Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Diplomacy way needed, to settle the difference for all who concerned on this rampant.
You all must be reasonable to stand for CHADEMA. What's standing over there between
you, in this type of politicized, the demonstration there is a storytelling talent. Means
a conflict of interest, don't be Undisciplined and disorderly youths. all of you have to
respect and follow the CHADEMA Party rules, and presents you are complain to the party
crisis committee.
 
tatizo lengine ndio hilo..kwanini hatuwei kuzuia hisia zetu?..unaposema taswira a.k.a zitto na wewe tukuite a.k.a nani?. unataka kutuaminisha kuwa zitto yeye hana wanaompinga?, ama unataka kutuaminisha kuwa zitto yeye hatakiwi kuwa na watetezi?,,mpaka sasa ndani ya chadema, wapinzani wa zitto ni wawili, mbowe na slaa, ina maana nawewe akwite mbowe ama slaa?..au wewe ndo saa nane?...
tujifunze kuwa objective jamani, jusijidhalilishe na michango yetu.....MOVIE INAENDELEA

nawaaminia mods wa jf,hii name calling itafanyiwa kazi
 
zitto umemshinda nani mission zako zote zimebuburuka hata kabla ya kufanikiwa mukichwa humo hakuna plan unamihemuko mumekuja usiku wa manane munaposti na kujijibu halafu unasema unauwezo upi kaka pole ndio mshahara wa msaliti timu nzima muko hapa id yenu leo mumeitupa tuanfurahi kwamba munathibitisha wote na wewe mwenyewe kwamba uring leader huu uwezi umeshindwa kwa chadema ulishindwa kwa nccr
hoja ya msingi tuizingatie.......saa nane ametumika vibaya sana
 
Hayo maswali yote unayouliza muulize ben yeye ndio inteligensia anaweza kujua mwisho wa mimi kuwasiliana na zitto ni saangapi pamoja na maswali mengine uliyouliza.
Kipi kigumu katika maswali hapo juu? Jibu maswali na sio kukimbia, ukikimbia unathibitisha tu umetumwa...
 
hahahah nimecheka sana maana wale wanaoamini ushirikina wanakumbia ukimuona paka anadu basi wewe au ndu yako atakufa. lakini sisi tulioenda shule shule Rational-Emotive Therapy's A-B-C Theory of Emotional Disturbance inatumbia hizo ni ndoto tu za mchana. ubarikiwe mkuu. Ila muulizeni zito kwanini hataki kuoa mpaka leo...

Unatumia theory hiyo hahahhah!!!!tumia Cognative theory utenganishe kati ya generalization na specifiation
Swala la kuoa zitto alishakujibu kule kwenye interview,Labda niulize mm yule mwali pale home anatoka lini?
 
Mchezo anaoufanya ben saanane na mamuya naujua sana,ndio maana nipo kolikoli kuwaumbua hapa.Nasubiria jambo moja litamkwe na mm nipigilie king ya mwisho.
Namsapoti zitto hadi tone langu la mwisho kwasababu wamekuwa wakimsakama kuanzia gazeti la mwanahalisi ambalo linamilikiwa na mtu wa chadema na aliyeandika makala zote ni kiongozi wa juu wa chadema,lakini hawakumshinda zitto.
Wamekuwa na tabia ya kumtenga na kumsakama ili hali wao wana akadi za ccm nyuma.

hapo kwenye red panadhihirisha kuwa una akili za kitumwa.
ni kwa nini wewe usitangaze hilo jambo mpaka usaidiwe kutangaziwa??
Mkuu unawatia aibu hao waliokutuma na pia una-shake credibilty ya upeo wako hapa JF.
Jitahidi uwe na fikra huru.

