Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

“Ni kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Katibu Mkuu kukutana na viongozi na wanachama wa CCM katika kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa wanachama.”
TUSIJEKUSIKIA AMETIMULIWA... VITA YENU YA NDANI INAMANUFAA SANA KWA WAKATI HUU
 
Episode 1: Ikaripotiwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Dr. Bashiru Ally Kakurwa amemuita, kupitia vyombo vya habari aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Camilius Membe kuzungumza naye juu ya tuhuma dhidi ya Membe ya kuanza kusaka kura za Urais za mwaka 2020.

Episode 2: Ikaripotiwa kuwa Membe, kupitia mitandao ya kijamii, akamjibu Dr. Bashiru. Pamoja na mambo mengine, Membe aliyaweka wazi mambo makubwa yafuatayo. Mosi, alikubali wito wa Katibu Mkuu wake na kuahidi kwenda kumuona atakaporejea nchini kwakuwa kwasasa yuko nje ya nchi. Pili, Membe aliomba 'muunda tuhuma' Cyprian Musiba awepo ili ajibu tuhuma zake. Tatu, Membe alikosoa namna alivyoitwa na Katibu Mkuu na kusema kuwa Katibu Mkuu ni mgeni kwenye uongozi wa chama.

Episode 3: Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru Ally Kakurwa hakusema ndiyo au hapana kuhusu ombi la Membe la uwepo wa Musiba katika kukutana kwao ili Membe asikie tuhuma zake na kuzijibu.

Episode 4: Ikaripotiwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru Ally Kakurwa amemjibu Membe kuhusu ugeni wake ndani ya CCM kwa kusema kuwa yeye Katibu Mkuu ni mgeni kwenye Team Lowassa na Team Membe lakini si mgeni CCM na taratibu zake.

Episode 5: Imeandikwa na gazeti la leo la Mwananchi kuwa mkongwe wa siasa na uongozi wa hapa nchini, Mzee Pius Msekwa amemkosoa Katibu Mkuu wa CCM hasa katika namna alivyomuita Membe. Msekwa amesema kuwa ni afadhali Katibu Mkuu angetumia barua au simu kumuita lakini si njia iliyotumika.

Episode 6: Dr. Bashiru na Membe wanakaribia kuonana. Wameshajibizana, kukosolewa na kuungwa mkono na watu mbalimbali ndani ya chama chao na hata nje ya chama chao cha Mapinduzi. Wote ni binaadamu wenye hisia za kufurahi na kuchukia. Watatazamana na kuzungumza vipi kiutulivu watakapokutana kwa uwepo wa yaliyotokea baina yao?

Political Forecast: CCM inamuandaa mgombea wa Urais wa 'kumsimamisha' upinzani mwaka 2020!
 
Ili maandiko yatimie hayana budi haya kutokea. Kiburi cha mfalme.
 
B2033C8F-3E15-4D8D-B481-EF1BF53B26C8.jpeg

Watatazamana kwa macho na kusikilizana kwa masikio yao, BTW
Dr Bashiru kashaharibu anatafuta huruma ya wenzake na Polepole kaanza kumsaidia
 
Wakikutana watapigana vidole tu kuonyeshana nani atamuumiza mwenzie zaidi.
 
Siasa ndani ya CCM ndivyo zilivyo miaka yote hasa baada ya Mwinyi kuondoka.Uzuri wa miaka ya nyuma ni kuwa waliokuwa na nia ya U rais walikuwa wanasiasa na kwa mantiki hiyo walikuwa na uwezo angalau wa kufuata misingi ya Uanasiasa kama uvumulivu.Kikwete alimuachia Mkapa na pamoja na kujenga mtandao wake (ambao I am sure Mkapa alikuwa anaujua)Mkapa hakumzuia ila alimlea na kumpa Uwaziri wa mambo ya nje kwa miaka kumi.Kikwete akaiva katika siasa na diplomasia.
Kwa sasa kuna hofu kuu ambayo walioko madarakani wameitengeneza wenyewe.Huwezi kuwa unalalamika kila siku kuwa U raisi ni mzigo wakati kuna watu wanaona U raisi ni fursa ya kuwatumikia wananchi.Kwa ulalamishi uliopo nahisi kuna watu ambao wanajianda kuchukua nafasi na bahati mbaya watu hao ni waandamizi ndani ya Chama chetu.MNYUKANO!!!
 
