Maamuz ya Ajabu sana.
Kuna wakulima wamekopa pesa benki kulimia Mazao alafu bei itakuwa chini kwa ķukosa soko. sijui watalipaje mikopo.
Wakulima wakiona kilimo hakilipi, watapunguza uzalishaji. Wenye malori watakosa mizigo, mabenki yatapungukiwa wateja wa kukopa,makampuni ya mbegu na madawa ya kilimo yatapunguza uzalishaji,mbolea zitakosa soko lililoķua linakua,
Umaskini utaongezeka hasa vijijini,vijana watazidi kuja mijini kuwa wamachinga kwani hawataona tija kwenye kilimo,na wakija mijini ambako hamna kazi wataishia kwenye umachinga na kujenga makazi holela mabondeni.
Kwavile mauzo ya Mazao nje yatapungua,tegemea shilingi kuzidi kushuka thamani.Tegemea pia wenye maduka ya bifhaa nyingine kupungukiwa na wateja kwani wakulima wengi watapungukiwa pesa. Biashara zitazidi kudorora. Umaskini utaongezeka Bali wachache kama wahindi wenye viwanda watanufaika kwakua watanunua Mazao bei ya kutupa, watasindika na kuuza nje bei ya juu. Si unajua wenye viwanda hawabanwi sana.
Yani siasa za bongo ni shida.