Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa msimamo wake dhidi ya vita ya maneno inayoendelea kati ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashiru Ally na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Taarifa iliyotolewa leo jioni Jumatatu Desemba 3, 2018 na Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole inaeleza kuwa kauli ya Bashiru kumtaka Membe ambaye ni mwanachama wa chama hicho kufika ofisini kwake ni ya kawaida ndani ya CCM.

“CCM inapenda kuwafahamisha kuwa imefuatilia kwa ukaribu mjadala unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wito alioutoa Bashiru kwa Membe,” inaeleza taarifa hiyo.

“Ni kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Katibu Mkuu kukutana na viongozi na wanachama wa CCM katika kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa wanachama.”

Chama hicho kimetoa rai kwa Watanzania kuwa wito huo ulikuwa ni wa kawaida hivyo uzushi, uchonganishi, fitina na uvumi mwingine wowote unaoendelea katika mitandao ya kijamii ina hila mbaya kwa CCM.

Katika taarifa hiyo Polepole amesema CCM inawataka Watanzania kuendelea kuwa na umoja, mshikamano na upendo katika kipindi hiki ambacho Rais John Magufuli anaendelea kuongoza nchi katika mageuzi ya uchumi na maendeleo.

Chama hicho pia kimeeleza ushindi wake ilioupata katika uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye Kata 47 Tanzania Bara uliofanyika Desemba 2, 2018.

Amesema CCM imepita bila kupingwa katika Kata 41 na katika Kata 6 ambako kumefanyika uchaguzi chama hicho kimeshinda kwa kishindo.

Desemba 17 na 18, 2018 jijini Dar es Salaam chama hicho kitakuwa na kikao cha kawaida cha uongozi wa Taifa.

Amefafanua kuwa Desemba 17, kitakuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa huku Desemba 18, kitafanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

Chanzo: Mwananchi
Hongera sana ccm kupita bila kupingwa kwani Tume wewe, msimamizi wa uchaguzi wewe utashindwaje?
 
Yanasemwa mengi na yatasemwa mengi ila kama kuna Kosa kubwa ambalo Rais Dkt. Magufuli amelifanya ( na naamini hapa atakuwa alishauriwa vibaya na Watu wake ) ni kuweka mbali au kukaa mbali na ' Fundi wa Diplomasia ' Benard Membe na kwa maoni yangu huenda leo hii tunaona baadhi ya matatizo ya hapa na pale yanatokea hasa Kimataifa kwakuwa hana ' Mafundi ' kama akina Membe.

Hata kama huyu Mtu ( Membe ) aliamua Kuachana na Ubunge lakini Mimi kama GENTAMYCINE bado naamini kwamba Mheshimiwa Rais Magufuli kwa ' Mandate ' yake kama ' Executive ' bado alikuwa anaweza Kumtumia katika ' Baraza ' lake la Mawaziri au hata katika maeneo mengine hasa ya Kidiplomasia ambayo kwa Mimi naona kwamba hadi hivi leo bado tunafanya vibaya na mifano juu ya hili iko mingi tu.

Kwa Mtu mwenye ' exposure ' kubwa na ' iliyotukuka ' kabisa huku akiwa amewahi Kuhudumu katika moja ya Idara / Taasisi muhimu / nyeti Kiusalama katika nchi hii kama Mzee Benard Membe leo hii kumuacha awe tu hivi ' huru ' nadhani ' technically ' kabisa hapa kuna Kosa kubwa sana lilifanyika ama kwa Watu kutokujua au Mheshimiwa Rais Magufuli alilishwa ' Sumu ' za ' Kimajungu ' na Watu wake wa karibu ambao anawaamini nae ' Sumu ' ikamuingia vilivyo na matokeo yake ndiyo haya sasa.

Sehemu yoyote ile hasa kwa Watu wenye ' akili ' sawasawa pale ukishaona kuwa Mtu fulani bado ana ' Potential ' fulani katika nchi ambayo ina Tija ya Kimaendeleo basi yakupashwa uendelee Kumuamini na Kumtumia ila kama pia umeona mwenyewe kwa Vipimo vyako kuwa GENTAMYCINE ni ' Tishio ' Kwako basi njia pekee ya Kumuweza ni ' Kumjumuisha ' katika ' Utawala ' wako ili uweze Kumlevya Kimamlaka lakini pia Kumdhoofisha ' Kimbinu ' pasipo Yeye kujua lakini kumuacha awepo awepo tu ni hatari kubwa kama ambavyo tunaanza kuiona sasa.

Hata hivyo bado hatujachelewa na hasa hasa Rais Magufuli bado hajachelewa kwani Mimi GENTAMYCINE naamini tena kwa 100% kuwa Mzee Benard Membe anaweza kuwa ni ' msaada ' mkubwa mno wa Kiutawala Kwake ama kwa huu muda alioubakisha kwa muhula wale huu wa Kwanza au hata kwa muhula wake wa pili na mwisho. Asiwasikilize wale ' Wanafiki ' ambao wamemzunguka na ambao hata Yeye pia alishakiri mara nyingi tu kuwa walishawahi hadi kumwambia kuwa Katibu Mkuu wa sasa wa CCM Ndugu Bashiru Ally Kakurwa hafai lakini Yeye mwenyewe akajiridhisha nae na kuamua kufanya nae Kazi na tunaona anafanya vyema tu.

Yangu ni hayo tu ila Mzee Benard Membe bado ni ' Lulu ' kubwa katika ' Utawala ' huu asiachwe na apewe ' Majukumu '.