kosa moja alilofanya na analoendelea kufanya magufuli ni kufikiri kila msomi ni kiongozi mzuri bashiru pamoja na usomi wake hazielewi wala hazijui siasa mambo yote ameyakuza yeye kama alikuwa na haja ya kumwita membe angetumia taratibu za kawaida na sio kuropoka majukwaani asipoangalia atabaki kuwa katibu kichekesho
 
Yanasemwa mengi na yatasemwa mengi ila kama kuna Kosa kubwa ambalo Rais Dkt. Magufuli amelifanya ( na naamini hapa atakuwa alishauriwa vibaya na Watu wake ) ni kuweka mbali au kukaa mbali na ' Fundi wa Diplomasia ' Benard Membe na kwa maoni yangu huenda leo hii tunaona baadhi ya matatizo ya hapa na pale yanatokea hasa Kimataifa kwakuwa hana ' Mafundi ' kama akina Membe.

Hata kama huyu Mtu ( Membe ) aliamua Kuachana na Ubunge lakini Mimi kama GENTAMYCINE bado naamini kwamba Mheshimiwa Rais Magufuli kwa ' Mandate ' yake kama ' Executive ' bado alikuwa anaweza Kumtumia katika ' Baraza ' lake la Mawaziri au hata katika maeneo mengine hasa ya Kidiplomasia ambayo kwa Mimi naona kwamba hadi hivi leo bado tunafanya vibaya na mifano juu ya hili iko mingi tu.

Kwa Mtu mwenye ' exposure ' kubwa na ' iliyotukuka ' kabisa huku akiwa amewahi Kuhudumu katika moja ya Idara / Taasisi muhimu / nyeti Kiusalama katika nchi hii kama Mzee Benard Membe leo hii kumuacha awe tu hivi ' huru ' nadhani ' technically ' kabisa hapa kuna Kosa kubwa sana lilifanyika ama kwa Watu kutokujua au Mheshimiwa Rais Magufuli alilishwa ' Sumu ' za ' Kimajungu ' na Watu wake wa karibu ambao anawaamini nae ' Sumu ' ikamuingia vilivyo na matokeo yake ndiyo haya sasa.

Sehemu yoyote ile hasa kwa Watu wenye ' akili ' sawasawa pale ukishaona kuwa Mtu fulani bado ana ' Potential ' fulani katika nchi ambayo ina Tija ya Kimaendeleo basi yakupashwa uendelee Kumuamini na Kumtumia ila kama pia umeona mwenyewe kwa Vipimo vyako kuwa GENTAMYCINE ni ' Tishio ' Kwako basi njia pekee ya Kumuweza ni ' Kumjumuisha ' katika ' Utawala ' wako ili uweze Kumlevya Kimamlaka lakini pia Kumdhoofisha ' Kimbinu ' pasipo Yeye kujua lakini kumuacha awepo awepo tu ni hatari kubwa kama ambavyo tunaanza kuiona sasa.

Hata hivyo bado hatujachelewa na hasa hasa Rais Magufuli bado hajachelewa kwani Mimi GENTAMYCINE naamini tena kwa 100% kuwa Mzee Benard Membe anaweza kuwa ni ' msaada ' mkubwa mno wa Kiutawala Kwake ama kwa huu muda alioubakisha kwa muhula wale huu wa Kwanza au hata kwa muhula wake wa pili na mwisho. Asiwasikilize wale ' Wanafiki ' ambao wamemzunguka na ambao hata Yeye pia alishakiri mara nyingi tu kuwa walishawahi hadi kumwambia kuwa Katibu Mkuu wa sasa wa CCM Ndugu Bashiru Ally Kakurwa hafai lakini Yeye mwenyewe akajiridhisha nae na kuamua kufanya nae Kazi na tunaona anafanya vyema tu.

Yangu ni hayo tu ila Mzee Benard Membe bado ni ' Lulu ' kubwa katika ' Utawala ' huu asiachwe na apewe ' Majukumu '.

