Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Kitu wanacho sahau ni kwamba, aliye muita Membe alitaja na sababu za kumwita kwamba ana muhujumu Rais Magufuli, saiz imekua mara umoja na mshikamano, mara korosho, yani full kujikanyaga
kJZWYia.gif

Fulu kujikanyaga hhahahaaaaaa!!!!!
 
Kitu wanacho sahau ni kwamba, aliye muita Membe alitaja na sababu za kumwita kwamba ana muhujumu Rais Magufuli, saiz imekua mara umoja na mshikamano, mara korosho, yani full kujikanyaga
Hivi polepole anataka kumdanganya nani ?
 
Watumishi fanyeni hujuma indirect dhidi ya serikali hii onevu kwenu ni miaka 3 hakuna ongezeko la mishahara na maslahi yenu inazidi kandamizwa.
 
KAULI MBIU YA 2020 NI KAZI NA BATA. NYIE SI MLIIPATA MKIWA MMEBAKISHA SIKU 5 TUINGIE KWENYE UCHAGUZI...SASA MTAJUTA...LAZIMA MPIGE KAZI NA MLE BATA.

Membe
cc Zitto
cc Aikael
 
CCM wana matatizo sana, ila tatizo moja kuu ni kwamba "Wanachama wao sio wakweli na wawazi", hasa wabunge. Pili hawana mtazamo wa mbali (Miaka 20 au 30 ijayo, japo wanahisi wanao mtazamo huo ila si kweli).

Wangekua ni wakweli na wawazi toka moyoni, kila mmoja angepaza sauti kutokana na mtazamo wake kuhusiana na viongozi wao na chama kinapoelekea. Na wasingepitia hizi AMBUSH WANAZOPATA kutoka kwa VYAMA PINZANI (Japo wanajidanganya hayatakua na madhara baadae, ila ndio yatakipasua zaidi chama kwa kuondoa umoja baina yao).

Mfano mzuri,

Chama cha Rais Jacob Zuma, aliekua rais wa South Africa 2009 - 14th February 2018, ANC (African National Congress) hawa jamaa wanamsimamo wa dhati, na wanaona/wana malengo ya mbali sana, si dhani kama kuna "CHAMA CHA SIASA" Africa nzima au Marekani kinafikia hata ROBO ya demokrasia au mtazamo walionayo.

Wawakilishi wao wote bungeni ni wawazi, na hawaendekezi unafiki. Pindi walipokua wakiona WAZIRI/KIONGOZI FULANI anakichafua chama kwa maamuzi ya ajabu, walikua wanamwambia RAIS amtengue haraka sana uwaziri na ateue mtu mwingine. Na Rais alitii maombi ya kamati kuu ya chama ANC (Kuna mawaziri walimwagwa kadhaa).

CCM wabunge hawana sauti hii. Tumeshuhudia mawaziri/ma DC kadhaa, wakitoa TWEETS/MAAGIZO za kebehi kwa raia (wapiga kura wao) ila hakuna maamuzi yoyote yaliofanyika.

Pili, ANC walipoona kashfa (zenye ushahidi na mashiko) zimemuelemea Rais (Ambaye wao ndio walimchagua kuwania kiti hicho cha Urais na kumsaidia kufanya campaign mpaka akashinda) walikaa kamati na kujadiliana swala hilo.

Maafikiano waliofikia, ni wampe siku Rais Jacob Zuma aandike barua ya kujiuzulu urais au wakambwage bungeni wao wenyewe kama atagoma kujiuzulu.

Nini mantiki ya maamuzi haya ya chama ANC,

Walitambua kua itawadia ugumu kumsafisha kwa wapiga kura, na itakuja kuwasababishia kupoteza wapiga kura wao waliowachagua (CREDIBILITY OF POLITICAL PARTY).

1) Ingewezekana wamuache aendelee mpaka amalize mhula wake wa uongozi, ila walikua hawapo tayari amalize muda kisha waanze kumsafisha kwa wapiga kura kwenye kampeni. Muda ungekua umeshakwenda.

Kitendo cha kumbadilisha kabla ya kumaliza kwake muda wa uongozi, imekua ni "kampeni" tosha kwa wapiga kura, wapinzani wamejikuta hawana sehem ya kuwajeruhi (Tactical Pyschological Campaign:- kampeni ya kisaikolojia kwa raia wa South Africa, kabla ya kampeni rasmi ya uchaguzi mkuu).

