Binafsi Sio Muumini sana wa haya mambo ya vyeti, sababu mifano hai tunayo hata Makazini mwetu humu, mtu anacheti kizuri, score nzuri lakini ufanisi na utendaji kazi wake hauendani na Grades/GPA's alizopata katika ngazi mbalimbali za Elimu..... Nafikiri kuna tatizo la kimfumo kuanzia namna ya Upatikanaji wa hawa Waalimu ambao tunawakabidhi Watoto wetu, mifumo ya kuwatrain na kuwaandaa hawa walimu, Mazingira ya kufanyia kazi, Mitaala ya Kielimu iliyopo, Maslahi ya walimu na mengineyo kama hayo....Elimu ikipewa hadhi yake inayostahili ni rahisi sana kama Taifa kufikia ndoto na mafanikio yetu ya elimu tunayoitamani.... Kuna watu wanavyeti vizuri tu na ni vihiyo/******(kama rais alivyosema).... Tuache Siasa kwenye Mambo ya msingi tusikimbilie kuhukum watu wa Division 4 tujiulize tu ni wapi tulikosea, na tuipe thamani elimu natuachane na hizi blah blah za division 4 mara One ambazo ni Siasa na sio uhalisia wa tatizo halisi la Elimu yetu ambayo inatengeneza watu wenye vyeti vizuri lakini wenye ufanisi mdogo katika utendaji kazi wa yale waliyoyapitia huko Madarasani.... I STAND TO BE CORRECTED