Basi gani la mkoani ulipanda ukajutia?

Basi gani la mkoani ulipanda ukajutia?

Nilikata kidinilo muda wa safari wanasema halipo tukapewa lingine sikumbuki jina tumepanda nimekaa karibu na mlango wa dharura aise Barabara zimechimbwa vumbi la njiani lote linaingia ndani pumzi inakata nikasimama ili kukwepa kuoga vumbi mpaka kwenye lami tulioga vumbi haswa kufika ubungo ilibidi kuoga Kwanza
Hii ilikuwa ni safari ya Ifakara Dar bila shaka. Bora lami ikamilike sasa ili haya mambo yabakie tu kuwa ni historia. Hiyo barabara ilikuwa inachosha sana.
 
Hapana. Luwinzo basi zake nyingine huwa anaziita Sweet Africa.

Hizo Happy Africa zilikuwa ni basi fulani hivi kuukuu za bodi ya kuchonga! Za jamaa mmoja wa Mafinga. Kuna msimu mmoja wa sikukuu nilikosa usafiri wa uhakika wa kwenda Njombe pale Ubungo, nikalazimika kupanda hilo basi. Kiukweli ile safari ilikiwa ni ngumu sana.
Siyo moja kweli? Mimi nilipanda hilo Happy Africa linatoka Ludewa linapita kijiji chetu kipo mbele ya Ludewa saa 11 alfajiri.

Kwa hesabu zangu za haraka nikajua Dar tutafika mchana. Gari likasimama Makambako kama masaa manne, likaanza safari hivyo hivyo Mikumi tukafika saa 4 usiku, tukakuta Twiga wapo barabarani ikabidi tusubiri watoke.

Dar tukafika saa 7 usiku.

Next time nikiwa narudi tena Dar walivyonitajia nikawaambia sipandi hilo gari wakajibu siku hizi kachukua Luwinzo.

Sasa hapo labda nilichanganya kusikia Africa
 
Kipindi hicho nilipanda MJ safari, gari watu wanakula muda wote, sio mayai ya kuchemsha wala mahindi ya kuchoma, hawachagui hawabagui. Mmoja tunafika Morogoro akajinyea kwenye bus, harufu yake mule ndani haifai. Nilikoma kabisa siku hio.
🀣🀣🀣acha tuongeze siku za kuishi watu mnavituko 🀣🀣🀣mtu kujinyea🀣🀣🀣
 
Kipindi hicho nilipanda MJ safari, gari watu wanakula muda wote, sio mayai ya kuchemsha wala mahindi ya kuchoma, hawachagui hawabagui. Mmoja tunafika Morogoro akajinyea kwenye bus, harufu yake mule ndani haifai. Nilikoma kabisa siku hio.
ChaiπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kuna Bus jina lake limenitoka Dar - Mwanza, picha linaanza Tv ipo pale kwa dereva kwenye dashboard yake, alafu anasimulia hiyo movie anayotizama kwa sauti mpaka watu wa siti ya mwisho anataka wasikie.
Nimepitiwa na usingiz kuja kuamka kofia yangu kavaa yeye dereva afu nipo siti ya kati kati nikajiuliza imemfikiajeπŸ˜‚.
Wanauza maji ila wanasema hatukupi mpak tusimame sehemu tusije tukakupa ukatusumbua mkojo.
Kila abiria ana tiketi ya rangi yake mwingine njano mwingine nyekundu acha tuu.
Mara konda aje asemw jamani tunapiga self wote tuseme ndiziii ili apost kwenye page ya UNICEF sijaelewa mpaka leo.
Wakaanza kubishana Ali kiba vs Diamond, dereva na konda
Nikipata pesa na mimi nitapanda basi ,mnapata raha kiasi hiki? Comedy za kutosha🀣
 
Happy Africa ni Luwinzo
Sio kweli
Luwinzo ni Sweet Afrika labda Kama umechanganya.
Happy Afrika ilikuwa ya bwana mmoja hivi wa Mafinga jina lake ljnafanana na jina la miongoni mwa wanafunzi wa Yesu.
Ilikuwa bluu hivi wakati Luwinzo hata kipindi ni Stamili sidhani Kama amewahi kuwa na rangi ya bluu
 
Route ndio alichukua Luwinzo
Siyo moja kweli? Mimi nilipanda hilo Happy Africa linatoka Ludewa linapita kijiji chetu kipo mbele ya Ludewa saa 11 alfajiri.

Kwa hesabu zangu za haraka nikajua Dar tutafika mchana. Gari likasimama Makambako kama masaa manne, likaanza safari hivyo hivyo Mikumi tukafika saa 4 usiku, tukakuta Twiga wapo barabarani ikabidi tusubiri watoke.

Dar tukafika saa 7 usiku.

Next time nikiwa narudi tena Dar walivyonitajia nikawaambia sipandi hilo gari wakajibu siku hizi kachukua Luwinzo.

Sasa hapo labda nilichanganya kusikia Africa
 
Gari zote tu ambazo safari zake zina wasukuma,wamangati, wamasai , watu wa tabora , kahama ,shinyanga ,dodoma kwenda kondoa......aisee hizi gari ni hazifai kunguni, chawa, mende ustaarabu zero usiombe ukabahatika kukaa siti moja na wale wavaa mashuka wananuka samli tu muda wote wanalamba ugoro. Kuna bibi mmoja alitema kohozi nje likarudi ndani siti ya nyuma yake likamnata jamaa sikioni.

Hiyo moja kioo cha dirisha hakikuepo makonda walishikilia boks kuziba upepo mwanzo mwisho.

Hizo tripu popote kambi
Mmasai kabeba ugoro kilo 2 , gari zima anatema mate yeye tu. Mwenyew anaita "Reja"
 
Machame coach,,,nilikata tiketi ya bus la saa moja na nusu coz lilikuepo na la saa moja kamili,,,bwana weeee kumbe bus la saa moja na nusu linapita saa mbili na la saa moja kamili linapita saa moja na nusu,,ile kuzama ndani sasa nashangaa mbona siti yangu sioni nkavunga,,safari ishapamba konda kukagua tiket sio ya gari yao ambalo ilibidi nipande lipo nyuma,,wakawasiliana wanavojua wao,, safari nikaendelea.

Arusha to Dodoma.
 
Bus ya kuitwa Shukurani Dar - Dom hata kama imebaki yenyewe sipandi.
Bus ya kuitwa Fikoshi sipandi bora niahirshe safari.
Niliwahi kupanda iringa - Mwanza gari ilkuwa fikoshi au premier(nimesahau).
Ila yote yalikuwa yanaongozana halafu yote miyeyusho.
Sitasahau, nilisimama kutokea iringa mpaka nimefika Singida ndio nikapata siti.
 
Nawaza aibu hii.. Kuna mwamba tumbo lilimchafuka tunatoka Dar kwenda Njombe, njiani alisimamisha gari zaidi ya mara 3. Ila yeye sikumuona anakula kula vibaya. Ile aibu haielezeki.

Sema mwamba akajiongeza, tumefika Mikumi kuna mtu alikua anashuka. Jamaa nae akaona ashuke safari iishie hapo, akihofia anawasimbua abiria ile simama simama.

Sema kuna faza alikua amekaa nae akasema hapana dogo shuka, kajisitiri tunaendelea wote ata ukisimamisha mara 10 na abiria wengine walisupport.
Hata huyo nae ilibidi ashukie njiani na sio sababu ya kula kula basi tu bahati mbaya ilimkuta ambae hata mimi na wewe inaweza kutukuta sema ni bonge ya aibu
 
Back
Top Bottom