CC. to Juliana Shonza Zitto Ben Saanane Mchange
 
Mchange, kwanza uandishi wako umekosa mtirriko mzuri wa mawazo hata kama kuna ukweli wowote kati ya unayoyazungumza itakuwa ngumu sana ujumbe wako kueleweka. Pili, naona unataka kujisafisha lakini hausafishiki. Ona hapa ulichoandika:

"2. Ni BEN SAA NANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ‘’patriotic movement seven’’ na akakifupisha PM7.
3. Ni BEN SAA NANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE "


Unajua nini Mchange, watu wote wenye akili hawawezi kukuamini kwa haya unayoyaandika. You are being too pretentious, unatungatunga tu vijistori vya kubumba na watu wengi waliojiunga humu JF ni watu wazima wenye akili zao, wanaweza kupembua pumba na mchele. Zako hizi ni pumba.

anataka kujifanya eti na yeye ni Jason Bourne....eti Cobra, Mdude.
Yaaniunatungwa jina wewe unaangaliatu.
Haya Mdude huyo naye anatiririka, japo njia anayotiririkia ina mbigili kibao.
 
Last edited by a moderator:
Hapa mimi nasubiri ushahidi kuwa je zitto hamjui ben?
Na kama kuna mwenye kunipa ushahidi kuwa zitto na ben wameshakutana uso kwa uso natoa hitimisho.
 
Kipi kigumu katika maswali hapo juu? Jibu maswali na sio kukimbia, ukikimbia unathibitisha tu umetumwa...

subiria utetezi wake kesho nadhani kama atathamini Jf.Huko ndiko utamtandika maswali.Zaidi ya hapo ww unaonekana umerukia wazo la 4 la 1 2 3 umemwahia nani??
 
Natafuta ile thread/post inayomuhusu Ben saanane na Usaliti kwa watanzani wenzake kule India .Huyu mtu ni hatari
 
Kunasehemu umekuta anahusika? yeye hanahaki ya kufahamiana na vijana kama wewe?au ww ukifahamiana na zitto utakuwa mtu wa zitto? Wamejishushia heshima sana..mwampamba,Julina shonza na kitila mkumbo to follow.Nadhani utakaa na kujua kwanini zitto anasakamwa sana chadema.

Sijui hata unachotaka kusema ni nini hapa.
 
Habari, nimeona mchango wangu huu niuanzishie uzi ili tujadiliane kwa mapana..

Mpaka tuufikie tunaouita ukombozi wa pili, basi tuna kazi na safari ndefu sana!

Kama vijana tunaweza tukainuka na kuanza kuporomosha mashtaka na kutaja majina ya watu bila hata facts, basi kazi ipo ndugu zangu.

Ufahamu wangu ni kuwa ili tufanikiwe kuwaondoa CCM madarakani lazima tufanye kazi hiyo kama timu moja, mawazo yangu ni kuwa hatutaweza kufikia hatua yoyote ikiwa tutakuwa na vijana wa namna hii.

Vijana wa aina ya Ben Saanane wanaoweza kukaa, kutengeneza mgogoro, kubuni njia za kuuendesha mgogoro, kutafuta suluhu na hatimaye kwenda kuuza huo mgogoro kwa viongozi wengine huku akiamini kuwa anakinusuru chama hakika anakosea sana.

Vijana wa aina ya Saanane ambao kazi yao nikutumia muda na akili zao nyingi kuwarubuni na kuwagombanisha vijana wa chama na viongozi wa chama ni hatari pengine kuliko ukoma.

Kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akinitaja kwenye mijadala yake yote. Bila hata kuangalia namna ninavyohusika, na kwa kuwa na leo hii ameamua kunitaja na kunihusisha moja kwa moja, na kwa kuwa viongozi, vijana na wanachama wengi wa chadema wamekuwa wakinihusisha mimi kuwa karibu sana na zitto kabwe. leo nitasema kitu kwenye hili.