Nawasilisha.
 
Kwa taarifa yako hata angekaa naye karibu huyo Membe ndio angefundishwa hiyo diplomasia. Ogopa mtu aliyekuja na mbinu ya kwamba kama una korosho na huna shamba hizo korosho utazila, lakini hatuoni wanaouza magari wakionyesha viwanda walipotengenezea hayo magari, na wanaochoma mahindi humu mjini hawaonyeshi mashamba walipoyalimia. Kipa wa ile timu yako ndio anazingua.
 
Yeye anaamini kuwa hali ikiwa mbaya anaweza akalituma Jeshi kwenda kuomba misaada huko nje.
Yeye haamini katika mgawanyo wa majukumu. Anadharau kazi za kichwa, anadharau kazi za unyeo, anadharau kazi za miguu, anadharau kazi za makalio. Anaamini mikono, virungu na risasi ndiyo jibu la kila kitu.
 
Kambi nzima haina cha fundi wala nini wote hao ni wachumia matumbo; hawana maono ya kutuvusha kutoka kwenye matatizo tuliyo nayo. Haiwezekani kila kukicha matatizo yanaongezeka kwa watanzania wakati tuna rasilimali kibao. Picha chini ccm tuanze upya.
 
Kwa taarifa yako hata angekaa naye karibu huyo Membe ndio angefundishwa hiyo diplomasia. Ogopa mtu aliyekuja na mbinu ya kwamba kama una korosho na huna shamba hizo korosho utazila, lakini hatuoni wanaouza magari wakionyesha viwanda walipotengenezea hayo magari, na wanaochoma mahindi humu mjini hawaonyeshi mashamba walipoyalimia. Kipa wa ile timu yako ndio anazingua.
Nimekuelewa vyema ... uko sahihi. Kiongozi ni lazima atafakari kwanza kabla ya kutoa tamko lolote. Matamshi ya kiongozi yanapoleta mtafaruku hayatatufikisha popote.
 
Yanasemwa mengi na yatasemwa mengi ila kama kuna Kosa kubwa ambalo Rais Dkt. Magufuli amelifanya ( na naamini hapa atakuwa alishauriwa vibaya na Watu wake ) ni kuweka mbali au kukaa mbali na ' Fundi wa Diplomasia ' Benard Membe na kwa maoni yangu huenda leo hii tunaona baadhi ya matatizo ya hapa na pale yanatokea hasa Kimataifa kwakuwa hana ' Mafundi ' kama akina Membe.

Hata kama huyu Mtu ( Membe ) aliamua Kuachana na Ubunge lakini Mimi kama GENTAMYCINE bado naamini kwamba Mheshimiwa Rais Magufuli kwa ' Mandate ' yake kama ' Executive ' bado alikuwa anaweza Kumtumia katika ' Baraza ' lake la Mawaziri au hata katika maeneo mengine hasa ya Kidiplomasia ambayo kwa Mimi naona kwamba hadi hivi leo bado tunafanya vibaya na mifano juu ya hili iko mingi tu.

Kwa Mtu mwenye ' exposure ' kubwa na ' iliyotukuka ' kabisa huku akiwa amewahi Kuhudumu katika moja ya Idara / Taasisi muhimu / nyeti Kiusalama katika nchi hii kama Mzee Benard Membe leo hii kumuacha awe tu hivi ' huru ' nadhani ' technically ' kabisa hapa kuna Kosa kubwa sana lilifanyika ama kwa Watu kutokujua au Mheshimiwa Rais Magufuli alilishwa ' Sumu ' za ' Kimajungu ' na Watu wake wa karibu ambao anawaamini nae ' Sumu ' ikamuingia vilivyo na matokeo yake ndiyo haya sasa.

