Bashe: Ualimu ni chaka la watu waliofeli, Hakuna dira ya taifa la viwanda

Bashe: Ualimu ni chaka la watu waliofeli, Hakuna dira ya taifa la viwanda

Akichangia kwenye bajeti ya Elimu mwaka 2016/17 mbunge wa Nzega Hussein Bashe amesema hali ya elimu nchini ni ya kusikitisha na hatari kwa ukuaji na usalama wa taifa, dira ya nchi haiendani na elimu inayotolewa, tunaenda kujenga taifa la viwanda lakini hatuna wataalamu wa sayansi

wale wanaofeli au kupata alama za mwisho za ufaulu ndio wanaenda kufundisha, amesema hii ni hatari sana kwani ni kama kujenga nyumba huku msingi wake ukiwa dhaifu mno


Huyu jamaa na ccm , sijui !! Tuombe Mungu .
 
Jamaa anajua anachokiongea sio Mawe mengine yaliyoenda bungeni kushangaa yani jitu bila aibu ooh sanamu lile litolewe awekwe fulani,mwingine oooh wapinzani wana sura mbaya
Bashe akiendelea hivi na JPJM asipoiunda upya CCM, miaka mitano hii itakuwa ya kwanza na ya mwisho; labda aondoke CCM.
 
Umenikumbusha wakati nipo primary kulikua na Mwalim wetu wa michezo, sasa alikua anatafuta wachezaji wataowakilisha Shule yetu kwenye mashindano ya Umitashumita, basi yule mwalim alikua anapenda Sana mtu akipiga kichwa mpira, basi ikitokea mpira umekuja juu ukiupiga kwa kichwa tu utasikia "Mwandike huyo atakua mchezaji mzuri! Umeona kapiga kichwa" na mwisho wa siku team yetu ya shule haikufika kokote, ilichezea kichapo cha kufa mtu!







Umekosea kuanza,ungeanza hadithi! hadithi!.......,
Kisha useme hadithi yako inatufundisha nini?Vinginevyo huyo uliyemquote,ulipaswa umtafute pm,huko mngeongea na kusimuliana hadithi zenu.
 
Nakumbuka mkuu.Ni vihiyo tu wasiokubali ukweli huu.
siku moja nilipost huku kuwa walimu ni kimbilio la watu waliofeli kuna watu wakanishambulia ila huo ndio ukweli lakini ili kupata walimu bora ni vizuri wakaboresha maslahi yao kwanza yawe juu kuliko hata wabunge
 
Hii mada kwa walimu wa shule za misingi na diploma hawaipendi kabisa yaani imetonesha kwenye vidonda vyao.Ukweli utabaki palepale hizo level ndizo vichaka halisi kwa waliofeli
haa haa kwa hiyo zamani na sasa walimu wengi walikuwa wa diploma ama degree? tulio wengi tukiwa sekindari za pugu na kibaha tumefundishwa na walimu wenye diploma na tulifaulu. hakukuwa na walimu wengi wenye degree kama ilivyo sasa. kumbuka jeuri yako hii imetokana na kufundishwa na walimu hao unaowaita wamefeli.
 
Kusema ukweli.... Watu niliosoma nao o level then wakafeli ndio wameenda kusomea ualimu wa primary. Hivyohivyo high school waliofeli nao walienda kusomea ualimu. Poleni sana wadogo zangu...
Kuna huyo mmoja alikuaga hawezi hesabu kabisa, lakini sasa anafundisha hesabu na sayansi shule ya msingi dah... Poleni sana
 
siku moja nilipost huku kuwa walimu ni kimbilio la watu waliofeli kuna watu wakanishambulia ila huo ndio ukweli lakini ili kupata walimu bora ni vizuri wakaboresha maslahi yao kwanza yawe juu kuliko hata wabunge
form six matokeo ni div two kama miaka 11 ilopita na nimwalimu,huyu nae alifeli!?
 
