Bashe: Ualimu ni chaka la watu waliofeli, Hakuna dira ya taifa la viwanda

Bashe: Ualimu ni chaka la watu waliofeli, Hakuna dira ya taifa la viwanda

Kwa hiyo mnasubiri serikali ije iweke mazingira mazuri,miundonbinu mizuri.Kwani nyie wananchi mmejipangaje?
mkuu unataka sisi wananchi ndo tulipe maslah mazuri kwa walimu au? tuchonge barabara nzuri na madaraja kwa ajiri ya waalimu kupta wanapokwenda kufuata mshahara? au tulete minara ya simu?.
 
Bashe! Bashe! Bashe! Una point lakini kumbuka aliyekufikisha hapo ni huyo unayemdiss, tumia busara na akili kwenye kutoa mawazo yako
Mkuu ukweli mchungu.Kama kweli tunahitaji mabadiliko katika sekta ya elimu.
 
Bashe tunamjua vizuri,ngoja tumpe chama magufuli mwezi ujao
Hongera bashe lkn kumbuka waandishi wako new habari hawana mishahara wanakaa zaidi miezi 3 bila malipo wanaishi ktk mazingira magumu na wewe ukiwa mtendaji mkuu.

Wakati unawasemea walimu wakumbuke na waandishi wako hawana wa kuwasemea wanaishi kwa bahasha.
 
mkuu unataka sisi wananchi ndo tulipe maslah mazuri kwa walimu au? tuchonge barabara nzuri na madaraja kwa ajiri ya waalimu kupta wanapokwenda kufuata mshahara? au tulete minara ya simu?.
Mimi naongelea kuhusu shule.Barabara ni kazi ya halmashauri.Si mnalipa kodi au mnawachia madiwani na DED wagawane.
 
kauli hizi za bashe si za kushangiliwa harakahara. ushahidi wa kwamba walimu ni kada ya watu waliofeli unahitajika hapa. je walimu hawakufaulu mafunzo yao ya uwalimu wakiwa chuoni? je kama ni kupata daraja la tatu au la nne form four mbona kwenye fani ya uganga wengi huchukuliwa waliopata four? mbona hatusikii mambo haya? bashe afafanue hili vizuri vinginevyo itamletea shida japo ana nia malengo mazuri japokuwa uwasilishaji ni tatizo.
 
sio kila anayepata division two kwenye mtihani wa taifa anaakiri kupita yule aliyepata division four kwenye mtihani huo huo. ushahidi ninao, kuna dogo mmoja alikuwa shule ya kata ya hapa kijijini, huyu dogo kwa mitihani ya ndani alikuwa anakimbiza sana (one na two zilikuwa kawaida sana kwake) hadi ile ya mikoa na wilaya (mock) hakuna aliyekuwa anamkamata, lkn cha ajabu NECTA dogo akagonga four ya 26 wale wenzake aliokuwa anawakimbiza wakapiga three nzuri wakaendelea mbele yule dogo akaenda kusomea ualimu wa primary kiroho safi, sasa hebu hapo tuambizane nani alifaa kuwa mwalimu kati ya dogo na hawa wenzake?. tusidanganyane kuwa ualimu hadi ufaulu, hiyo ni hapana badala yake ni kuwa kazi yoyote ili mtu aipende ni kulipwa vizuri na mazingira mazuri ya kufanyia kazi FULL STOP.

Ndio mana tunataka mabadiliko ktk sector ya elimu Tanzania kutokana nanmatatizo km hayo. Njia zinazotumika ku assess performance za wanafunzi ni wrong. How could a student be assessed na only one exam?

Wizara inabidi ianze upya kufumua hiyo system waliyonayo. Wanafunzi wantakiwa kuwa assessed kutokana na assignments, half terms tests na exams. Hiyo itasaidia wale watakaofeli exams lkn kuna assignments zinawabeba.

Lazima tuungane kupigia kelele wizara ya elimu kubadili system yake ili kuwapa chances wanafunzi wote kuendelea na elimu ya juu
 
kauli hizi za bashe si za kushangiliwa harakahara. ushahidi wa kwamba walimu ni kada ya watu waliofeli unahitajika hapa. je walimu hawakufaulu mafunzo yao ya uwalimu wakiwa chuoni? je kama ni kupata daraja la tatu au la nne form four mbona kwenye fani ya uganga wengi huchukuliwa waliopata four? mbona hatusikii mambo haya? bashe afafanue hili vizuri vinginevyo itamletea shida japo ana nia malengo mazuri japokuwa uwasilishaji ni tatizo.
Kwani mwenzetu umesomea wapi sio Tanzania hii? Ina maana haya ulikuwa huyajui au unapenda ku criticise kila kitu ili mradi na ww umesema.

Unataka kutuambia hujui km walimu ni failures?
 
