kwahiyo rais na waziri mkuu ni watu waliofeli? kama ni hivyo anavyotaka kutuaminisha tutarajie nini kwa nchi yetu kama tunaongozwa na watu waliofeli? wakati mwingine kuwasifia watu kama hawa wanaoropoka ropoka hovyo na sisi tunajivisha joho la ujinga wao bila kujua.
yeye alifundishwa na walimu wa aina gani mpaka akafika hapo alipo ? atuambie kama yeye alifundishwa na walimu waliofaulu tu. hivi ufaulu kwake ni upi ? kupata A,B ,C au kupata threshold inayotakiwa kuweza kukwea ngazi nyingine?
anafikiri tatizo la elimu nchini limesababishwa na walimu waliofeli ? je wale waliofundishwa na standard 4 na sasa hivi ni maprofessor anaweza akawashawishi kwa kijihoja kama hiki? hajui kuwa walimu wote waliosimamia uchaguzi na waliompigia kampeni ni hao hao anaowatusi bila hata aibu?
wabunge wetu wajifunze namna ya kukosoa sera mbovu za serikali siyo kukimbilia kutafuta mchawi kwa kushambulia kada za watu. tatizo la elimu yetu ni mazingira mabovu ya kufundishia na kujifunzia.
tunawalazimisha walimu wakapigane vita wakati hawana silaha huku wakiwa na njaa tutashinda vita kwa hali hiyo?
mchango wa hovyo ever kuusikia kwa mbunge kijana tena kutoka kwetu Tabora. jinga mkubwa.