Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

Tatizo ni kuwa Maghuful ndo kashikilia rungu, alafu yupo karbu na Lowasa...Mtandao wa membe ushavurugwa parefu sana...kuanzia mabalozi mpak jeshini, huwez kuwashawishi kwa lolote hawa watu kwa sababu wananufaika na utawala uliopo et zaman walikuwa company yako, hlo tu linatosha kumwangusha Membe, usishangae Membe akafutwa uanachama wa CCM kwa nguvu......!! acha kabisa haya mambo
 
Yanasemwa mengi na yatasemwa mengi ila kama kuna Kosa kubwa ambalo Rais Dkt. Magufuli amelifanya ( na naamini hapa atakuwa alishauriwa vibaya na Watu wake ) ni kuweka mbali au kukaa mbali na ' Fundi wa Diplomasia ' Benard Membe na kwa maoni yangu huenda leo hii tunaona baadhi ya matatizo ya hapa na pale yanatokea hasa Kimataifa kwakuwa hana ' Mafundi ' kama akina Membe.

Hata kama huyu Mtu ( Membe ) aliamua Kuachana na Ubunge lakini Mimi kama GENTAMYCINE bado naamini kwamba Mheshimiwa Rais Magufuli kwa ' Mandate ' yake kama ' Executive ' bado alikuwa anaweza Kumtumia katika ' Baraza ' lake la Mawaziri au hata katika maeneo mengine hasa ya Kidiplomasia ambayo kwa Mimi naona kwamba hadi hivi leo bado tunafanya vibaya na mifano juu ya hili iko mingi tu.

Kwa Mtu mwenye ' exposure ' kubwa na ' iliyotukuka ' kabisa huku akiwa amewahi Kuhudumu katika moja ya Idara / Taasisi muhimu / nyeti Kiusalama katika nchi hii kama Mzee Benard Membe leo hii kumuacha awe tu hivi ' huru ' nadhani ' technically ' kabisa hapa kuna Kosa kubwa sana lilifanyika ama kwa Watu kutokujua au Mheshimiwa Rais Magufuli alilishwa ' Sumu ' za ' Kimajungu ' na Watu wake wa karibu ambao anawaamini nae ' Sumu ' ikamuingia vilivyo na matokeo yake ndiyo haya sasa.

Sehemu yoyote ile hasa kwa Watu wenye ' akili ' sawasawa pale ukishaona kuwa Mtu fulani bado ana ' Potential ' fulani katika nchi ambayo ina Tija ya Kimaendeleo basi yakupashwa uendelee Kumuamini na Kumtumia ila kama pia umeona mwenyewe kwa Vipimo vyako kuwa GENTAMYCINE ni ' Tishio ' Kwako basi njia pekee ya Kumuweza ni ' Kumjumuisha ' katika ' Utawala ' wako ili uweze Kumlevya Kimamlaka lakini pia Kumdhoofisha ' Kimbinu ' pasipo Yeye kujua lakini kumuacha awepo awepo tu ni hatari kubwa kama ambavyo tunaanza kuiona sasa.

Hata hivyo bado hatujachelewa na hasa hasa Rais Magufuli bado hajachelewa kwani Mimi GENTAMYCINE naamini tena kwa 100% kuwa Mzee Benard Membe anaweza kuwa ni ' msaada ' mkubwa mno wa Kiutawala Kwake ama kwa huu muda alioubakisha kwa muhula wale huu wa Kwanza au hata kwa muhula wake wa pili na mwisho. Asiwasikilize wale ' Wanafiki ' ambao wamemzunguka na ambao hata Yeye pia alishakiri mara nyingi tu kuwa walishawahi hadi kumwambia kuwa Katibu Mkuu wa sasa wa CCM Ndugu Bashiru Ally Kakurwa hafai lakini Yeye mwenyewe akajiridhisha nae na kuamua kufanya nae Kazi na tunaona anafanya vyema tu.

Yangu ni hayo tu ila Mzee Benard Membe bado ni ' Lulu ' kubwa katika ' Utawala ' huu asiachwe na apewe ' Majukumu '.

Nawasilisha.
Rais hajafanya kosa kubwa kama unavyotaka kuaminisha umma kwa kumuacha Mh Membe kwenye safu za uongozi.
 
