Basi gani la mkoani ulipanda ukajutia?

Basi gani la mkoani ulipanda ukajutia?

Sai Baba, nilikuwa natoka Arusha kwenda Dar. Usiku kabla ya safari nililala late sana, nikayachelewa mabasi ya mapema.

Hapo ndiyo nikakutana na hicho chuma, nikakikwea. Nadhani ndiyo kilikuwa kinatoka body, kilikuwa bomba sana.

Ila kilipoanza kutembea tu, fasta nikagundua kuwa nimeyatimba.

Hiyo ilikuwa ni miaka mingi sana iliyopita, so sijui sasa mabasi yao yakoje, ila tangu wakati huo hayo mabasi sina mpango nayo.

Ova
Hadi umenikumbusha story yangu na mimi ya adha ya usafiri wa mabasi, zipo 2 ila hii ilikuwa kali zaidi.

Ilikuwa safari ya Dar Arusha nikachelewa kidogo kufika Ubungo magari yameshaondoka mengi likawa limebaki Osaka, hapo saa mbili asubuhi. Picha linaanza gari likaondoka pale saa 5, niliteseka sana njiani gari halitembei linasimama kila mahali kuokoteza abiria.

Tulifika Arusha saa 6 usiku, na nilikuwa binti mdogo wa miaka 20 ilibidi mama anisubiri usiku wote huo stendi peke yake.
Tokea hiyo siku mimi na mama tuliapa kutokupanda Osaka maisha yetu yote, ni bora tuahirishe safari.
 
Kuna Bus jina lake limenitoka Dar - Mwanza, picha linaanza Tv ipo pale kwa dereva kwenye dashboard yake, alafu anasimulia hiyo movie anayotizama kwa sauti mpaka watu wa siti ya mwisho anataka wasikie.
Nimepitiwa na usingiz kuja kuamka kofia yangu kavaa yeye dereva afu nipo siti ya kati kati nikajiuliza imemfikiaje😂.
Wanauza maji ila wanasema hatukupi mpak tusimame sehemu tusije tukakupa ukatusumbua mkojo.
Kila abiria ana tiketi ya rangi yake mwingine njano mwingine nyekundu acha tuu.
Mara konda aje asemw jamani tunapiga self wote tuseme ndiziii ili apost kwenye page ya UNICEF sijaelewa mpaka leo.
Wakaanza kubishana Ali kiba vs Diamond, dereva na konda
Nimecheka mpaka nimebubujikwa machozi ya furaha kama Lucas Mwamshamba
 
Siyo moja kweli? Mimi nilipanda hilo Happy Africa linatoka Ludewa linapita kijiji chetu kipo mbele ya Ludewa saa 11 alfajiri.

Kwa hesabu zangu za haraka nikajua Dar tutafika mchana. Gari likasimama Makambako kama masaa manne, likaanza safari hivyo hivyo Mikumi tukafika saa 4 usiku, tukakuta Twiga wapo barabarani ikabidi tusubiri watoke.

Dar tukafika saa 7 usiku.

Next time nikiwa narudi tena Dar walivyonitajia nikawaambia sipandi hilo gari wakajibu siku hizi kachukua Luwinzo.

Sasa hapo labda nilichanganya kusikia Africa
Ilo hapo
 
Attachments

  • IMG-20240626-WA0255.jpg
    IMG-20240626-WA0255.jpg
    17.6 KB · Views: 11
Hadi umenikumbusha story yangu na mimi ya adha ya usafiri wa mabasi, zipo 2 ila hii ilikuwa kali zaidi.

Ilikuwa safari ya Dar Arusha nikachelewa kidogo kufika Ubungo magari yameshaondoka mengi likawa limebaki Osaka, hapo saa mbili asubuhi. Picha linaanza gari likaondoka pale saa 5, niliteseka sana njiani gari halitembei linasimama kila mahali kuokoteza abiria.

Tulifika Arusha saa 6 usiku, na nilikuwa binti mdogo wa miaka 20 ilibidi mama anisubiri usiku wote huo stendi peke yake.
Tokea hiyo siku mimi na mama tuliapa kutokupanda Osaka maisha yetu yote, ni bora tuahirishe safari.
Nifah miaka 20 ww mdogo? Wakati unge
Nimecheka mpaka nimebubujikwa machozi ya furaha kama Lucas Mwamshamba
Kuna wajinga humu wanachekesha mpaka watu wakikuona wanafikiri unachizj🤣
 
Kuna Costa nilipanda Karatu Arusha likaharibikia mto wa mmbu najiuuta mmbwa wale hawakutufaulisha
 
Abood Yani hili gari Kila nikipanda lazima nikasirike maana lipo slow halafu likifika moro lazima tukawangiwe kule kwenye karakana Yao.Yani kama bwna Abudi anasoma huku aache huu ujinga halafu Kila siku nasema sipandi tena ila nakuta napanda Sasa sijui Kwann
 
Kwa sababu ratiba zako zinalingana na lenyewe. Ingekua mnapishana ungetafuta jingine
 
Hadi umenikumbusha story yangu na mimi ya adha ya usafiri wa mabasi, zipo 2 ila hii ilikuwa kali zaidi.

Ilikuwa safari ya Dar Arusha nikachelewa kidogo kufika Ubungo magari yameshaondoka mengi likawa limebaki Osaka, hapo saa mbili asubuhi. Picha linaanza gari likaondoka pale saa 5, niliteseka sana njiani gari halitembei linasimama kila mahali kuokoteza abiria.

Tulifika Arusha saa 6 usiku, na nilikuwa binti mdogo wa miaka 20 ilibidi mama anisubiri usiku wote huo stendi peke yake.
Tokea hiyo siku mimi na mama tuliapa kutokupanda Osaka maisha yetu yote, ni bora tuahirishe safari.
Pole sana b... kwa huo wakati hadi uliweza kuhisi unaweza kufika safari kesho yake. Lol

Ila mama aliteseka mno siku hiyo.

Ova
 
Back
Top Bottom