1. Naomba niweke wazi hapa leo, kuwa sikuwahi kumfahamu mtu anayeitwa Ben Saa nane kabla mwezi wa nne 2011.
sijawahi kumsikia jina wala kumuona sura yake.(hawezi kubisha kwenye hili)

2. Ben ndiye alikuwa wa kwanza kunipigia simu, kati kati ya kipindi cha kampeni za uchaguzi wa BAVICHA - 2011 mimi nikiwa nagombea uenyekiti na yeye akiwa ni mgombea wa kimkakati(alitumwa na baadhi ya viongozi kuja kuuvuruga uchaguzi-uthibitisho upo) ambapo aliponipigia simu na kunieleza kuwa tuna haja ya kukaa kama wagombea na kuangalia namna tunaweza shiriki salama kwenye huo uchaguzi kwa madai kuwa amepata tetesi makao makuu wanamgombea wao na wanajiandaa kukata majina ya watu, jina lake na langu yakikiwemo. Nilimsikiliza na kumpuuza.

3. Baada ya hapo sijawahi kuwasiliana nae tena ben saa nane, mpaka usiku wa siku jina langu limekatwa na kamati kuu ya chama, tena aliwasiliana na mimi kupitia grayson nyakarungu, aliyekuwa swahiba wake…cha kusikitisha ni kuwa mwana mkakati ben aliwashauri mwampamba, nyakarungu na kisandu kuungana, akanishirikisha na mimi. Huku nikijua dhamira yake kuwa ni unafiki. Nikamsikiliza kwa kuwa sikuwa tena na cha kupoteza (nimeshaenguliwa tayari).

Masikini ya mungu BEN akawahadaa vijana wa watu (Mwampamba na Nyakarungu) wakaenguliwa huku yeye akiwa ni wa kwanza kukiri kuwa wameamua kuongeza nguvu.

4. Unafiki wa Saanane uliendelea siku ya tatu baada ya kuisha kwa uchaguzi wa BAVICHA maana baada ya kukatwa jina langu, wanafiki wengi walifikiri ningetoa tamko la kukipinga chama ama kuhama chama, sikufanya hivyo, kwangu mimi uchaguzi ule haukuwa ligi, ilikuwa ni mechi tu ya kirafiki. Hapo mwenyekiti wa chadema wilaya ya Kibaha akaomba kukutana namimi, nikakubali, nikakutana nae ubungo plaza, tukiwa hapo tulikuwa na mwampamba na nyakarungu, aliposimuliwa saa nane kuwa tunaenda kukutana ubungo Plaza, akaandika humu jamii forums kwa kutumia ID fake yake kuwa tumekutana na mimi nina mpango wa kuhama chama.

Nlimwambia Mwampamba kuwa saa nane ana kazi maalum, mwampamba hakunielewa, akanipinga sana sana sana, naamini leo atanielewa vizuri sasa.

5. Kwa kipindi chote hicho saa nane alikuwa anaitisha vikao vya kila aina, saa nane anatukana na kutoa kejeli za kila aina kwa viongozi wa kuu hasa katibu mkuu na mwenyekiti (lengo ni kutaka kluthibitisha kuwa kuna vijana wanawapinga viongozi hawa). Ninataja maeneo machache ambayo saa nane alipenda kuitishia vikao vyake, KWA JOHN FEDHA-KINONDONI, BLUE PEARL HOTEL-UBUNGO PLAZA na LUCH TIME HOTEL-UBUNGO EXTERNAL….naomba nikiri hadharani hapa, si mimi, mwampamba wala Juliana anayemsema aliyewahi kwenda kukutana na saa nane akajinunulia kinywaji wala chakula…kwa saa nane huwa tukifika tunakula, tunakunywa mpaka tunapochoka saa nane yeye hulipia-tukambatiza jina tukamwita manji. (lakini siku zote nimekuwa nikiwaambia wenzangu kuwa kaeni chonjo na huyu jamaa ana kazi maalum---leo wamejionea)

6. kati kati mwaka jana 2011 mwenyekiti wetu wa taifa freeman mbowe alikamatwa kwa kilichodaiwa kutokutii amri ya mahakama hapa napo saa nane akafanya vitu vyake, kama kawaida yake, akawakusanya vijana wake wote ambao yupo nao kwa kazi maalum akaanza kuwajaza ujinga…naomba nikiri tena hapa kuwa usipokuwa makini ni rahisi sana kuingia kwenye kumi na nane za huyu jamaa. Ni lalzima uwe makini kama mchange kumshinda na ndio maana ananichukia sana sana.