Bashe! Bashe! Bashe! Una point lakini kumbuka aliyekufikisha hapo ni huyo unayemdiss, tumia busara na akili kwenye kutoa mawazo yako

Ukweli mchungu, watanzania hatujazoea kusema ukweli yani mtu akisema ukweki lazima watokee wanafki wa kukukatisha tamaa
 
Umenikumbusha wakati nipo primary kulikua na Mwalim wetu wa michezo, sasa alikua anatafuta wachezaji wataowakilisha Shule yetu kwenye mashindano ya Umitashumita, basi yule mwalim alikua anapenda Sana mtu akipiga kichwa mpira, basi ikitokea mpira umekuja juu ukiupiga kwa kichwa tu utasikia "Mwandike huyo atakua mchezaji mzuri! Umeona kapiga kichwa" na mwisho wa siku team yetu ya shule haikufika kokote, ilichezea kichapo cha kufa mtu!

Hahahaaaa....kichwa tu kinakufanya kuwa mchezaji mzuri duuuuu
 
Tumefundishwa na walimu wa UPE darasa la saba lakini tulitoka vizuri kuzidi hawa wanaofundishwa na wenye diploma.
 
Nchi za Ulaya miongoni mwa taaluma ambazo zinatiliwa mkazo katika kuangalia Academic credentials ni ualimu.
Hapa kwetu sijui nani alitudanganya .
 
sio kila anayepata division two kwenye mtihani wa taifa anaakiri kupita yule aliyepata division four kwenye mtihani huo huo. ushahidi ninao, kuna dogo mmoja alikuwa shule ya kata ya hapa kijijini, huyu dogo kwa mitihani ya ndani alikuwa anakimbiza sana (one na two zilikuwa kawaida sana kwake) hadi ile ya mikoa na wilaya (mock) hakuna aliyekuwa anamkamata, lkn cha ajabu NECTA dogo akagonga four ya 26 wale wenzake aliokuwa anawakimbiza wakapiga three nzuri wakaendelea mbele yule dogo akaenda kusomea ualimu wa primary kiroho safi, sasa hebu hapo tuambizane nani alifaa kuwa mwalimu kati ya dogo na hawa wenzake?. tusidanganyane kuwa ualimu hadi ufaulu, hiyo ni hapana badala yake ni kuwa kazi yoyote ili mtu aipende ni kulipwa vizuri na mazingira mazuri ya kufanyia kazi FULL STOP.
Mkuu mbona umeniwahi kusema nilichotaka kusema?
Na tena katika mazingira yaliyopo nchini kama yale ya mitihani kuvuja bado kufaulu mtihani hakujawa kigezo sahihi sana cha kulinganisha uelewa na akili za watu,unaweza ukazuzuka na division one ya kubebwa na mazingira machafu ukaidharau division three ya kuchakarika kumbe mwenye three akawa mzuri kuliko mwenye one na tumeshuhudia haya vyuoni,utakuta mtu ameingia chuo na division two ya point kumi na moja anazikimbiza one za point tano tena kwa mbali sana.
Na kama tunaamini akili na uwezo wa mwanafunzi kupitia mitihani ni kwanini hatuwaamini walimu hawa ambao wamepita chuoni na kuhitimu baada ya kufaulu mitihani yao?Na mbona tuna kumbukumbu ya walimu ambao ni wazuri sana kwa kufundisha kwenye levels hizo za primary na secondary schools(ambao tunawaita walifeli)kuliko hata baadhi ya walimu wanaofundisha vyuo vikuu?(ambao hubakishwa kuwa walimu kwa kuwa wamefaulu sana)
 
Serikali inabidi ilitazame jambo hili walimu inabidi wawe na minimum division two na GPA ya upper second. Sio mtu ana gentlemen tu huku form six ana dv Three eti anakabidhiwa watoto awafundishe, serikali ianze kupitia sifa za walimu.
Hzo GPA kwan hazitengenezw humo vyuoni? Tunachohitaj ni wale walio fanya vizur kidato cha nne na sita,ndo wakasomee uwalimu.
"Hakuna dhambi mbaya kama woga".-Mh.Godbless Lema.
 
Ukweli mchungu, watanzania hatujazoea kusema ukweli yani mtu akisema ukweki lazima watokee wanafki wa kukukatisha tamaa
Sidhani kama unanisema mimi ila ni vema mwalimu asiwe victim wa dharau kila mahali...tuko nyuma ya keyboard zetu tukiandika tuandikayo kwa sababu ya huyo mwalimu
 
Kwani mwenzetu umesomea wapi sio Tanzania hii? Ina maana haya ulikuwa huyajui au unapenda ku criticise kila kitu ili mradi na ww umesema.

Unataka kutuambia hujui km walimu ni failures?
mimi nimesomea hapa hapa tanzania toka primary mpaka chuo kikuu. nimefundishwa na walimu haohao anaosema bashe kwamba ni chaka la waliofeli. unavyosema walimu ni failures unamaanisha nini? je hawa hawakufaulu mafunzo yao ya uwalimu? mimi ingawa sio mwalimu lakini nitauenzi mchango wa walimu daima dumu. changamoto kubwa za elimu zinasababishwa na serikali kutokuweka mkazo mzito kwenye elimu. tusiwadhalilishe walimu kwa kutumia mapungufu yaliyopo sekta ya elimu. serikalj itatue changamoto za elimu.
 
Back
Top Bottom