Hii mada kwa walimu wa shule za misingi na diploma hawaipendi kabisa yaani imetonesha kwenye vidonda vyao.Ukweli utabaki palepale hizo level ndizo vichaka halisi kwa waliofeli
Hata mimi mwenye Degree ya UDSM imetonesha kwenye kidonda kwasababu namimi ni mwalimu japokuwa nilifaulu
 
Serikali inabidi ilitazame jambo hili walimu inabidi wawe na minimum division two na GPA ya upper second. Sio mtu ana gentlemen tu huku form six ana dv Three eti anakabidhiwa watoto awafundishe, serikali ianze kupitia sifa za walimu.
Hapa tutafukuzwa wengi mkuu
 
sekta ya elimu ni moja ya sekta ambayo iliharibiwa sana kwa sababu ya kuingizwa siasa na maslahi duni ya walimu hata pale serikali ilipokuja na mikakati mbalimbali ya kufufua elimu lakini mikakati hiyo ililenga kuongeza majengo na madawati ,kuongeza ufaulu bila kuangalia maslahi duni ya walimu.Hali hii ilipeleka walio na sifa ya kujiunga kusomea kozi ya walimu kuikimbia fani hii.Kutokana na tatizo la ajira watu waliopata maksi za chini wengi walikimbilia kusomea fani hiyo ingawa hawakuwa na sifa, hao watu tunawajua kwani ni ndugu zetu,marafiki zetu wengine tumesoma nao haimaanishi kuwa ni wote hawana sifa ila wengi hawakuwa na sifa pia kumbuka iliingizwa siasa ya kubadilisha madaraja ili mradi ionekane ufaulu umeongezeka
Ushahidi kama kweli waliokuwa wanaingia hawakuwa na sifa ni hatua ya hivi karibuni ya waziri wa elimu kuwasimamisha baadhi ya vigogo wa TCU kwa sababu ya kuruhusu udahili wa wanafunzi wasio na sifa kujiunga elimu ya juu kusomea kozi kama za uwalimu
 
Hii hoja haina uhalisia kiasi hichi ambacho watu wanaamin' mm ni mwalimu, nafundsha secondary-Kahama, nina BA(ED) ya DUCE upper second, ACSEE nina div 2 point 10, CSEE nina div 3 point 22! Sasa inamaana mm nlifeli? Yawezekana wapo waliofeli lakin si kwa kiwango hichi ambacho watu wanaamini! Mfumo uliowekwa na serikali haswa kwa walimu wa primary ndio tatzo' huko primary yawezekana wapo wengi waliofeli hata wengine kugushi vyeti
 
sekta ya elimu ni moja ya sekta ambayo iliharibiwa sana kwa sababu ya kuingizwa siasa na maslahi duni ya walimu hata pale serikali ilipokuja na mikakati mbalimbali ya kufufua elimu lakini mikakati hiyo ililenga kuongeza majengo na madawati ,kuongeza ufaulu bila kuangalia maslahi duni ya walimu.Hali hii ilipeleka walio na sifa ya kujiunga kusomea kozi ya walimu kuikimbia fani hii.Kutokana na tatizo la ajira watu waliopata maksi za chini wengi walikimbilia kusomea fani hiyo ingawa hawakuwa na sifa, hao watu tunawajua kwani ni ndugu zetu,marafiki zetu wengine tumesoma nao haimaanishi kuwa ni wote hawana sifa ila wengi hawakuwa na sifa pia kumbuka iliingizwa siasa ya kubadilisha madaraja ili mradi ionekane ufaulu umeongezeka
Ushahidi kama kweli waliokuwa wanaingia hawakuwa na sifa ni hatua ya hivi karibuni ya waziri wa elimu kuwasimamisha baadhi ya vigogo wa TCU kwa sababu ya kuruhusu udahili wa wanafunzi wasio na sifa kujiunga elimu ya juu kusomea kozi kama za uwalimu
 
Ualimu pasua kichwa,mtu ana 4 ya pointi 32 anakwenda kusomea ualimu?,
Anakwenda kusoma nini wakati mwenyewe ndiyo hivyo tena,hapo unatarajia mtoto wako atokea na DV 1,2 au 3?
 
