THE BIG SHOW
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 18,543
- 14,803
Mohamed said Mudeeer maandiko yako yameufungua ulimwengu.
Reactions tunaziona sasa.
Reactions tunaziona sasa.
Wakati mwingine tubishana naye ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Anachojua ni kwamba waislamu wanaonewa basi. Kuna hoja nyingine kwa makusudi hataki kujibu. Tatizo anapotosha wengi.
To be honest kuna sehemu anakuwa na hoja lakini kamwe hawezi kuangalia upanda wa pili. Umeona Prof. Hirji alikuwa alikuwa anaangalia pande zote. Juzi imetokea ESCROW na watu wenye mawazo finyu wanasema wahusika ni wakristo. Kiongozi mkuu wa nchi na makamu wake ni waislamu. Ina maana wamekaa kimya wakati hao wakristo wanatafuna ma hela ya ESCROW.
Mi nilimuelewa mzee Said aliposema lengo ilikuwa ni kueleza historia ya wazee wake waliosahaulika katika historia. Hilo jina la kitabu kaliweka kuvutia wasomaji, ila maelezo ya ndani ni kwa ajili ya wazee wake. Kwa lengo lake hilo alifunga fikra zake kufikiria kuwa 'heroes' waliosahaulika au wasiotajwa si wazee wake tu.
Nimependa Prof Hijri alivyoeleza kuwa kwenye jamii yetu hii waliosondwa vidole vya uovu wanatoka makundi yote. Sijafanya tafiti ila nimeona kwa jamii. Na siku zote huwa nawashangaa wanao nasibisha uovu katika jamii na imani tulizoletewa. Mi naamini hata huko waliko wakristo wengi au waislamu wengi lawama za uonevu kati yao zipo tu, sembuse sie tulioletewa.
Prof. Hirji mwenyewe kutoka kwenye kinywa chake ni lini alipokujajua kuwa
historia ya uhuru wa Tanganyika ina upungufu.
Na baada ya kusoma paper yangu, "Tanzania: "Nation Without Heroes,"
au kabla ya hapo?
Inawezekana wako wengi waliodhulumiwa lakini dhulma dhidi ya Waislam
ina historia yake ya pekee.
Katika uzi huu nimeweka kisa cha Sergeant Rashid Zahaki kama kilivyoandikwa
na Prof. Njozi katika kitabu chake "Muslims and the State in Tanzania.''
Nimeweka pia hutoba ya Mzee Kitwana Kondo ndani ya Bunge mwaka 1999
Matumbo,
Hilo la MUM na Prof. Njozi tujaalie tunaweza tukaliingiza hapa lakini naona
ingependeza tupate jibu kutoka kwa muhusika mwenyewe.
Mimi niko na nyinyi kwenye paper yangu: "Tanzania: "A Nation Without Heroes"
na "critique" ya Prof. Hirji iliyoletwa hapa.
Mzee Mwanakijiji anaita historia za hisia "HISTOHISIA"
Prof Karim anasema beating drums on one side confusing both
Lakini umeshindwa kujibu hoja zake, unachofanya ni kuleta nukuu kuonyesha ni namna gani waislamu wamekuwa wakilalamika.
Prof Hirji ameonyesha jinsi ni kiasi gani history inazungumza kuwa watu walipata magumu mengi lakini haikuwa sababu ya imani zao. Ameonyesha ni kiasi gani waafrika wa Tanganyika waliunganishwa na kiu yao ya kupata uhuru, kinyume na upotoshaji wako.
Matumbo,
Nukuu ndiyo ushahidi wa majibu ya maswali.
Ukikataa nukuu yaani rejea sasa hapa tutatunia nini kutia uzito hoja zetu?
Critique haitoshi kujibu kitabu changu.
Nitakupa mfano mdogo kutoka kwako mwenyewe.
Kabla ya mimi kuandika habari za Abdul Sykes wewe ulimjua na uliyajua
yote aliyofanya katika TAA, TANU na kwa Nyerere mwenyewe?
Hutoweza hata siku moja kunijibu kwa "critique," ikiwa mimi katika hayo
nimesema uongo.
Majibu ya uongo wangu utaweza kuyaleta kwa wewe kueleza ukweli.
Ukweli huu hutaweza kuueleza ila uandike kitabu.
Mkuu Mohamed Said
Hoja alizotoa Prof. Karim Hirji zinazima madai yako yote unayotoa sehemu mbalimbali juu ya kile unachokiita "kuonewa kwa waislam Tz". Hisia za UDINI ndio zinakuongoza. Na kwa jinsi hii ni ngumu kushawishi umma wenye kuweza kupambanua ukweli ni upi. Hoja zako ziko bias sana hata mtoto wa primary atatambua wewe ni MDINI. Ndiyo, wewe ni mdini kwa sababu unafungamanisha hali mbaya za waislam hapa nchini kuwa ni matokeo ya "mfumo Kristu" kitu ambacho si kweli. UNAWAGAWA WATANZANIA.
ACHA MARA MOJA.
Mohamned Said kaachwa mtupu. Kuna vitu viwili muhimu sana hapa. Kwanza hoja za kisayansi za Prof. Hirji. Pili prof sio Mkristo maana kwa kurunzi ya Mohamned Said hilo lingekuwa tatizo.
Wanyonge wa Tanzania ni dini zote. Mafisadi wa Tanzania ni dini zote.
Nadhani hapa unamnukuru Kitwana Kondo mwaka 1999. Kama ilikuwa kweli basi sidhani kuwa mambo yatakuwa yamebadilika hadi leo.
Kwa kweli imani yako imefunika kila kitu unabakia tu kuamini chochote kile mradi tu kielezee mambo ya kuonewa kwa waislamu. Hata kama kimetungwa. Hivi kweli unaamini kuwa wanafunzi waliofanya mtihani darasa la 7 mwaka 1999 walikuwa asilimia 71 ni waislamu na asilimia 29 ni wakristo? Ukifanya hesabu za haraka haraka tu utaona kuwa waislamu Tanzania bara wapo kwa asilimia kubwa mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga. Mikoa ya DSM, Tabora, na Kigoma ni mchanganyiko. Mikoa iliyobakia wakristo ni wengi kwa mbali sana.
My cousin K. HIRJI is an opportunist trying to sacrifice Prof. Mohammed Said at a behest of publicity that is all. Indeed if Mr. Mohammed Said had not dared written this version of history Karim would not peep out of his comfort zone.
Mwanakijiji,
Mimi nimekuja na historia ambayo si wengi walikuwa wamepatapo
kuisikia.
Haikuwepo kabisa.
My cousin K. HIRJI is an opportunist trying to sacrifice Prof. Mohammed Said at a behest of publicity that is all. Indeed if Mr. Mohammed Said had not dared written this version of history Karim would not peep out of his comfort zone.