Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Kama mtakumbuka, Basilio Matei ndie alikuwa RPC Arusha wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010. Matei ni miongoni mwa RPC wachache sana ambao katika utendaji wao huzingatia zaidi haki kuliko matakwa ya chama tawala, na hivyo serikali ya chama hicho hakupendezewa na alichokifanya Arusha siku ile ya kutangaza matokea ya kura za ubunge ambapo kulikuwa na ucheleweshaji mkubwa sana wa bila sababu za msingi.
Kama mtakumbuka, ilipofika majira ya jioni na bado matokeo yalikuwa hayajatangazwa na umati mkubwa wa watu kufurika nje ya ofisi za halmashauri -- wafuasi wa CDM na pia wa CCM, RPC Matei personally alikwenda kwenye ofisi hizo kuwasihi wahusika (Mkurugenzi na timu yake) kutangaza matokeo (yoyote yale) kabla giza halijaingia lau sivyo jeshi la polisi lisingeweza kumudu ghasia ambazo zingetokea iwapo matokeo yangeendelea kutotangazwa na kutangazwa usiku.
Alikuwa na sababu za msingi kabisa kufanya vile katika kusimamia usalama na amani katika eneo lake.
Hatimaye yalitangazwa kwa Lema kuwa msindi. hata hivyo serikali haikupendezwa na alichokifanya RPC huyo -- yaani kushinikiza matokeo yatangazwe haraka kwani hatua hiyo iliikosesha serikali na 'vyombo' vyake muda wa kuchakachua matokeo na kumtangaza Batilda kuwa mshindi. Tusisahau poia hapa kwamba vigogo kadha wa CCM walikwenda katika ofisi za kuhesabu kura mchana ule wakati matokeo yanangojewa, akiwemo si mwingine bali EL.
Siku chache tu baadaye alihamishwa ghafla, nakupelekwa makao makuu Dsm na badala yake kumuweka Andangenye.