Yeyote atakayekwamisha juhudi za rahisi Magufuli either kwa kutumwa au kwa kujituma. Ataozea jela.
 
Rais Magufuli ni mtu wa watu na hana wa kulinganishwa kamwe hapa nchini kwa kizazi chote cha Post-Sokoine. Amepeleka umeme hadi Chiponda ambako ndiko nyumbani kwao Bernard Membe.

View attachment 955577
Waziri wa Nishati Kalemani, akizindua kuwashwa kwa umeme katika Kijiji cha Chiponda, mkoani Lindi. Hizo ni juhudi za Rais Magufuli na slogan yake ya maendeleo hayana vyama. Anawaaibisha wenye roho za kwa nini?

Cha ajabu, naona Membe badala ya kufurahia huduma, mawazo yake yako mbingu ya tano. Anafikiria jinsi anavyoaibishwa kuletewa umeme na mwenzake wakati yeye alishindwa miaka 15 akiwa Mbunge na Waziri.
Hahahaa...... Membe siyo Bulembo utakoma kuvamiavamia.......unaye huyo wenyewe wakongwe wanamwita la mdimu!
 
Tunapokaribia uchaguzi wa 2020 hakuna ubishi kuwa ndani ya CCM kuna makundi, kwa elewa wangu kuna kundi la Bernard Membe aliyekuwa mgombea 2015 vile vile bado kuna masalia ya kundi la Lowassa. Ingawa Magufuli naye anajitahidi kutengeneza kundi lake lkn bado changa halina nguvu ya kisiasa nguvu yake inategemea vyombo vya dola.

Wasioamini siasa za fitina ndani ya CCM hasa uchaguzi unapokaribia wamuulize, Salim Ahmed Salim, John Malecela, Mohamed Bilali, na Jakaya Kikwete.

Baada ya jina la Membe kuanza kusikika kuwania urais tayari fitina zimeanza kutengenezwa na mitandao imeanza kujengwa, hofu kubwa ya CCM ni ndani ya chama kuliko nje ya chama, inawezekana kabisa kwa mara ya kwanza rais Magufuli akapata mpinzani.

Rais Magufuli anajua jinsi alivyopita kwenye tundu la sindano kwenye mchakato wa kura ya maoni, anajua fika nguvu ya Lowassa aliyokutana nayo, bila fitina za Mkapa nafikiri leo asingekuwa pale, ndiyo maana anafanya kila awezalo kumuweka Lowassa karibu na himaya yake, anajua Lowassa ni kiungo muhimu kati yake na wanamtandao, ni muda tu tutaanza kuona vijana wa CCM mitandaoni na kwenye majukwaa wakimsafisha Lowassa.

Kwa upande mwingine mtandao wa Membe ni mpana, ukimtaja Membe umemtaja rais msataafu Jakaya Kikwete umemtaja Pius Msekwa, umemtaja Hawa Ghasia, umemtaja Kinana, Nape, Rostam Azizi. Ana marafiki wengi ndani na nje ya nchi, anao marafiki Falme za Kiarabu, Mabalozi wengi wa western countries ni washirika wake.

Membe siyo Lowassa kuwa ukimfanyia figisu kidogo tu atakubali yaishe. Kosa alilofanya Lowassa ambalo sidhani kama Membe atalifanya ni kuhama chama, najua Membe atapambana ndani ya chama kwa kutumia uzoefu wake, ujuzi wake, na diplomasia yake.

Membe ni mwana usalama aliyefanya kazi ya intelijensia ndani ya system kwa muda mrefu na amepanda sana vyeo ndani ya idara hiyo nyeti na hivyo anazijua siri nyingi za serikali na namna nzuri ya kufanya umafia.

Tukumbuke tu kuwa aliyemfix Lowassa hadi kuamua kuondoka CCM ni komred Membe na mtandao wake wa akina Kinana, Nape, kwa hiyo CCM ya akina Bashiru Ally ijiandae kisaikolojia, isidhani itapata mtelemko itakapokuwa ina dili na mbobezi wa fitina Mh. Bernard Membe.
2020 CCM twende na MEMBE
 
Mwenyekiti wa CCM akumbuke wazi kwamba Kikwete aliingia KK na HK na majina yake mfukoni. Wajumbe wakamshinda.

