dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 22,129
- 49,391
Hapa ndo ungetegemea wale viongozi wetu wa dini wasimame na kukemea bila chenga utovu huu mkubwa uliooneshwa na kiongozi huyu tena si kiongozi wa kisiasa (mbunge) tu bali pia kiongozi wa kijamii (M/Kiti wa Simba Sports Club). Lakini la ajabu hutasikia lolote kutoka kwa wadini hawa! Rage kusimama na kuonesha bastola yake hadharani anataka kupeleka ujumbe gani kwa jamii? Anataka jamii iige nini kutokana na hilo? Anataka vijana waige nini? Anataka wenye mitazamo mikali ya kidini (fundamentalists) wafikiwe na ujumbe gani? Anataka mashabiki wa Simba na vilabu vingine wajifunze nini? Au pia anakusudia kufikisha ujumbe gani kwa wana-CCM wenzie? Sijajua hasa lengo lake.
Lakini viongozi wetu wa dini kimyaaaaa! Ama kweli, kwa unafiki wao, wanafiki huchuja mbu na kumeza ngamia; yamepata kunena hivyo maandiko fulani. Well, labda ni mapema mno, huenda watatoa tamko.
Lakini viongozi wetu wa dini kimyaaaaa! Ama kweli, kwa unafiki wao, wanafiki huchuja mbu na kumeza ngamia; yamepata kunena hivyo maandiko fulani. Well, labda ni mapema mno, huenda watatoa tamko.