nkongu ndasu
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 22,532
- 6,628
vipi upolis? vipi uganga na vipi jeshi?Ndiyo maana kulikuwa na usemi : Umekosa hata ualimu?
vipi upolis? vipi uganga na vipi jeshi?Ndiyo maana kulikuwa na usemi : Umekosa hata ualimu?
Ndio maana tunaambiwa kabla ya kuzungumza kitu kifanyie utafiti kwanza huyo mheshimiwa hajafanya utafiti wa kutosha kuja na hitimisho hilo, kuna utafiti usio rasmi niliufanya kwenye shule tatu nikabaini kwamba walimu wazuri wanaokubalika na wanafunzi ni wale wenye diploma na kama ujuavyo walimu wenye diploma ni wale waliokosa sifa za kwenda chuo (wengi wao).Tena unaweza kuwa na akili sana ya kufaulu mtihani lakini ukashindwa kuwafundisha wengine wakuelewe lakini mwingine akawa na ufaulu wa kawaida akawa mzuri sana kuelewesha,cha muhimu ni kwamba walimu wanakwenda kufundisha wakiwa wamepitia mafunzo ya ualimu na kufaulu mitihani yao ya mafunzo,ACHENI MWALIMU AITWE MWALIMU,tusijifanye wajuaji sana wakati ujuaji wenyewe tumepewa na walimu hawa hawa.
Me too nimesoma Tanzania primary to A level. Niliposoma degree nje ndio nilipogundua mapungufu ya elimu yetu. Elimu ya Tanzania haimuandai mwanafunzi career wise ipo more academic.mimi nimesomea hapa hapa tanzania toka primary mpaka chuo kikuu. nimefundishwa na walimu haohao anaosema bashe kwamba ni chaka la waliofeli. unavyosema walimu ni failures unamaanisha nini? je hawa hawakufaulu mafunzo yao ya uwalimu? mimi ingawa sio mwalimu lakini nitauenzi mchango wa walimu daima dumu. changamoto kubwa za elimu zinasababishwa na serikali kutokuweka mkazo mzito kwenye elimu. tusiwadhalilishe walimu kwa kutumia mapungufu yaliyopo sekta ya elimu. serikalj itatue changamoto za elimu.
Anawaumbua bila shaka, huu ndo ukweliBashe jiangalie
Exams performance is not enough to determine the performance of the students, we need students to be assessed in different ways therefore assignment and half terms testsMkuu mbona umeniwahi kusema nilichotaka kusema?
Na tena katika mazingira yaliyopo nchini kama yale ya mitihani kuvuja bado kufaulu mtihani hakujawa kigezo sahihi sana cha kulinganisha uelewa na akili za watu,unaweza ukazuzuka na division one ya kubebwa na mazingira machafu ukaidharau division three ya kuchakarika kumbe mwenye three akawa mzuri kuliko mwenye one na tumeshuhudia haya vyuoni,utakuta mtu ameingia chuo na division two ya point kumi na moja anazikimbiza one za point tano tena kwa mbali sana.
Na kama tunaamini akili na uwezo wa mwanafunzi kupitia mitihani ni kwanini hatuwaamini walimu hawa ambao wamepita chuoni na kuhitimu baada ya kufaulu mitihani yao?Na mbona tuna kumbukumbu ya walimu ambao ni wazuri sana kwa kufundisha kwenye levels hizo za primary na secondary schools(ambao tunawaita walifeli)kuliko hata baadhi ya walimu wanaofundisha vyuo vikuu?(ambao hubakishwa kuwa walimu kwa kuwa wamefaulu sana)
Siko mbali nae ila serikali ianze kwanza kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza kwa mazingira ya sasa hata ukiwachukua wanafunzi wenye daraja la kwanza ukawapeleka kufundisha bado wanafunzi watafeli tu.