Mimi nimefundishwa kuwafahamu wanafiki. Hasa ninapokuwa naongea nao uso kwa macho saa nane kwangu alikuwa mnafiki kwa hiyo sikumpa nafasi hata chembe.

7. katika kipindi chote hiko sijawahi kumsikia mwana mkakati saa nane akiwasema vizuri viongozi wa chadema. Mtu pekee aliyekuwa anamsifia alikuwa ni zitto.

SAA NANE NA ZITTO
Nimeshtushwa sana na maandishi aliyoyaandika Saanane leo, hii inatokana na ama kuchanganyikiwa au kujihami kutokana na kushushuliwa na kuonekana mwongo. Naomba nieleze vizuri hapa.

1. Ben Saanane ndiye alikuwa muitishaji mkuu wa vikao vya hotelini(makutano) akiwa na saa yake ya kurekodi aliyonunuliwa na kiongozi mmoja wa chama kwa kinachoitwa kazi ya ushushu. Yeye ndiy aliyekuwa mwenyekiti wa vikao na mwandishi wa kila kinachosemwa.

2. Ni BEN SAANANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ‘’patriotic movement seven’’ na akakifupisha PM7. Akashawishi kikundi hicho kizunguke nchi nzima kuhamasisha viongozi wa huko kufanya mageuzi ndani ya chama. Saa nane unafiki utakupeleka pabaya.

3. Ni BEN SAANANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE (kwa kuwa nilikuwa naijua dhamira yake niliendelea kumkeli)

4. Ni BEN SAANANE ndiye aliyeshauri namna ya kuhakikisha kikundi hicho kinapata pesa, wakati mimi nilimpinga ku anzia kuanzisha hiko kikundi mpaka namna ya kukusanya kwake pesa..wakati yeye alikuwa anasisitiza kwenye njia ya kukusanya michango, tena tuwachangishe viongozi wa chama na watu wengine maarufu.

5. Akiwa mkweli atakumbuka na kukiri kuwa nilimwambia kuanzisha kikundi hicho ni sawa na kuanzisha chama ndani ya chama, aliumizwa na misimamo yangu sana.

6. Ni BEN SAANANE ndiy aliyekuwa anasisitiza tuombe kukutana na zitto kabwe ili tumuombe ufadhili wa kufadhili kikundi chetu kilichoasisiwa na SAANANE na akanipa jukumu la kuhakikisha ninamwambia na kumshawishi zitto tukutane nae tufanye nae kikao, sababu yake kubwa ni kwamba Zitto ni rafiki yangu sana na itakuwa rahisi kumpata. Hapa tulirumbana sana, mimi nilielewa dhamira yake na nikiri leo hadharani kuwa nilimshauri zitto asikubali kukutana na kikundi hiki, na niukamwambia kabisa kuwa lengo la kikundi hiki ni kuthibitisha makundi ndani ya chama.-leo yametimia.

7. Ni SAANANE aliyewaapia kujito a kwenye kikundi alichokianzisha mwenyewe kwa sababu ya kutokumpata zitto kwenye kikao, siku ambayo saa nane alipendekeza zitto tukutane naye zitto alikwenda marekani kuzindua tawi la chadema, ni saa nane ndiye aliyenilaumu sana kuwa kwa nini sikumuarifu kuwa zitto hatokuwepo, nilimjibu sio wajibu wangu kuwaambia watu kuwa zitto yupo ama hayupo.

