanya wageni wawe na sauti katika rasilimali za taifa kuliko wazawa kama ilivyo sasa,” kilisema chanzo hicho.

  Chanzo hicho kilibainisha kuwa Mkapa alifikia hatua ya kudai kuwa kama angepata nafasi ya kuwa kiongozi tena wa taifa hili angerekebisha sera ya ubinafsishaji haraka ili walau Watanzania waanze kufaidi rasilimali za nchi yao, badala ya kuwa mashuhuda wa wageni wanaoendelea kuneemeka na rasilimali za nchi.

  Alisema tatizo kubwa lililopo katika nchi za Afrika ni kutumia baadhi ya mambo wanayotakiwa kuyafanya na wafadhili au mifuko ya fedha, bila kuyafanyia tathmini ya kina ili kujua kama hayataleta madhara katika siku za usoni.

  “Mkapa alionyesha kujutia uamuzi alioufanya kwenye uwekezaji na aliweka wazi kuwa kama angeruhusiwa kurudi katika nafasi hiyo, basi jambo la kwanza kulirekebisha ni ubinafsishaji,” kilisema chanzo hicho.

  Mkapa katika utawala wake alibinafsisha mashirika mengi ya umma, ikiwemo Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa bei ya chini, kitendo ambacho kilizua malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, pia alibinafsisha Shirika la Ndege Tanzania (ATC) na mengine mengi, kiasi cha kuzua malalamiko mbalimbali ndani na nje ya nchi.

  Aidha, katika utawala wake pia alilalamikiwa kwa kuwapendelea wawekezaji wa kigeni kuliko wazalendo, hasa katika sekta ya madini na kuingia mikataba mibovu ambayo hadi sasa imekuwa mzigo mkubwa kwa taifa, sambamba na wawekezaji hao kupata misamaha ya kodi kwa kigezo cha kuwavutia.

  Kuingia mikataba mibovu huku ndiko kulikomfanya Rais Jakaya Kikwete kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini na kutoa ushauri wa namna bora ya kushughulikia sekta hiyo.

  Majuto hayo ya Mkapa yanakuja huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya wabunge na wananchi wakitaka afutiwe kinga yake ili aweze kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yake akiwa ikulu.

  Katika utawala wake, Mkapa anadaiwa kutumia madaraka yake kuanzisha miradi mbalimbali inayomhusu, ama kwa kupitia familia yake au ndugu zake, ukiwemo ule wa makaa ya mawe wa Kiwira, ambao hivi karibuni wamiliki wake wametajwa hadharani kwa mara ya kwanza. Chagizo la kutaka kutolewa kinga limezidi kupata kasi baada ya waliokuwa mawaziri wake, Basil Mramba (Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini) na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja, kufikishwa mahakamani kwa kosa la kulisababishia taifa hasara ya sh bilioni 11 kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya M/S Stewart. Kinga ya Mkapa inaweza kuondolewa kama Bunge litapiga kura ya kutaka kutengua kinga hiyo, lakini ni lazima hoja hiyo iungwe mkono na theluthi mbili ya wabunge wote.
   
 18. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nakuunga mkono mkuu.

  Rais anao wajibu wa kufanya mazuri kwa nchi yake ambayo kwayo tunamlipa mshahara mzuri na kumtayarishia mafao mazuri anapostaafu ambayo anaendelea nayo hadi kufa. Kwa mfano anapata 80% ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, ana ulinzi, ana magari ya serikali na watumishi wanaolipwa na serikali, anaweza kutibiwa nje ya nchi, anaruhusiwa kufanya ziara zake binafsi za kimatembezi nje ya nchi mara 4 kwa mwaka kwa gharama ya kodi ya wananchi nk.

  Kwa hayo mazuri tulimlipa, je kwa mabaya aliyofanya - asilipwe kwayo?

  Kanuni yetu ni carot and stick. Ukifanya vizuri -carot, ukifanya vibaya - stick, period!
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  And be praised for his conduct as well
   
 20. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Amen!
   
Loading...