Vile vile kuna tofauti kubwa ya kufundisha na ufaulu kuna walimu ndiyo walifeli wakaenda ualimu lakini uwezo wao kufundisha ni mkubwa kuliko wale waliofaulu, mfumo wetu wa elimu mbovu bado unashindwa kumtofautisha mtu aliyefaulu na yule aliyefeli, kuna watu wana ufaulu hafifu lakini ni watendaji wazuri (wakiwemo walimu) suala elimu ni mtambuka sana linaanza hata kwa mzazi mwenyewe
Mwalimu ni Mwezeshaji tu kujifunza ni mwanafunzi mwenyewe.
i agree on that 100%.Exams performance is not enough to determine the performance of the students, we need students to be assessed in different ways therefore assignment and half terms tests
Umekosea kuquote au?Unaogopa nini??
kwa hili nakubaliana nawe. ila kusema walimu wetu ni chaka la waliofeli i dont agree 100%. wako walimu waliamua kujiunga na mafunzo ya ualimu kwa vile serikali waliweka uwalimu kama moja ya fani ya kupata mkopo toka taasisi ya mikopo. wengine tulimaliza nao A level tena walipata tu na wengine one. mkopo ulipelekea waamue kusomea uwalimu. bado naamini serikalj ina mchango mkubwa wa kushusha ubora wa elimu yetu.Me too nimesoma Tanzania primary to A level. Niliposoma degree nje ndio nilipogundua mapungufu ya elimu yetu. Elimu ya Tanzania haimuandai mwanafunzi career wise ipo more academic.
Mwanafunzi wa A level anasoma let say business, apart from kusoma the theories about businesses hajui how to apply them in real life.
Wakati Elimu za wenzetu by the time upo A level unakuwa prepared to work in the firm through internships or report writing ambapo unapata na mental from those firms to guide the students.
In Tanzania, walimu wenyewe hawana confidence hata wanachokifundisha, ukiwauliza maswali too much anakukomesha.
Na pia system yetu ina problem jinsi mwanafunzi anavyokuwa assessed, exams assessment is not enough to determine the students performance. Hivyo system needs to be changed
By that, you can see a problem in our education system. Serikali needs to do something la sivyo tutaendelea kuwa taifa la mambumbu yani lisilojua any better
Umenikumbusha wakati nipo primary kulikua na Mwalim wetu wa michezo, sasa alikua anatafuta wachezaji wataowakilisha Shule yetu kwenye mashindano ya Umitashumita, basi yule mwalim alikua anapenda Sana mtu akipiga kichwa mpira, basi ikitokea mpira umekuja juu ukiupiga kwa kichwa tu utasikia "Mwandike huyo atakua mchezaji mzuri! Umeona kapiga kichwa" na mwisho wa siku team yetu ya shule haikufika kokote, ilichezea kichapo cha kufa mtu!
Namuunga mkono hoja kwa asilimia 95% maana mfumo wa elimu yetu hauendani na matazamio yetu. Hivi hawa watunga sera wa Tanganyika wanashindwa hata kupitapita kwenye vijitabu vya kale walau kujua ilikuwaje Wachina wakafanikiwa kwenye Green Revolution, bara Ulaya walifanya nini wakafanikiwa kupitia kwenye tanuri la mapinduzi ya viwanda na inakuwaje tunaamini kwamba tutafanikiwa kiviwanda wakati watu wetu wanasoma kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu bila kuwa na historia ya kulifahamu vyema jembe au walau kushika nyundo?
Tunataka viwanda ambavyo mzizi wake hautokani na ubunifu au ugunduzi uliounganishwa na kilimo? Maendeleo ya viwanda hayatakuwepo ikiwa wanafunzi wataishia kuona jembe na nyundo kwenye bendera ya CCM pekee pasipo kuwatengenezea mazingira ya kuwa na tamaa ya kuhitaji trekta ili lichukue nafasi ya jembe lililopo katika bendera ya CCM au crusher litakalobadili nyundo iliyopo katika bendera ya CCM.
Huu ni mkweli mchungu katika taifa letu lakini ukweli utabaki kwamba mtoto umleavyo ndivyo akuavyo katika taifa hivyo aliyesoma kwa nadharia ataishi kinadharia.😵
vazi lake linatisha