Namuunga mkono hoja kwa asilimia 95% maana mfumo wa elimu yetu hauendani na matazamio yetu. Hivi hawa watunga sera wa Tanganyika wanashindwa hata kupitapita kwenye vijitabu vya kale walau kujua ilikuwaje Wachina wakafanikiwa kwenye Green Revolution, bara Ulaya walifanya nini wakafanikiwa kupitia kwenye tanuri la mapinduzi ya viwanda na inakuwaje tunaamini kwamba tutafanikiwa kiviwanda wakati watu wetu wanasoma kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu bila kuwa na historia ya kulifahamu vyema jembe au walau kushika nyundo?
Tunataka viwanda ambavyo mzizi wake hautokani na ubunifu au ugunduzi uliounganishwa na kilimo? Maendeleo ya viwanda hayatakuwepo ikiwa wanafunzi wataishia kuona jembe na nyundo kwenye bendera ya CCM pekee pasipo kuwatengenezea mazingira ya kuwa na tamaa ya kuhitaji trekta ili lichukue nafasi ya jembe lililopo katika bendera ya CCM au crusher litakalobadili nyundo iliyopo katika bendera ya CCM.
Huu ni mkweli mchungu katika taifa letu lakini ukweli utabaki kwamba mtoto umleavyo ndivyo akuavyo katika taifa hivyo aliyesoma kwa nadharia ataishi kinadharia.😵
Mbona hamuungi mkono kuwa wabunge nao ni chaka la waliofeli na ndiyo maana wanatuletea sera na mipango ya elimu mibovu
 
Akichangia kwenye bajeti ya Elimu mwaka 2016/17 mbunge wa Nzega Hussein Bashe amesema hali ya elimu nchini ni ya kusikitisha na hatari kwa ukuaji na usalama wa taifa, dira ya nchi haiendani na elimu inayotolewa, tunaenda kujenga taifa la viwanda lakini hatuna wataalamu wa sayansi

wale wanaofeli au kupata alama za mwisho za ufaulu ndio wanaenda kufundisha, amesema hii ni hatari sana kwani ni kama kujenga nyumba huku msingi wake ukiwa dhaifu mno



Kapatia sana lakini kasema uogo kuwa tangu 1961 tuliangalia quatity na si quality. Hivi anaweza kulinganisha ufaulu wa miaka ya 70 na wa sasa. Uwongo mmoja huharibu ukweli wote
 
Dhana ya mtihani ikitumika vibaya inaweza kuzalisha wahalifu kama wezi wa mitihani na majawabu yake na waghushi vyeti feki ili wafikie malengo yao mazuri kupitia uhalifu.Mtihani utoshe tu kupima uwezo wa kukumbuka maarifa uliyojifunza.Haingii akilni umuulize mtu aliyefaulu umkalishe umpe mtihani uleule au mwingine afanye uone kama atapata alama zilezile,na kwa aliyefeli hivyohivyo.Utapata matokeo mengine tu.Mtihani utumike kupima na kuona ni kwa namna gani mtu anaweza kuchanganua masuala yanayaikabili jamii yake katika sekta za uzalishaji mali na sekta ya kutoa huduma.Dhana ya mtihani kama zana imekuwa ikitumika vibaya kudunisha na kufifisha uwezo wa mtu huku mwingine akiinuliwa kuendelea mbele na masomo.Wengi wamedumaa kifikra na kimaono na wanajiona hawana uwezo wa kusaidia jamii zao hata kama walisoma kwa kuwa tu walifanya mtihani wakafeli.Huu mtazamo unaotumiwa na jamii yetu.Elimu yetu ina vizingiti vingi sana vinavyochochea uhalifu mwingi tu katika jamii.Watu wakikosa elimu ni hatari tupu.WATU WASOME.
 
Back
Top Bottom