Yanasemwa mengi na yatasemwa mengi ila kama kuna Kosa kubwa ambalo Rais Dkt. Magufuli amelifanya ( na naamini hapa atakuwa alishauriwa vibaya na Watu wake ) ni kuweka mbali au kukaa mbali na ' Fundi wa Diplomasia ' Benard Membe na kwa maoni yangu huenda leo hii tunaona baadhi ya matatizo ya hapa na pale yanatokea hasa Kimataifa kwakuwa hana ' Mafundi ' kama akina Membe.
Hata kama huyu Mtu ( Membe ) aliamua Kuachana na Ubunge lakini Mimi kama GENTAMYCINE bado naamini kwamba Mheshimiwa Rais Magufuli kwa ' Mandate ' yake kama ' Executive ' bado alikuwa anaweza Kumtumia katika ' Baraza ' lake la Mawaziri au hata katika maeneo mengine hasa ya Kidiplomasia ambayo kwa Mimi naona kwamba hadi hivi leo bado tunafanya vibaya na mifano juu ya hili iko mingi tu.
Kwa Mtu mwenye ' exposure ' kubwa na ' iliyotukuka ' kabisa huku akiwa amewahi Kuhudumu katika moja ya Idara / Taasisi muhimu / nyeti Kiusalama katika nchi hii kama Mzee Benard Membe leo hii kumuacha awe tu hivi ' huru ' nadhani ' technically ' kabisa hapa kuna Kosa kubwa sana lilifanyika ama kwa Watu kutokujua au Mheshimiwa Rais Magufuli alilishwa ' Sumu ' za ' Kimajungu ' na Watu wake wa karibu ambao anawaamini nae ' Sumu ' ikamuingia vilivyo na matokeo yake ndiyo haya sasa.
Sehemu yoyote ile hasa kwa Watu wenye ' akili ' sawasawa pale ukishaona kuwa Mtu fulani bado ana ' Potential ' fulani katika nchi ambayo ina Tija ya Kimaendeleo basi yakupashwa uendelee Kumuamini na Kumtumia ila kama pia umeona mwenyewe kwa Vipimo vyako kuwa GENTAMYCINE ni ' Tishio ' Kwako basi njia pekee ya Kumuweza ni ' Kumjumuisha ' katika ' Utawala ' wako ili uweze Kumlevya Kimamlaka lakini pia Kumdhoofisha ' Kimbinu ' pasipo Yeye kujua lakini kumuacha awepo awepo tu ni hatari kubwa kama ambavyo tunaanza kuiona sasa.
Hata hivyo bado hatujachelewa na hasa hasa Rais Magufuli bado hajachelewa kwani Mimi GENTAMYCINE naamini tena kwa 100% kuwa Mzee Benard Membe anaweza kuwa ni ' msaada ' mkubwa mno wa Kiutawala Kwake ama kwa huu muda alioubakisha kwa muhula wale huu wa Kwanza au hata kwa muhula wake wa pili na mwisho. Asiwasikilize wale ' Wanafiki ' ambao wamemzunguka na ambao hata Yeye pia alishakiri mara nyingi tu kuwa walishawahi hadi kumwambia kuwa Katibu Mkuu wa sasa wa CCM Ndugu Bashiru Ally Kakurwa hafai lakini Yeye mwenyewe akajiridhisha nae na kuamua kufanya nae Kazi na tunaona anafanya vyema tu.
Yangu ni hayo tu ila Mzee Benard Membe bado ni ' Lulu ' kubwa katika ' Utawala ' huu asiachwe na apewe ' Majukumu '.
Nawasilisha.