Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Chadema wako bize kumpotosha Membe kama walivyompotosha Lowasa.

Mahaba ya Chadema kwa Membe yanasitajaabisha , badala ya kumlilia Mbowe yupo gerezani wako bize kumlilia mwana ccm Membe!!!!

Wana chadema kina nani umeona wamemzungumzia membe, Acha mahaba ya kijinga utakuja kufanywa kitu kibaya na hao hao unaowaletea mahaba
 
Unatetea tumbo Sababu ya ruzuku,bila ruzuku gazeti lako huna uwezo wa kuprint hata headlines
 
membe analinyima jiwe usingizi mpaka ifike 2020 jiwe ukichaa utazidi kumpanda nakuokota makopo.
Nape, jack Gotham, na Membe wamepata wafadhili huko ulaya , Canada, Marekani , India na Uarabuni wanataka kuja kuijenga Dodoma iwe kama Dubai lakini hawataki Rais awe ni mtukufu malaika toka chato na Naibu Rais ndugu Bashite, wanataka Rais mwingine kabsa:
 
Tunapokaribia uchaguzi wa 2020 hakuna ubishi kuwa ndani ya CCM kuna makundi, kwa elewa wangu kuna kundi la Bernard Membe aliyekuwa mgombea 2015 vile vile bado kuna masalia ya kundi la Lowassa. Ingawa Magufuli naye anajitahidi kutengeneza kundi lake lkn bado changa halina nguvu ya kisiasa nguvu yake inategemea vyombo vya dola.

Wasioamini siasa za fitina ndani ya CCM hasa uchaguzi unapokaribia wamuulize, Salim Ahmed Salim, John Malecela, Mohamed Bilali, na Jakaya Kikwete.

Baada ya jina la Membe kuanza kusikika kuwania urais tayari fitina zimeanza kutengenezwa na mitandao imeanza kujengwa, hofu kubwa ya CCM ni ndani ya chama kuliko nje ya chama, inawezekana kabisa kwa mara ya kwanza rais Magufuli akapata mpinzani.

Kuna uwezekanao Lowassa akawa Waziri 2019-2020 !
Nimeota tu ndoto za Mchana
 
Tatizo ni kuwa Maghuful ndo kashikilia rungu, alafu yupo karbu na Lowasa...Mtandao wa membe ushavurugwa parefu sana...kuanzia mabalozi mpak jeshini, huwez kuwashawishi kwa lolote hawa watu kwa sababu wananufaika na utawala uliopo et zaman walikuwa company yako, hlo tu linatosha kumwangusha Membe, usishangae Membe akafutwa uanachama wa CCM kwa nguvu......!! acha kabisa haya mambo
Jana Musiba ambaye ni msemaji wa kienyeji wa CCM alipendekeza Membe akamatwe na kuporwa kadi ya CCM nadhani CCM wanaweza kutekeleza Amri ya msemaji wao wa kienyeji
 
Ni wazo tu...kwamba sio lazima Membe amkwamishe Magufuli ndani ya CCM. Muungano wa Membe, Lissu na Lowasa nje ya CCM unaweza kumuondoa Magufuli madarakani mwaka 2020. Magufuli na CCM yake wasidhani wamesimama thabiti kiasi hicho.

Na ni wazi kwamba ndani ya CCM Membe hawezi kumtikisa Magufuli.
 
Kiingerza chako cha Darasa la Tatu Shule ya Msingi umenikera sana tu.
Ha ha ha aa..!Sikujua kama na mimi wa kutoka darasa la kwanza kwenye shule za 'Mtakatifu' Kayumba ninaweza kufananishwa na wanafunzi wa darasa la tatu wa B. Primary au OB. Primary katika kumudu lugha ya malkia wa Uingereza....!! Hongera sana mwalimu wetu wa lugha hiyo hapo shuleni kwetu.
====
Blackbold: Kwa sababu uzi huu unahusiana na 'mbobezi wa diplomacy'...lugha iliyotumika hapo wanadiplomasia watakuwa wameelewa.
 
Kuna uwezekanao Lowassa akawa Waziri 2019-2020 !
Nimeota tu ndoto za Mchana
Marekani huwa inatokea na Nchi zingine kama South Africa nk huko wapo mawaziri toka upinzani, lakini Musiba msemaji wa kienyeji wa CCM atafurahia lowasa kupewa uwaziri wakati yeye hajapewa ukuu wa wilaya?
 
Wabangua korosho nao ni wahanga wa 25% pia ni sehemu ya jamii, wenzie walianzia msituni wanaexpirience kusikia milio ya baruti.Asiwaamini sana ukikosa network umekosa vyote hata uwe na jeshi imara
Yeye anaamini kuwa hali ikiwa mbaya anaweza akalituma Jeshi kwenda kuomba misaada huko nje.
Yeye haamini katika mgawanyo wa majukumu. Anadharau kazi za kichwa, anadharau kazi za unyeo, anadharau kazi za miguu, anadharau kazi za makalio. Anaamini mikono, virungu na risasi ndiyo jibu la kila kitu.
 
Tunapokaribia uchaguzi wa 2020 hakuna ubishi kuwa ndani ya CCM kuna makundi, kwa elewa wangu kuna kundi la Bernard Membe aliyekuwa mgombea 2015 vile vile bado kuna masalia ya kundi la Lowassa. Ingawa Magufuli naye anajitahidi kutengeneza kundi lake lkn bado changa halina nguvu ya kisiasa nguvu yake inategemea vyombo vya dola.