8. Ni Saanane huyu huyu mnafiki tuliyerumbana naye hasa mimi nay eye juu ya namna ya kumshirikisha zitto kwenye michango ya kikundi chake cha PM7. Naomba ninukuu mabishano yetu..mimi ‘’ kama swala ni kukusanya pesa, kwanini tumfuate Zitto kwanza na sio mtu mwengine yeyote’’?...saa nane..’’kwa sababu zitto ni kijana na ana mitazamo chanya kwa vijana wenzie na pia tunafanana nayo mitazamo hiyo sio kamakina mnyika wao status quo’’…mimi..’’kama Zitto tumemwomba tuonane naye na amesafiri bila kutujibu hauoni kuwa anatuudharau, kwanini tujipeleke kwa zitto tunayemnung’unikia kila leo?’’..saa nane.. ’’ hapana ni lazima atusaidie, zitto kwa vyovyote lazima agombee uenyekiti, na hatuwezi fanya hii kazi tukamfungulia milango bila nay eye kutoka jasho lake, ni lazima atupe pesa’’….mimi sasa kwanini tunakataa wenzetu kutumiwa halafu na sisi tunajitumikisha wenyewe kwa zitto?’’…saa nane..’’Mchange, hakuna jinsi tunaweza acha mshirikisha zitto, mwisho wa siku zitto atakuwa beneficiary kwenye huu mpango’’… …………………ukifuatilia kwa makini mazungumzo yetu ambayo kwa bahati nzuri nimeyarekodi kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho utaweza kumuelewa SAANANE kuwa alikuwa na kazi maalum.

Niseme hapa kuwa wote kwa pamoja, saa nane na zitto kila mmoja ameniambia kwa mdomo wake kuwa hawajawahi kuonana uso kwa macho, zitto yeye anasema kuwa anaweza akakutana leo na saa nane barabarani na akapishana nae bila kumfahamu.

Wote kwa pamoja wameniambia kuwa mawasiliano yao huwa ni kwa simu hasa SMS na mara chache kwa emails.

Na moja kati ya malalamiko aliyokuwa ananipa saa nane nimpe zitto ni kuwa..
1.kwa nini hapokei simu za wapiganaji wake akiwemo yeye?...
2..kwanini anakuwa na mpiganaji kama saa nane na hataki kuonna nae….
3…kwanini hataki kukifadhili kikundi cha PM7.?

Kwa mtiririko wa matukio ulivyo, na kwa jinsi SAA NANE alivyoandika mashtaka yake dhidi ya zitto huku akizani anamchafua, hakika amejidharirisha sana.

Mtu mmoja mpinzani mkubwa sana wa zitto amenitumia sms kwenye facebook, ananiambia JF vipi maana COMPUTER YANGU HAIFUNGUI..huyu nae ni mjinga sababu anashabikia ujinga.

Kumshambulia zitto kwa mashtaka ya uwongo namna hii kuna mfanya zitto awe na nafasi ya kuonekana anasingiziwa mamba mengi sana hasa ndani ya chama.

Kwa mimi ninayemfahamu Saanane nje na ndani, na ninayefahamiana na kufanya kazi na Zitto, kwa mashtaka haya ya uwongo, basi hakika nitazidi kumuamini Zitto.

Nitazidi kuamini kuwa Zitto amesingiziwa mambo mengi sana ndani na nje ya chama, ninazidi kumuamini na kumtia moyo kwamba hizi ni hatua za mwisho za watu wanaokupinga, wakishindwa kukupinga kwa facts, watakupinga kwa uwongo…saa nane amekubali kutumika vibaya kwa kisingizio cha kuwa anakilinda chama na viongozi wake.

Napata mashaka kama anakielewa anachokisema, huwezi kumtenganisha zitto na uongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama, hivyo sio rahisi kumchafua zitto ukaacha kukichafua chama.

Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.

Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu ..

Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane.

Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.

Mchafue Zitto kama unahisi una sababu ya kufanya hivyo kwa mambo ambayo una ushahidi nayo.