2) Wamedhihirisha wana demokrasia madhubuti, sambamba na mifano kama ya nchi BRAZIL & INDIA.

3) Chama cha ANC kimepata nguvu zaidi, badala ya fikra za "watu wasiokua na uelewa" kufikiria kwamba ni AIBU na CHAMA KITATETEREKA. Raia wameongeza IMANI kwenye chama ya kwamba kina msimamo na si chama cha watu wachache (Baada ya kuonesha UWAJIBISHWAJI wa viongozi wa juu).

4) ANC walikua wana uwezo wa kuingia MKATABA na Rais Jacob Zuma, sambamba na vyama vya upinzani, kua "Mh Rais akijiuzulu KINGA yake na FAMILIA yake ""ISISHTAKIWE MAHAKAMANI"" (Kama ilivyokua kwa Mh Rais Robert Mugabe).

***Kwanini hawakuweka makubaliano hayo? Na baada tu ya kuachia ngazi ya Urais Jacob Zuma akafunguliwa CASE YA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA & RUSHWA?

***Pamoja na mwanaye wa kiume (Kipenzi Chake) Duduzane Jacob Zuma, alipofika Airport tu alikamatwa kisha kufunguliwa case ya Uhujumu Uchumi, Matumizi mabaya ya madaraka, na Rushwa???

Majibu yanarudi pale pale "TACTICAL PYSCHOLOGICAL CAMPAING FOR A LONG TERM RUN".

5) Walifanya hivi kuepusha "MACHAFUKO" kwenye uchaguzi ujao, kuhofia Raia wasije wakawafanyia fujo na kuvunjika kwa amani ya nchi yao (kama tulivyoahuhudia baadhi ya raia wasio na ajira kuvunja maduka ya watu S.A kipindi cha nyuma).

Nawasilisha imani yangu,
Povu ruksa, ukitaka hata kunitukana poa tu.
 
Chama ni watu na watu ndiyo chama. Viongozi bila watu si chama na watu bila viongozi si chama pia
Mitafaruku ndani ya chama ni jambo la kawaida, lakini muhimu no jinsi ya kuishughulikia mitafaruku hiyo.
Imewahi kutokea 1995 baina ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM wakati huo marehemu Laurence Gama na Capt.. Jakaya Mrisho kikwete Naibu Waziri wa fedha wakati huo
Jakaya Mrisho Kikwete alimtuhumu hadharani Katibu Mkuu Laurence Gama kuwa anampendelea mgombea mmoja wapo.
Mwinyi M/kiti was was CCM wakati aliwaita akawasuluhisha faragha. Hatukusikia tena mtafaruku
Yuko wapi leo wa kuwasuluhisha wana CCM? Yuko wapi mwenye mabavu ya ubongo dhaifu wa mabavu. Ni nani was kupunguza kuni wakati wana CCM wanachochea moto wa mitafaruku
Tumpate wapi jasiri wakati wote wanajificha ufunguni Simba wa mitafaruku anakinyemelea CCM
Au ndiyo upinzani was kweli alio usema marehemu baba was Taiga Mwl. Julius Kambarage Nyerere
Wako wapi waliowasuluhisha Arap Moi na Oginga Kule Kenya
 
Mbowe kuwa ndani ni triki ya kiwango cha juu sana , ni mchongo mmoja makini sana ambao wachumia tumbo hawatoelewa milele.
Kwahiyo kajipeleka?

Mkuu muwe mnaweka mikakati maalumu ya kukinyanyua chama na hatimaye kushika dola, lkn si hizi mbwembwe zenu za kumsifia Membe
 
Polepole aise, lkn ndiyo kusema umoja na mshikamano ndani ya CCM utaisha iwapo kada mwingine ataonesha msimamo wa kugombea nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya ccm? - ni kweli kuwa Katibu Mkuu kumtuhumu mwanachama jukwaani kabla hajaongea naye privately kwamba ni utaratibu wa kawaida ktk chama?

CCM - Tujitahidi kuchaguwa maneno kabla ya kuzungumza,
CCM - Tujitahidi kupitia hotuba (rehearsal) kabla ya kuhutubia umma,
CCM - Tujitahidi kuondoa na kujiepusha na makundi, na
CCM - Tujitahidi kuitii katiba yetu wenyewe (mtu akioneha nia ya kugombea si dhambi wala uhaini)
 
Back
Top Bottom