Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Alichoandika Polepole ni kama vile anajibu maswali ya History O level ....LAND ALIENATION, FORCED LABOUR and MEAGRE WAGES.
Sasa hata yeye mwenyewe mbona ni Olevel leaver mkuu!!
He is in right track
 
Mbona kasi ya wito imeisha Ghafla. Maana mwanza Bashiru alisema na kuuliza kwani nyie hamumsikii Membe.. leo imekuwa ni aje kwa hiari na ni kubadilishana uzoefu na sio kuthibitisha tuhuma???
Mara nyingi huwa nikangalia Bashiru akiongea huwa namuoa kama ni mtu wa kupayuka, kuropoka na kupaniki haraka
Huwezi amini kwamba huyu ndiye yule akivutia wasikilizaji kwa weledi wake wa kujenga hoja.
downloadfile-2.jpg
 
Endelea kujidanganya polepole kawakusanye vilaza ila sio humu Mkuu wa mkoa Kilimanjaro vs wakuu wa wilaya?????tunazidi kupiga dua hata hivyo vikao mupasuke zaidi mnatutesa sana nyie 25%no increment,debe LA maindi 2000,biashara haziendi!!!napiga dua hapa
 
Chama hicho kimetoa rai kwa Watanzania kuwa wito huo ulikuwa ni wa kawaida hivyo uzushi, uchonganishi, fitina na uvumi mwingine wowote unaoendelea katika mitandao ya kijamii ina hila mbaya kwa CCM.

Nani kayaanzisha?
Aliyeanzisha hili sakata angefanya kwa siri kupitia nyaraka badala ya mitandao ya kijamii, waliopo nje wangeyajuaje?
 
Hivi hakukua na waandishi wa habari wa kumuuliza maswali Polepole?
Maanake ameongea kama vile hakumsikiliza Bashiru au ni kama vile watanzania hawakumsikia Bashiru alichoongea.
Anyway labda tulimnukuu vibaya Bashiru au kuna uwezekano Bashiru mwenyewe alijinukuu vibaya
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa msimamo wake dhidi ya vita ya maneno inayoendelea kati ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashiru Ally na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Taarifa iliyotolewa leo jioni Jumatatu Desemba 3, 2018 na Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole inaeleza kuwa kauli ya Bashiru kumtaka Membe ambaye ni mwanachama wa chama hicho kufika ofisini kwake ni ya kawaida ndani ya CCM.

“CCM inapenda kuwafahamisha kuwa imefuatilia kwa ukaribu mjadala unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wito alioutoa Bashiru kwa Membe,” inaeleza taarifa hiyo.

“Ni kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Katibu Mkuu kukutana na viongozi na wanachama wa CCM katika kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa wanachama.”

Chama hicho kimetoa rai kwa Watanzania kuwa wito huo ulikuwa ni wa kawaida hivyo uzushi, uchonganishi, fitina na uvumi mwingine wowote unaoendelea katika mitandao ya kijamii ina hila mbaya kwa CCM.

Katika taarifa hiyo Polepole amesema CCM inawataka Watanzania kuendelea kuwa na umoja, mshikamano na upendo katika kipindi hiki ambacho Rais John Magufuli anaendelea kuongoza nchi katika mageuzi ya uchumi na maendeleo.

Chama hicho pia kimeeleza ushindi wake ilioupata katika uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye Kata 47 Tanzania Bara uliofanyika Desemba 2, 2018.

Amesema CCM imepita bila kupingwa katika Kata 41 na katika Kata 6 ambako kumefanyika uchaguzi chama hicho kimeshinda kwa kishindo.

Desemba 17 na 18, 2018 jijini Dar es Salaam chama hicho kitakuwa na kikao cha kawaida cha uongozi wa Taifa.

Amefafanua kuwa Desemba 17, kitakuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa huku Desemba 18, kitafanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

Chanzo: Mwananchi
Wapinzani tumetwist plan za ccm, ccm bila polisi hawatuwezi
 
Ukichimama Nchale, Ukikaa Nchale, Ukikimbia Nchale, Ukilala Nchale
 
Ukichimama Nchale, Ukikaa Nchale, Ukikimbia Nchale, Ukilala Nchale
 
Watu hawata amini lakini nawaambia wana JF Bernard anatemeshwa uanachama! KM hakukurupuka kwa ile kauli, ile ni kauli ya kimkakati kabisa aliyotumwa kuitoa na vyombo vya kimkakati

Bernard alitakiwa atoe kauli kama ile aliyoitoa ya kujibu ili ipatikane sababu na uhalali wa kumuita iwe kwa heri au kwa shari. Inajulikana kwamba yeye hatakuja kipindi cha hivi karibuni

Kwa kufanya hivyo mchakato wa kumvua uanachama utaanza. Kitakacho tokea watajitokeza wa kumtetea kwa kupinga utaratibu utakaotakaka kumtimua Bernard kwa sababu kuthibitisha kosa lake ni vigumu

Hapo pia panasubiriwa kwa hamu kwa sababu wanatafutwa waungaji mkono wake, na wote wataopinga Bernard kuadhibiwa watachukuliwa kua ni timu Bernard na watadhibitiwa vilivyo. Udhibiti huu waweza kuhusisha vyombo kadhaa kama vile vya ukusanyaji mapato, udhibiti rushwa, vyombo vya ulinzi na usalama na hata kutumbuliwa kutoka kwenye nafasi au ajira zao

Jambo hili lina blessings za PM mstaafu ambaye siku hizi anasifiwa sana na wakuu wa chama tawala. PM mstaafu kasahau kua wafuasi wake wengi wamekua persecuted na kua victimized kwa kule tu kua waliwahi kumuunga mkono
 
Sampuli hizi ndo zinamshauri jiwe hivi nipo kwenye daladala cwez kushuka jamani
 
Back
Top Bottom