Tena unaweza kuwa na akili sana ya kufaulu mtihani lakini ukashindwa kuwafundisha wengine wakuelewe lakini mwingine akawa na ufaulu wa kawaida akawa mzuri sana kuelewesha,cha muhimu ni kwamba walimu wanakwenda kufundisha wakiwa wamepitia mafunzo ya ualimu na kufaulu mitihani yao ya mafunzo,ACHENI MWALIMU AITWE MWALIMU,tusijifanye wajuaji sana wakati ujuaji wenyewe tumepewa na walimu hawa hawa.Tumefundishwa na walimu wa UPE darasa la saba lakini tulitoka vizuri kuzidi hawa wanaofundishwa na wenye diploma.
na usichoke kuzitupia humu!he's a friend of mine
bado kuna changamoto kubwa mkuu. unajuaje yule aliyepata division one form four ama form six alifaulu mwenyewe kwa uwezo wake? je ni sahihi kusema yule aliyepata four form six hana uwezo kuliko yule aliyepata one siku ya mtihani wa mwisho? tukibase tu kwenye vyeti ni shida. wenzetu marekani kipaumbele cha kwanza ni ujuzi na cha pili ni cheti. bado walimu wana mchango mkubwa kwa taifa letu. tatizo serikali imewapuuza...Hzo GPA kwan hazitengenezw humo vyuoni? Tunachohitaj ni wale walio fanya vizur kidato cha nne na sita,ndo wakasomee uwalimu.
ni kweli ndugu yangu tukichukua vyeti kama kigezo ni shida. mimi nimefundishwa na walimu wa UPE primary na nikafaulu vizuri na nikaenda Pugu sekondari. na tukiwa huko tulifundishwa na walimu wenye diploma na nilifaulu. leo shule nyingi zina walimu wenye degree kuliko diploma kwa nini wanafunzi wanafeli? sidhani kama shida kubwa ni walimu....Tena unaweza kuwa na akili sana ya kufaulu mtihani lakini ukashindwa kuwafundisha wengine wakuelewe lakini mwingine akawa na ufaulu wa kawaida akawa mzuri sana kuelewesha,cha muhimu ni kwamba walimu wanakwenda kufundisha wakiwa wamepitia mafunzo ya ualimu na kufaulu mitihani yao ya mafunzo,ACHENI MWALIMU AITWE MWALIMU,tusijifanye wajuaji sana wakati ujuaji wenyewe tumepewa na walimu hawa hawa.
Swali zuri sana mkuu, a philosophical one.Mbona Bashe kila anachoongea kinaletwa hapa JF?
We jamaa hebu uje napokaa upate japo kinywaji. Well said!Siko mbali nae ila serikali ianze kwanza kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza kwa mazingira ya sasa hata ukiwachukua wanafunzi wenye daraja la kwanza ukawapeleka kufundisha bado wanafunzi watafeli tu.
Vile vile kuna tofauti kubwa ya kufundisha na ufaulu kuna walimu ndiyo walifeli wakaenda ualimu lakini uwezo wao kufundisha ni mkubwa kuliko wale waliofaulu, mfumo wetu wa elimu mbovu bado unashindwa kumtofautisha mtu aliyefaulu na yule aliyefeli, kuna watu wana ufaulu hafifu lakini ni watendaji wazuri (wakiwemo walimu) suala elimu ni mtambuka sana linaanza hata kwa mzazi mwenyewe
Mwalimu ni Mwezeshaji tu kujifunza ni mwanafunzi mwenyewe.
Walimu mnalalamika mishahara midogo, mbona nikiangalia salary slip zenu naona mishahara mnawazidi hata watumishi wengine wa serikali? Scale za mishahara kwa watumishi wa serikali ni zile zile. Wenye degree wanapokea TGS D, wenye diploma TGS C, wenye certificate TGS B, nk. Watumishi wengine wa serikali wanawazidi kwa visafari safari vya siku mbili tatu tu! Mwezi huo akikosa safari mnalingana kipato. Ushauri: Jitahidini muongeze ubunifu wa kazi zitakazopelekea kuwa na muda wa ziada ili mlipwe overtime allowances. Kwa mwalimu ambaye atajituma hadi masaa ya ziada atapata pesa nzuri ambayo itamfanya alingane kipato na mtumishi mwingine wa serikali ambaye anasafari za kikazi. Hiyo hoja ya bashe inaukweli ndani yake hasa kwenye kipengele cha uhaba wa wataalamu upande wa sayansi ambayo ndiyo inahitajika sana kwenye uendeshaji wa viwanda. Wanafunzi wenye ufaulu mzuri wanashindwa kwenda kufundisha sababu serikali haijawaandalia mazingira mazuri yanayowashawishi waingie kwenye fani hiyo. Mtu mwenye div one anaona akienda ualimu atakua amepoteza elimu yake bure.
ni kweli kwa sasa elimu yetu imeporomoka lakini chanzo ni serikali yenyewe. walimu wamepuuzwa. kwa mfano shule nyingi za primary vijijini hazina walimu wa kutosha. shule yenye walimu wengi hawazidi sita. pia kwa upande wa sekondari walimu wa masomo ya hisabati na sayansi ni shiida. tofauti na enzi zetu tukisoma.Huko primary kunasikitisha aisee ngazi ya degree nako ni sikitiko yaani Elimu yetu ni hovyo
mkuu uko sahihi. na sio huko tu je uganga vipi?Hivi police ndo wanakuwaga wamepata DV 1 ee
kwa hiyo huko elimu haihitajiki? kwa hiyo aliyepata division one siku ya mwisho ana akili nyingi kuliko aliyepata four eeh? haaa haaa....Kazi ya upolisi au tusema askari kwa ujumla haihitaji akili nyingi, inahitaji nguvu nyingi na akili kidogo.