Acheni ujinga, siyo kila kitu kina ushahidi wa mazingira, maandishi au picha, hii siyo mahakama. Huenda amri iliyotolewa ni ya mdomo (matamshi) tu. Labda ukamuulize Basilio mwenyewe!
Mimi namsifu afande kwa kuheshimu maadili ya kazi yake na kumheshimu Mungu pia, siijui dini/imani ya kamanda Basilio lakini inaonekana hawezi kuuwa binadamu asiye kuwa na kosa kwa utashi wa mtu mwingine. Aliyetoa amri ya kuua 5 kwa sababu ya kumuokoa mbunge wake kwa sababu wana toka dini moja, nadhani hapa kuna haja ya kuwa na mashaka na imani au dini zao kama msingi wake ni amani!
EL pamoja na ufisadi wake lakini imani/dini yake ali-iheshimu sana aka-amua kutumia njia mbadala, badala ya kuua watu live, aliona bora atumie mlungula, alikuwa tayari apoteze hata 800 millioni kwani atazitafuta zingine kifisadi fisadi.
Basilio wala asijali kwani kuna maisha hata akivuliwa unjagu, kwani siku hazigandi 2015 CDM watakurudisha kazini kwa record yako ya kuzingatia maadili ya kazi yako siyo utashi wa mtu.