Wale unaocheka nao sasa kesho wataanza kuimba Membe! Membe! MEMBE! usije ukabaki na butwaa.

Mimi ninakushauri mkuu wetu. Huenda hawa watu wakawa mapesa mengi au wakasaidiwa kwa mapesa mengi kutoka nje, Si unawajua CIA jinsi wanavyowapachika watu wanaowataka kuwa marais?

Hakikisha mpaka mwaka 2020 wote tunakuwa na pesa mifukoni. Kama si hivyo kuna haja ya kujiandaa kisakolojia kwamba upepo wa siasa unaweza kuwa mgumu kwetu. Wameanza mapema hawa!
 
Rais Magufuli ni mtu wa watu na hana wa kulinganishwa kamwe hapa nchini kwa kizazi chote cha Post-Sokoine. Amepeleka umeme hadi Chiponda ambako ndiko nyumbani kwao Bernard Membe.

View attachment 955577
Waziri wa Nishati Kalemani, akizindua kuwashwa kwa umeme katika Kijiji cha Chiponda, mkoani Lindi. Hizo ni juhudi za Rais Magufuli na slogan yake ya maendeleo hayana vyama. Anawaaibisha wenye roho za kwa nini?

Cha ajabu, naona Membe badala ya kufurahia huduma, mawazo yake yako mbingu ya tano. Anafikiria jinsi anavyoaibishwa kuletewa umeme na mwenzake wakati yeye alishindwa miaka 15 akiwa Mbunge na Waziri.
One of the very hopeless post ever made by you. Kwan rais anapopeleka umeme chiponda anampelekea membe?

Kwan watanzania ni wale tu walio maswahiba wa jpm? Na kwa ushauri huu eti membe alishindwa kupeleka umeme hivi miradi ya rea ilianza kipindi gani vile? Magu alichofanya ni kukamilisha tuu. Kwan umeme wa rea ulikuwa unaenda kwa awamu. Na unategemea zaidi michango ya walaji wala sio hisani. Hivyo pato linapopatikana huelekezwa sehemu iliyokusudiwa hadi nchi nzima umeme uenee
 
Tatizo ni kuwa Maghuful ndo kashikilia rungu, alafu yupo karbu na Lowasa...Mtandao wa membe ushavurugwa parefu sana...kuanzia mabalozi mpak jeshini, huwez kuwashawishi kwa lolote hawa watu kwa sababu wananufaika na utawala uliopo et zaman walikuwa company yako, hlo tu linatosha kumwangusha Membe, usishangae Membe akafutwa uanachama wa CCM kwa nguvu......!! acha kabisa haya mambo
Ndugu Magu ata akigombea na halima Mdee kama uchaguzi ni huru anapigwa kweupe, Magu alibugi kutengeneza Maadui nje na ndani ya CCM
 
CCM aliyoongoza Kikwete au Mkapa ilikuwa na watu makini wakiunda kundi wanunda kweli,

Mwenyekiti aliiogopa CCM yenye meno

Tusidanganyane na kufarijiana, hakuna mwenye Ubavu wa kumuyumbisha Magufuli , ambaye kaifanya CCM kibogoyo kama taasisi nyingine mfano Bunge,

Tuwe wakweli kwamba hofu aliyowajaza wanachama wa CCM hakuna hata kwenye uthubutu wa kuandaa mpango wa kumtoa kabla ya 2025 pia usishangae kwa CCM anayoiongoza anawapangia mpaka mgombea mwaka 2025-2035

CC Pascal Mayalla

Britannica
NENO
 
Tatizo unawaza slowslow kama mwendo wa konokono

Nilichomuelewa Genta kama Membe angekuwepo kwenye wadhifa wowote hata ya ubalozi UN huenda huu upinzani na challenge kuelekea uchaguzi 2020 Mh Rais asingeupata na pia angempatia wadhifa angeua ego ya huyu membe ambaye ana timu kubwa tu huko ccm tiss kugombea urais na pia angeweza kuuliwa kisiasa kama muhongo na nchemba alivyofanywa