Nawasilisha.
Umeandika uozo, kakojoe ulale. Popoma mkubwa wewe
 
Naunga mkono mdau. Huyu ndiye mlimutaka mwaka 2015. Angewaua kwanza wale maadui zake 11, ndipo aanze upya kwa maadui wengine waliojitokeza tangu atoe tamko hilo mwaka 2012.

Bernard Membe: Nina maadui 11, ikifika 2016 watakimbilia Kenya! - JamiiForums
 
Rais Dk. John Pombe Magufuli, hana kinyongo chochote na Viongozi wenzake ndani ya CCM na ndani ya Serikali na ndani ya Dola lakini wao wanamhujumu kwa nia zao mbaya. Wengi walipewa nafasi huko nyuma walishindwa ku-deliver, amekuja mwenzao wanaanza kumuonea wivu.

Magufuli pitia hiki Kitabu cha The Prince cha Karne ya 16 kutoka kwa gwiji la Kitaliano, Niccolo Machiavelli, upate ushauri namna ya ku-deal na adversaries wako.

Machiavelli's The Prince
hatufai kabisa huyu dubuwasha, MEMBE 2020
 
Membe nadhani alikua anabebwa tu na familia ya first citizen wa wakati huo, sasa hivi anaonekana kama ana nguvu kidogo kwasababu jamaa aliyepo ameboa mambo mengi but otherwise Lowassa alikua hakuna wa kupambana nae kule endapo wangeruhusu KURA au demokrasia kuchukua mkondo wake
 
"Rais ni mtu wa kushutumiwa kila mara. Ukiona hataki kushutumiwa, ujue hajui sababu ya kuwa hapo."- Harry_Truman.
 
Endeleen kuimba na kuyakata mauno wenyewe
 
"Rais ni mtu wa kushutumiwa kila mara. Ukiona hataki kushutumiwa, ujue hajui sababu ya kuwa hapo."- Harry_Truman.
Ukiona mtu anakushutumu bila kushauri njia bora ujue huyo anaumia sana ukifanikiwa na ukishamjua basi hautakiwi tena kuchukua ushauri wake kwani hautatoka moyoni.
 
Ni wazo tu...kwamba sio lazima Membe amkwamishe Magufuli ndani ya CCM. Muungano wa Membe, Lissu na Lowasa nje ya CCM unaweza kumuondoa Magufuli madarakani mwaka 2020. Magufuli na CCM yake wasidhani wamesimama thabiti kiasi hicho.

Na ni wazi kwamba ndani ya CCM Membe hawezi kumtikisa Magufuli.
Tatizo sio kumng'oa ishu iko hapo kwenye tume maana wana uwezo wa kupindua kama alivyofanya jecha kule zanzibar
 
kama ni hewa basi katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa kuachia nafasi yake, haiwezekani atutoe kwenye reli kwa siku zote hizi!
 
Rais Magufuli ni mtu wa watu na hana wa kulinganishwa kamwe hapa nchini kwa kizazi chote cha Post-Sokoine. Amepeleka umeme hadi Chiponda ambako ndiko nyumbani kwao Bernard Membe.

View attachment 955577
Waziri wa Nishati Kalemani, akizindua kuwashwa kwa umeme katika Kijiji cha Chiponda, mkoani Lindi. Hizo ni juhudi za Rais Magufuli na slogan yake ya maendeleo hayana vyama. Anawaaibisha wenye roho za kwa nini?

Cha ajabu, naona Membe badala ya kufurahia huduma, mawazo yake yako mbingu ya tano. Anafikiria jinsi anavyoaibishwa kuletewa umeme na mwenzake wakati yeye alishindwa miaka 15 akiwa Mbunge na Waziri.
Una maanisha huo umeme ni hisani au wamepewa bure ?
 
Yani hata na kikwete angeungana nao na mkapa na kinana kumuangush Magu hio ni ndoto ambayo haitatimia kabisa jamaa anapiga 10yrs anakabidhi kijiti kwa huyo anaefata sijui nani
 
Umedanganywa kizembe sana ! Magufuli hana nguvu yoyote ndani ya ccm na wala hajawahi kuwa nayo , muda utaongea .
Mm ninachofurahia ni jinsi mnavyocheza ngoma inayopigwa na ccm huku mwenyekiti wenu akiwa ndani.

Chadema mna vichwa vigumu sana sana!

Sasa kwa akili yenu mnaona kabisa pale Membe yupo kumtoa Magu 2020?
 
Ukiona mtu anakushutumu bila kushauri njia bora ujue huyo anaumia sana ukifanikiwa na ukishamjua basi hautakiwi tena kuchukua ushauri wake kwani hautatoka moyoni.
"Ni afadhali kuwa na jeshi la kondoo linaloongozwa na Simba, kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo."- Napoleon_Bonaparte.

Hebu na wewe kapitie hizi quotes huenda zitakusaidia kuondokana na huo upumbavu uliorithi kutoka kwa wazazi wako. zimo humu zimeletwa na Great thinker mmoja hivi!
 
Ni wazo tu...kwamba sio lazima Membe amkwamishe Magufuli ndani ya CCM. Muungano wa Membe, Lissu na Lowasa nje ya CCM unaweza kumuondoa Magufuli madarakani mwaka 2020. Magufuli na CCM yake wasidhani wamesimama thabiti kiasi hicho.

Na ni wazi kwamba ndani ya CCM Membe hawezi kumtikisa Magufuli.
Endelea kujidanganya kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, IGP na RPCs ni Wateule wa Membe, Lissu na Lowasa.
 
Back
Top Bottom