SAANANE acha tabia ya KUBUNI MGOGORO, KUUANZISHA, KUUENDELEZA, NA KISHA KUUTUMIA KAMA CHANZO CHAKO CHA KUPATA PESA.

SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq tharasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..

Nimeiweka kwa ushahidi manake utashangaa baada ya maeleko ya Zitto Mchange anaweza kubadili
 
Hahahahaa, jamani mie mbavu zangu. Jamaa amekaa tu anakodoa macho watu wanamtungia hadi jina.
anataka kujifanya eti na yeye ni Jason Bourne....eti Cobra, Mdude.
Yaaniunatungwa jina wewe unaangaliatu.
Haya Mdude huyo naye anatiririka, japo njia anayotiririkia ina mbigili kibao.
 
pumba anazo yule ambaye anakimbia kivuli chake,anayetaka kuuaminisha umma kwamba hatumiwi wakati huo huo maelezo yake yanajifunga,soma vizuri maelezo ya mchange utaelewa maana kamaliza kila kitu.bado sijafunguka nitakapo amua kufunguka nitafunguka kivingine,ila kwa leo dozi ya mchange inatosha
Zitto ulitokana wapi na hizi takataka,fb kumekua moto wamekuja jf

Taswira na malindi mnajaza post ili uzi uwe mrefu kama wa Ben Saanane,hautamvutia yeyote

Juliana,ben,habib,gray huu usaliti wenu kama mlishirikiana na yule mzee aliyetabiria kufa kwa chadema na tiss,kwa huu uropokaji wenu watawaondoa

wasaliti,washirikina wakubwa.pumbav nyie na vizazi viunoni mwenu
 
Last edited by a moderator:
Unatumia theory hiyo hahahhah!!!!tumia Cognative theory utenganishe kati ya generalization na specifiation
Swala la kuoa zitto alishakujibu kule kwenye interview,Labda niulize mm yule mwali pale home anatoka lini?

ndiyom maana mnafeli mitihani hivihivi unaambiwa without using mathetical tables solve the following wewe unaamua kuachana na kiti unakaa chini. jibu swali kwanini zito hataki kuoa? kwani mwali kuwa ndani ndiyo kuoa wewe vipi? naona leo mnasaidiana , kyama chenu kimefika.uneniambia alikuwa hajapata mwenza ningekuona una busara lakini kwa hili bure kabia.
 
2. Ni BEN SAANANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ‘’patriotic movement seven’’ na akakifupisha PM7. Akashawishi kikundi hicho kizunguke nchi nzima kuhamasisha viongozi wa huko kufanya mageuzi ndani ya chama. Saa nane unafiki utakupeleka pabaya.

ni sawa kabisa Ben Saanane aliwashawishi na kuunda hicho kikundi(kama ni kweli).
Je hao wanakikundi hawakua na akili timamu mpaka kupangwa na kuunda kikundi na kutungiwa majina na kukaa kimya kwa mda wote huo mpaka yeye mwenyewe Ben Saanane kuanzisha mjadala wa kuwaanika wanakikundi hao hadi na wao ndo waje kujibu hoja kwa kumsema na kumsuta muasisi wa kikundi hicho??
je Ben Saanane asingevunja jungu hili hizi harakati za kundi hili zingeendelea mpaka lini kuharibu misingi ya cha hichi(kama ni kweli liku adhamira kuu)
CC. to Juliana Shonza Ben Saanane Zitto Exaud Mamuya Mchange
 
Last edited by a moderator:
Saa tisa, tehe tehe hata jina linaonesha na kusadifu mtu alivyo hilo ni jina alopewa tiss, kuitiss chadema. Ben saa 8???? hakuna jina la hivyo.
 
Saa tisa, tehe tehe hata jina linaonesha na kusadifu mtu alivyo hilo ni jina alopewa tiss, kuitiss chadema. Ben saa 8???? hakuna jina la hivyo.

Ukiandika TISS gogle jina la Ben saanane la kwanza kutokea
 
Back
Top Bottom