Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Hii ni ccm mpya ya JPM tuwaache na yao.
 
Ni wazo tu...kwamba sio lazima Membe amkwamishe Magufuli ndani ya CCM. Muungano wa Membe, Lissu na Lowasa nje ya CCM unaweza kumuondoa Magufuli madarakani mwaka 2020. Magufuli na CCM yake wasidhani wamesimama thabiti kiasi hicho.

Na ni wazi kwamba ndani ya CCM Membe hawezi kumtikisa Magufuli.
Kuna baadhi ya moderators sijui JF inawaokota wapi maana naona kama akili zao haziko sawa. Hivi wameona hii thread ya "Muungano wa Membe Lowasa na Lissu nje ya CCM unaweza kumng'oa Magufuli" ni thread inapaswa kuunganishwa na thread ya "Membe Vs Bashiru"? Hivi ni vitu viwili tofauti, huyo moderator aliyeunganisha hizi thread anashindwaje kuona hilo? Baadhi yenu moderators mnakera sana. Kama hamtaki tuweke thread wekeni nyie basi.
 
Mtu mmoja anapoitwa na taasisi ambayo yeye ni mwanachama wake inawezaje kuathiri umoja wetu kama Taifa?
sisi watanzania vipaumbele vyetu siyo nani kaitwa na nani bali uhakika wa masoko kwa mazao yetu,sera bora kwa biashara zetu halali na mifumo bora ya kutuhudumia.
 
OK-- wewe ndo hukuelewa.. nasema nataka Membe awe Rahisi na hoja yangu nikutaka wafanyakazi kula bata za maposho na safari kuliko wa sasa anawekeza kwenye miradi ya Maendeleo tu nakutuacha sisi bila mafungu kama zamani


Hivi katika Kiswahili chetu tuna neno Rahisi au Rais? Huwa sipendi na nachukia mno kama siyo sana kuona Mtanzania tena mwenye Kiswahili chake ' Kiutambulisho ' anakikosea halafu Wageni wanakipatia 100%.
[/QUOTE]

Naona bado utakuwa una ' Familiarize ' na JamiiForums App Mkuu kwani kuna ' Upopoma ' nauona unaufanya. Anyways karibu sana.
 
Yote yataishia sirini au yataanikwa?


Mwanzoni watafanya siri ila mwishowe kila mmoja atakuja kivyake kumtuhumu mwenzie kuwa ana vidole vikubwa inabidi ashitakiwe na kufungwa au kupotezwa kabisa kisha wanaanza kumchamba kwamba fulani alikuwa mwehu, au alikuwa vile.
 
Watu hawata amini lakini nawaambia wana JF Bernard anatemeshwa uanachama! KM hakukurupuka kwa ile kauli, ile ni kauli ya kimkakati kabisa aliyotumwa kuitoa na vyombo vya kimkakati

Bernard alitakiwa atoe kauli kama ile aliyoitoa ya kujibu ili ipatikane sababu na uhalali wa kumuita iwe kwa heri au kwa shari. Inajulikana kwamba yeye hatakuja kipindi cha hivi karibuni

Kwa kufanya hivyo mchakato wa kumvua uanachama utaanza. Kitakacho tokea watajitokeza wa kumtetea kwa kupinga utaratibu utakaotakaka kumtimua Bernard kwa sababu kuthibitisha kosa lake ni vigumu

Hapo pia panasubiriwa kwa hamu kwa sababu wanatafutwa waungaji mkono wake, na wote wataopinga Bernard kuadhibiwa watachukuliwa kua ni timu Bernard na watadhibitiwa vilivyo. Udhibiti huu waweza kuhusisha vyombo kadhaa kama vile vya ukusanyaji mapato, udhibiti rushwa, vyombo vya ulinzi na usalama na hata kutumbuliwa kutoka kwenye nafasi au ajira zao

Jambo hili lina blessings za PM mstaafu ambaye siku hizi anasifiwa sana na wakuu wa chama tawala. PM mstaafu kasahau kua wafuasi wake wengi wamekua persecuted na kua victimized kwa kule tu kua waliwahi kumuunga mkono
Likifanyika hili kwa mgogoro huu uliopo itakuwa sawa na kumwaga petrol kwenye moto. Tukiacha unafiki wa kisiasa ukweli ni kwamba Magu ameshachokwa ndani ya ccm na hata vyama vya upinzani wanaona bora aje kiongozi mwingine hata kama wa ccm ili wapambane naye kwa siasa za kistaarabu. Lengo kuu la Magu ni kutaka kuua mfumo wa vyama vingi ili baadaye aitawale Nchi milele, na haya yametokana na Mkakati na maelekezo toka kwa Kagame. Lakini alichoshindwa kuangalia ni kuwa Tanzania ni tofauti na Rwanda. Walioongoza awamu 2, 3. na 4 wapo ukiachilia wengine wenye chama chao tofauti na Rwanda ambapo Kagame yupo pekee hivyo hakuna wa kumnyooshea kidole baada ya kufanikiwa kuwaua waliomtangulia na baadhi ya wale aliyokuwa nao kwenye chama Chake wakati walipoanzisha uasi
 
2020 twende na Membe huyu mpuuzi nchi imemshinda.
1544005046283.png
 
Back
Top Bottom