Wasioamini siasa za fitina ndani ya CCM hasa uchaguzi unapokaribia wamuulize, Salim Ahmed Salim, John Malecela, Mohamed Bilali, na Jakaya Kikwete.

Baada ya jina la Membe kuanza kusikika kuwania urais tayari fitina zimeanza kutengenezwa na mitandao imeanza kujengwa, hofu kubwa ya CCM ni ndani ya chama kuliko nje ya chama, inawezekana kabisa kwa mara ya kwanza rais Magufuli akapata mpinzani.

Rais Magufuli anajua jinsi alivyopita kwenye tundu la sindano wakati wa mchakato wa kura ya maoni, anajua fika nguvu ya Lowassa aliyokutana nayo, bila fitina za Mkapa nafikiri leo asingekuwa pale, ndiyo maana ameanza jitihada za kumuweka Lowassa karibu na himaya yake, anajua Lowassa ni kiungo muhimu kati yake na wanamtandao, ni muda tu tutaanza kuona vijana wa CCM mitandaoni na kwenye majukwaa wakimsafisha Lowassa.

Kwa upande mwingine mtandao wa Membe ni mpana, ukimtaja Membe umemtaja rais msataafu Jakaya Kikwete umemtaja Pius Msekwa, umemtaja Hawa Ghasia, umemtaja Kinana, Nape, Rostam Azizi. Membe ana marafiki wengi ndani na nje ya nchi, anao marafiki Falme za Kiarabu, Mabalozi wengi wa western countries ni washirika wake.

Membe siyo Lowassa kuwa ukimfanyia figisu kidogo tu atakubali yaishe. Kosa alilofanya Lowassa ambalo sidhani kama Membe atalifanya ni kuhama chama, najua Membe atapambana ndani ya chama kwa kutumia uzoefu wake, ujuzi wake, na diplomasia yake.

Membe hana papara ni mtu mkimya, mwana diplomasia mbobevu, mwana usalama aliyefanya kazi ya intelijensia ndani ya system kwa muda mrefu na amepanda sana vyeo ndani ya idara hiyo nyeti na hivyo anazijua siri nyingi za serikali na namna nzuri ya kufanya umafia.

Tukumbuke tu kuwa aliyemfix Lowassa hadi kuamua kuondoka CCM ni komred Membe na mtandao wake wa akina Kinana, Nape, kwa hiyo CCM ya akina Bashiru Ally ijiandae kisaikolojia, isidhani itapata mtelemko itakapokuwa ina dili na mbobezi wa fitina Mh. Bernard Membe.
Nawaza tu kwa nguvu, hivi kwa mfano Mwenyekiti akiamua kumvua uanachama Membe si ndiyo atakuwa ameshaimaliza kazi mwenyekiti?
 
Kuna mambo mengi yanaweza kudhaniwa tofauti ila ninachokiona ni kwamba sisi tumekuwa goigoi hat kwa maisha yetu wenyewe.. Uthabiti wa kufikiri umeshuka sana sio kwa wasomi hata kwa baadhi ya wanasiasa. Tumezidiwa na wananchi wasio na uwezo ambao wana majibu na suluhisho la maisha magumu wanayoyapitia hata wanaweza kupaaza sauti ikibidi. Kwa nini Membe? Membe ana suluhisho la mambo mengi yanayoikabili nchi japo ni MCCM lakini ana kiwango cha ufanisi na uelewa wa kazi ya taasisi tunayotamani aingie. Katika kipindi chake tuliona mahusiano na nchi mbalimbali yalivyoimarika na kuleta tija katika maeneo mbalimbali na hata miradi mingi awamu hii inayojivunia ni legacy iliyojengwa kupitia Membe eneo la diplomasia na Kikwete akiwa Mkuu wa nchi. Membe ana majibu ya Mafao ya wastaafu kufikia hata asilimia 80 na fao la kujitoa na mengineo. Membe ana majibu ya Ajira maana walijega mifumo rafiki ya uwekezaji wa nje na ndani na mazingira rafiki kwa wageni waliopenda kuwekeza Tanzania ambapo ndiko chimbuko kubwa la ajira.
Membe ana majibu ya bei za mazao ya wakulima maana walijenga mahusiano mazuri ya kibiashara na mataifa mbalimbali ambapo ilimsaidia mkulima kuona thamani ya mazao yake,
Membe na team ikwete waliweza kuwezesha maboresho ya sera za afya, Kilimo, Elimu na kuwezesha misaada na uwekezaji mkubwa katika eneo la afya na elimu za afya,
Membe ana majibu ya nyongeza za mishahara kwa watumishi wa serikali na wa taasisi binafsi
Membe anajua umuhimu wa sekta binafsi maana walijitahidi sana hata kusadia guarantee schemes kwa wajasiriamali wa ndani kununua bidhaa mbalimbali nje.
Membe ana majibu ya Mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama sa maisha ikiwemo vifaa va ujenzi maana kipindi chao ndio kiliwezesha uwekezaji mkubwa katika vifaa vya ujenzi akiwemo Dangote.
Membe ana majibu yauhuru wa makama, vyama vya siasa, elimu bora, uhuru wa Diaspora, utawala bora, uwajibikaji, umoja wa kitaifa na fursa kwa wote.
Membe ana majibu ya sera endelevu za uwekezaji na ushirikiano wa kimataifa
Membe ana busara na mwenye haiba ya huruma na kujali wananch wake bila kuwabeza
Membe anatufaa....
 
Ndg wana jf.kuna mvumo mkubwa ktk media nyingi kuhusu mh membe na ccm,leo membe akiamua kuihama ccm atatoka na kundi kubwa kuliko lowassa?
 
Back
Top Bottom