Fikiria mbali ndugu
Bado niko palepale, kuna watu wakuwapa ubalozi na kuna watu sio wa kupewa cheo chochote. Unafikir jpm alishindwa hata kumpa ukuu wa chuo chochote?Kuna vyeo vingap huko Serikalini jpm anagawa?Ukiona jpm kuna watu kawatupa pembeni jua anamaana yake na anataarifa nyingi kuhusu hao watu
 
KUNAWATU MNAOTA DONTO SANA ZA MCHANA...HII KITU INAYOENDELEA NI MKAKATI TU..HIVI KWANINI LICHA YA KULA PESA ZA GADAFI NAKIWANDA HAKIKUJENGWA LAKINI HAWAJAMFUATILIA???

Mwenyekiti wa CCM akumbuke wazi kwamba Kikwete aliingia KK na HK na majina yake mfukoni. Wajumbe wakamshinda.

Wale unaocheka nao sasa kesho wataanza kuimba Membe! Membe! MEMBE! usije ukabaki na butwaa.

Mimi ninakushauri mkuu wetu. Huenda hawa watu wakawa mapesa mengi au wakasaidiwa kwa mapesa mengi kutoka nje, Si unawajua CIA jinsi wanavyowapachika watu wanaowataka kuwa marais?

Hakikisha mpaka mwaka 2020 wote tunakuwa na pesa mifukoni. Kama si hivyo kuna haja ya kujiandaa kisakolojia kwamba upepo wa siasa unaweza kuwa mgumu kwetu. Wameanza mapema hawa!
 
Linjemba limechacha na ni lifukara la pesa mpaka hekima na busara
Membe fyeeekelea mbali tu
 
Narudia yeyote atakayekwambisha jihudi za Magufuli, iwe kwa kutumwa au bahati mbaya. Ataozea jela.
 
bora kiundwe chama kingine cha upinzani maana naona chadema imekwishaa kabisaa chaliii
 
Hili jambo hata mimi mpaka sasa najiuliza na mpaka leo sijapata jibu.

Nilichunguza sikuona hizo tweet bali niliona akaunti tofauti tofauti kwa jina la Bernard Membe na zote zikiwa na post za miaka ya nyuma.

Je,hili jambo ni hewa kwa malengo maalumu?
 
Mkuu unatapa tapa mpaka wenzio tunashindwa kuelewa direction yako. ...tulia tuangalie hii ngoma inachezwaje mana membe sio wa kuletewa dharau zile
 
CCM aliyoongoza Kikwete au Mkapa ilikuwa na watu makini wakiunda kundi wanunda kweli,

Mwenyekiti aliiogopa CCM yenye meno

Tusidanganyane na kufarijiana, hakuna mwenye Ubavu wa kumuyumbisha Magufuli , ambaye kaifanya CCM kibogoyo kama taasisi nyingine mfano Bunge,

Tuwe wakweli kwamba hofu aliyowajaza wanachama wa CCM hakuna hata kwenye uthubutu wa kuandaa mpango wa kumtoa kabla ya 2025 pia usishangae kwa CCM anayoiongoza anawapangia mpaka mgombea mwaka 2025-2035

CC Pascal Mayalla

Britannica
Umedanganywa kizembe sana ! Magufuli hana nguvu yoyote ndani ya ccm na wala hajawahi kuwa nayo , muda utaongea .
 
Rostam Aziz kamtema membe kama hot potato
Wahindi huwa wanaangalia nyota ya mtu siyo nyinyi manunguembe ya chadrama mcharuko mizee ya kukurupuka na kucheza singeli ya kila mtu anaye wapa pesa uwiii
Ufukara utawauwa chadrama mcharuko
 
Tatizo ni kuwa Maghuful ndo kashikilia rungu, alafu yupo karbu na Lowasa...Mtandao wa membe ushavurugwa parefu sana...kuanzia mabalozi mpak jeshini, huwez kuwashawishi kwa lolote hawa watu kwa sababu wananufaika na utawala uliopo et zaman walikuwa company yako, hlo tu linatosha kumwangusha Membe, usishangae Membe akafutwa uanachama wa CCM kwa nguvu......!! acha kabisa haya mambo
Word
 
Back
Top Bottom