-Wanabidii Salaam. Ama baada ya Salaama napenda niendeleze mjadala wa sasa unaohusiana na
"Sangoma Masalia" au PM7 unaoongozwa na ndugu yangu au kaka yangu Zitto Kabwe. Ndugu wanajukwaa mimi ni mmoja wa watu waliokuwa wakitoa mchango mkubwa kwa hili kundi. Jinsi Zitto anavyosema kwamba damu yake iko ndani ya CHADEMA, mimi pia nakiri kwamba damu yangu iko ndani ya CHADEMA. Nimekuwa mfuasi wa Zitto kwa takribani miaka miwili. Nilikutana na zitto kwenye moja ya vikao vya chama, na kwa vile nililalamika kutokukutendewa haki, alinifariji sana na kunifanya niwe karibu naye. Kila mara tulipokutana hata pale makao makuu, zitto alinipa hela nyingi tu akiniambia kwamba nitumia kama nauli. Kiwango cha chini ambayo Zitto amewahi kunipa ni Tsh 50,000
-Siku moja nikiwa pale mlimani city, Mh. Zitto aliniita nikutane naye Ubungo Plaza hotel . nilichukua bajaj na kukimbia pale ambako nilimkuta akiwa Juliana pamoja January Makamba na kunipa kazi maalum ndani ya Jamiiforums. Ndugu zangu, nakiri kwamba, Mengi anayoyasema Bwana saanane ni ya kweli. Kundi la PM7 lipo. Wakina Juliana nao ni wafuasi wa hilo kundi la PM7. Uhusiano wa Juliana na Zitto ni zaidi ya mnavoambiwa. Zitto na Juliana ni wapenzi. Hii nathibitisha kwa maana kwamba, nimekutana nao kwenye hoteli moja eneo la Sinza ambako nilikuwa nikikutana na Mh. Zitto kwa kazi maalum ya kufanikisha ndoto zake za Urais.
-Sijaja hapa kumchafua au kushabikia wakina saanane, nakuja hapa kuwawekea umma wazi tabia halisi ya huyu mtu ambaye wamemwamini. Juzi jioni, baada ya tuhuma dhidi yake kutolewa, kama kawaida alinitumia ujumbe mfupi kwamba niingie JF nianze kutoa mashambulizi, lakini bahati mbaya nilikuwa mkoani na sikuwa na mtandao au airtime. Kwa hiyo sikuweza kuingia kwenye simu kufanikisha hiyo shughuli. Baada ya dakika thelathini kabla sijamjibu akatuma ujumbe mwingine tena akinitishia. Mimi sikuelewa kinachoendelea nikampuuzia hadi kesho yake asubuhi
-Nikidhania yote yameisha, Zitto alinitumia ujumbe mzito akiniambia kwamba nanukuu "Wewe unajifanya kujua ilhali unaishi kwa fadhili zangu. Hujui mimi ni nani" huu ujumbe ulinikera na kunilazimu kumjibu kwa hasira. Kwamba asinibabaishe. Simwogopi mimi namwogopa mungu. Hapa akajinijibu kwamba ananipa masaa 72 kufanya shughuli yake ambayo ni kuingia kwenye mitandao kujibu mashambulizi. Wakuu nakiri kwamba mimi sitishwi na nguvu ya Giza.
-Zitto aliniomba niende naye safari fupi November 2011. Safari hii ilikuwa ni ya kwenda Tanga, Saa tisa mchana, mimi Zitto pamoja na January Makamba, tukiwa na gari aina ya Nissan Patrol Silver, hii safari aliyetuongoza alikuwa ni January. tulienda kwa mganga wa kienyeji ambaye ilibidi tuandamane hadi kwenye andaki Fulani na kunilazimisha kula kiapo cha utiifu kwake Zitto.
-Leo ameniambia kwamba nisipo fanya shuguli yake ntakiona. Na shuguli yenywe ni ya kuwachafua viongozi wa CHADEMA. Muda mwingine nawachafua viongozi wa CCM kutumia ID kadhaa humu JF. Sasa naiwekea umma wa kitanzania kwamba nikifa, kifo changu kimetokana na Zitto kabwe. Nimeshindwa kulala muda wa siku tatu na kama watabisha, basi nami nitaziweka wazi hizo ID ambazo tumekuwa tukizitumia Ni nyingi sana ili watanzania waamue ukweli uko wapi...
chicco,
nice 2,
chepe kubwa,
Taswira,
Pilitoni,
chicco, Freshthinking, Honey K,
Tuntemeke etc. yote ni ID mpya inayotumia password yetu ile ile. Ilhali Nice 2 akitumia Zitto mwenyewe. Kana hizi ID's kama huzijui. Passowrd ndo zilezile