Bashe: Ualimu ni chaka la watu waliofeli, Hakuna dira ya taifa la viwanda

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Akichangia kwenye bajeti ya Elimu mwaka 2016/17 mbunge wa Nzega Hussein Bashe amesema hali ya elimu nchini ni ya kusikitisha na hatari kwa ukuaji na usalama wa taifa, dira ya nchi haiendani na elimu inayotolewa, tunaenda kujenga taifa la viwanda lakini hatuna wataalamu wa sayansi

wale wanaofeli au kupata alama za mwisho za ufaulu ndio wanaenda kufundisha, amesema hii ni hatari sana kwani ni kama kujenga nyumba huku msingi wake ukiwa dhaifu mno

Apewe Wizara ya Mambo ya ndan
Umenikumbusha wakati nipo primary kulikua na Mwalim wetu wa michezo, sasa alikua anatafuta wachezaji wataowakilisha Shule yetu kwenye mashindano ya Umitashumita, basi yule mwalim alikua anapenda Sana mtu akipiga kichwa mpira, basi ikitokea mpira umekuja juu ukiupiga kwa kichwa tu utasikia "Mwandike huyo atakua mchezaji mzuri! Umeona kapiga kichwa" na mwisho wa siku team yetu ya shule haikufika kokote, ilichezea kichapo cha kufa mtu!
 
Namuunga mkono hoja kwa asilimia 95% maana mfumo wa elimu yetu hauendani na matazamio yetu. Hivi hawa watunga sera wa Tanganyika wanashindwa hata kupitapita kwenye vijitabu vya kale walau kujua ilikuwaje Wachina wakafanikiwa kwenye Green Revolution, bara Ulaya walifanya nini wakafanikiwa kupitia kwenye tanuri la mapinduzi ya viwanda na inakuwaje tunaamini kwamba tutafanikiwa kiviwanda wakati watu wetu wanasoma kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu bila kuwa na historia ya kulifahamu vyema jembe au walau kushika nyundo?
Tunataka viwanda ambavyo mzizi wake hautokani na ubunifu au ugunduzi uliounganishwa na kilimo? Maendeleo ya viwanda hayatakuwepo ikiwa wanafunzi wataishia kuona jembe na nyundo kwenye bendera ya CCM pekee pasipo kuwatengenezea mazingira ya kuwa na tamaa ya kuhitaji trekta ili lichukue nafasi ya jembe lililopo katika bendera ya CCM au crusher litakalobadili nyundo iliyopo katika bendera ya CCM.
Huu ni mkweli mchungu katika taifa letu lakini ukweli utabaki kwamba mtoto umleavyo ndivyo akuavyo katika taifa hivyo aliyesoma kwa nadharia ataishi kinadharia.o_O
 
Hongera Mh.Bashe kwa kuongea ukweli.Mimi kwa mawazo yangu wanafunzi wanapata grade za juu ndio wawe waalimu.Walipwe mishahara minono kuliko hata Wabunge.Wabunge walipwe mara mbili ya madiwani.Kitendo cha wanafunzi waliofeli kuwa walimu tumejitia kwenye kitanzi kama nchi.
 
Serikali inabidi ilitazame jambo hili walimu inabidi wawe na minimum division two na GPA ya upper second. Sio mtu ana gentlemen tu huku form six ana dv Three eti anakabidhiwa watoto awafundishe, serikali ianze kupitia sifa za walimu.
 
Akichangia kwenye bajeti ya Elimu mwaka 2016/17 mbunge wa Nzega Hussein Bashe amesema hali ya elimu nchini ni ya kusikitisha na hatari kwa ukuaji na usalama wa taifa, dira ya nchi haiendani na elimu inayotolewa, tunaenda kujenga taifa la viwanda lakini hatuna wataalamu wa sayansi

wale wanaofeli au kupata alama za mwisho za ufaulu ndio wanaenda kufundisha, amesema hii ni hatari sana kwani ni kama kujenga nyumba huku msingi wake ukiwa dhaifu mno

Mbona Bashe kila anachoongea kinaletwa hapa JF?
 
nanukuu. "UALIMU NA ELIMU VIPEWE UMUHIMU" wakimaliza hapo na kuipa thamani taaluma ya ualmu kama zilivyo taaluma nyingine na kubadilisha ile dhana kuwa ualimu ni kazi ya wito basi tutasguhudia mabadiliko makubwa sana katika elimu.
 
Umenikumbusha wakati nipo primary kulikua na Mwalim wetu wa michezo, sasa alikua anatafuta wachezaji wataowakilisha Shule yetu kwenye mashindano ya Umitashumita, basi yule mwalim alikua anapenda Sana mtu akipiga kichwa mpira, basi ikitokea mpira umekuja juu ukiupiga kwa kichwa tu utasikia "Mwandike huyo atakua mchezaji mzuri! Umeona kapiga kichwa" na mwisho wa siku team yetu ya shule haikufika kokote, ilichezea kichapo cha kufa mtu!
Hadithi hadithiii.....malizia basi!
 
Siko mbali nae ila serikali ianze kwanza kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza kwa mazingira ya sasa hata ukiwachukua wanafunzi wenye daraja la kwanza ukawapeleka kufundisha bado wanafunzi watafeli tu.
Vile vile kuna tofauti kubwa ya kufundisha na ufaulu kuna walimu ndiyo walifeli wakaenda ualimu lakini uwezo wao kufundisha ni mkubwa kuliko wale waliofaulu, mfumo wetu wa elimu mbovu bado unashindwa kumtofautisha mtu aliyefaulu na yule aliyefeli, kuna watu wana ufaulu hafifu lakini ni watendaji wazuri (wakiwemo walimu) suala elimu ni mtambuka sana linaanza hata kwa mzazi mwenyewe
Mwalimu ni Mwezeshaji tu kujifunza ni mwanafunzi mwenyewe.
 
Hongera Mh.Bashe kwa kuongea ukweli.Mimi kwa mawazo yangu wanafunzi wanapata grade za juu ndio wawe waalimu.Walipwe mishahara minono kuliko hata Wabunge.Wabunge walipwe mara mbili ya madiwani.Kitendo cha wanafunzi waliofeli kuwa walimu tumejitia kwenye kitanzi kama nchi.
Hii hoja nzuri saana St Joseph watakuwa walimu nchi nzima, maana GPA zao zipo vizuri saana.
 
Back
Top Bottom