Prof Hirji, kama unafuatilia huu mnakasha somo hapa chini kiduchu.
Jan P van Bergen katika kitabu chake,-Development and Religion in Tanzania,-(1981) ametoboa siri kuhusu uadui aliokuwa nao Nyerere dhidi ya Uislamu na Waislamu.Kitabu kinaeleza kwa ufasaha jinsi Nyerere wakati alipokuwa madarakani alivyokuwa akifanya mikutano ya siri na viongozi wa Kanisa kuweka mikakati ya kuupa nguvu Ukristo.
Katika mikutano hiyo Nyerere aliwahakikishia viongozi wa Kanisa kuwa anaaunga mkono Ukristo.Kitabu hicho kinaeleza jinsi Nyerere alivyotimiza ahadi yake hiyo kwa Kanisa kwa kuhakikisha kuwa anawapa Wakristo nafasi za juu katika serikali na chama.Kitabu hiki kilikuwa kikiuzwa-Catholic Bookshop, Dar es Salaam. Lakini ilipokuja kudhihirikia Kanisa kuwa kitabu hiki kilikuwa kinatoa habari nyeti na siri za Kanisa kuhusu njama dhidi ya Waislam, kwa haraka sana kikaacha kuuzwa. Hadi hivi sasa kitabu hicho ni marufuku kuletwa tena Tanzania.Kitabu cha pili ni cha Dr John C. Sivalon,-Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985-(1992).
Kitabu hiki kinaeleza njama ndani ya serikali kuuhujumu Uislam. Sivalon anafichua kuwa kuanzia mwaka 1961 baada ya Tanganyika kupata uhuru, Kanisa lilikuwa na hofu mbili. Hofu ya kwanza ilikuwa umoja wa madhehebu za Kiislamu kati ya Sunni, Bohora, Ismailia na Ithnasheri. Hofu ya pili ilikuwa kuhamishwa kwa makao makuu ya EAMWS kutoka Mombasa kuja Dar es Salaam. Kanisa lilikuwa linahofu kuwa mali walizokuwanazo Waasia Waislamu zikitiwa katika shughuli za Waislamu ambao walikuwa na nguvu kubwa katika uwanja wa siasa zitaathiri maslahi ya Ukatoliki katika Afrika ya Mashariki.
Kwa ajili hii Kanisa likatanganza kuwa Uislamu ni adui wake na ikaanza mikakati ya hujma dhidi ya Uislamu ili kuudhoofisha.