Sehemu yoyote ile hasa kwa Watu wenye ' akili ' sawasawa pale ukishaona kuwa Mtu fulani bado ana ' Potential ' fulani katika nchi ambayo ina Tija ya Kimaendeleo basi yakupashwa uendelee Kumuamini na Kumtumia ila kama pia umeona mwenyewe kwa Vipimo vyako kuwa GENTAMYCINE ni ' Tishio ' Kwako basi njia pekee ya Kumuweza ni ' Kumjumuisha ' katika ' Utawala ' wako ili uweze Kumlevya Kimamlaka lakini pia Kumdhoofisha ' Kimbinu ' pasipo Yeye kujua lakini kumuacha awepo awepo tu ni hatari kubwa kama ambavyo tunaanza kuiona sasa.

Hata hivyo bado hatujachelewa na hasa hasa Rais Magufuli bado hajachelewa kwani Mimi GENTAMYCINE naamini tena kwa 100% kuwa Mzee Benard Membe anaweza kuwa ni ' msaada ' mkubwa mno wa Kiutawala Kwake ama kwa huu muda alioubakisha kwa muhula wale huu wa Kwanza au hata kwa muhula wake wa pili na mwisho. Asiwasikilize wale ' Wanafiki ' ambao wamemzunguka na ambao hata Yeye pia alishakiri mara nyingi tu kuwa walishawahi hadi kumwambia kuwa Katibu Mkuu wa sasa wa CCM Ndugu Bashiru Ally Kakurwa hafai lakini Yeye mwenyewe akajiridhisha nae na kuamua kufanya nae Kazi na tunaona anafanya vyema tu.

Yangu ni hayo tu ila Mzee Benard Membe bado ni ' Lulu ' kubwa katika ' Utawala ' huu asiachwe na apewe ' Majukumu '.

Nawasilisha.
2020 twende na Membe
 
Alitutoka Mw.Nyerere na bado CCM ikasonga Mh.Mzee kipenzi cha wanaompenda Lowassa akakatwa akaitwa Kamanda baadaye CCM ikasonga.

Huu mziki called Membe umetoka lini?

Mashabiki ni wakina nani Kama ZITTO na MNYIKA wanaupenda basi utakuwa mzuri.
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania kuhusu matokeo ya uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 47 Tanzania Bara uliyofanyika tarehe 02 Desemba 2018 na kwamba CCM imepita bila kupingwa katika Kata 41 na katika Kata 6 ambako kumefanyika uchaguzi CCM imeshinda kwa kishindo.

Katika chaguzi hizi ambazo CCM imeendelea kuongoza inajivunia umakini mzuri wa kufuata Taratibu, Kanuni na Sheria za Nchi yetu, Sera nzuri, ahadi zinazotekeleka na siasa safi na uongozi bora.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuwashukuru watanzania na wanaCCM wote kwa kuendelea kukiamini na kukichagua na kwamba CCM itaendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa haraka katika maeneo yao.

Aidha Chama kinapenda kuwafahamisha kuwa tarehe 17 hadi tarehe 18 Desemba 2018 Jijini Dar es salaam kutakuwa na vikao vya Chama vya kawaida vya Uongozi Taifa ambapo tarehe 17 Desemba 2018 kutakuwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na tarehe 18 Desemba 2018 Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kitaketi. Hivyo taarifa hii inawajulisha wajumbe wote wa vikao husika kufika katika vikao hivyo

CCM inapenda kuwafahamisha kuwa imefuatilia kwa ukaribu mjadala unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wito alioutoa Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM kwa Ndg. Benard Membe ambaye ni Mwanachama wa CCM kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Katibu Mkuu kukutana na Viongozi na Wanachama wa CCM katika kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa wanaCCM.

Tunapenda kutoa rai kwa watanzania kuwa wito wa Katibu Mkuu ulikuwa ni wito wa kawaida wa Kiongozi wa CCM kwa mwanachama wa CCM, hivyo uzushi, uchonganishi, fitina na uvumi mwingine wowote unaoendelea hasa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya Magazeti yenye hila mbaya, wana CCM na Umma wa watanzania wanaombwa waupuuze.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawataka wana CCM na watanzania kwa ujumla kuendelea kuwa na umoja, mshikamano na upendo zaidi katika kipindi hiki ambacho Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anandelea kutuongoza katika Mageuzi makubwa ya kiuchumi na ya kimaendeleo kwa watanzania wote.
1.jpeg
 
Back
Top Bottom