Bashe: Ualimu ni chaka la watu waliofeli, Hakuna dira ya taifa la viwanda

Bashe: Ualimu ni chaka la watu waliofeli, Hakuna dira ya taifa la viwanda

"Ona Kila Kitu kimewekwa Nyuma Kama Taaluma ya Ualimu" (Allen Snr 2016).
 
Akichangia kwenye bajeti ya Elimu mwaka 2016/17 mbunge wa Nzega Hussein Bashe amesema hali ya elimu nchini ni ya kusikitisha na hatari kwa ukuaji na usalama wa taifa, dira ya nchi haiendani na elimu inayotolewa, tunaenda kujenga taifa la viwanda lakini hatuna wataalamu wa sayansi

wale wanaofeli au kupata alama za mwisho za ufaulu ndio wanaenda kufundisha, amesema hii ni hatari sana kwani ni kama kujenga nyumba huku msingi wake ukiwa dhaifu mno


Mh. Bashe hoja yako ni nzuri lakini kuhusu "Ualimu" kuwa "chaka la waliofeli" sikubaliani nalo! Wapo waalimu waliobobea katika fani kadhaa na ni suala la mchakato na maandalizi ya kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji kupitia sera ya elimu kwa ajili ya kupata wananchi bora watakaokuwa na uwezo wa kujitegemea na kushiriki katika kuleta maendeleo ya nchi ( katika dira iliyowekwa)!!.. Labda sijakuelewa lakini Ualimu si kichaka....
 
Naomba mwalimu mwenye GPA ya 5.0 aje afundishe nanjilinji huku halafu tusubiri matokeo yake maana naona bado watu hawajui tatizo la elimu tanzania ni lipi, kila mtu ana ana rukaruka tu.
 
Kwani mwenzetu umesomea wapi sio Tanzania hii? Ina maana haya ulikuwa huyajui au unapenda ku criticise kila kitu ili mradi na ww umesema.

Unataka kutuambia hujui km walimu ni failures?
Lakin hao hao ndio walio kufanya ujue kubofya keyboard hapo ulipo aisee!! Ama kweli mnakata tawi mlilo kalia.
 
Ni kweli ila kujibu kitu ulicho kisoma kwa miaka mitatu ndani ya masaa mawili au matatu ni kazi.Watu tumetofautiana vichwa.
Kimsingi mfumo wa elimu yetu ni mbovu sana.
 
Hizo ni isolated cases,na hii inatokana na mazingira aliyonayo mtahiniwa siku ya mtihani.Niseme wazi hata hivyo kwamba it is not the rule of the game.The rule of the game ni kwamba anayepata division one ni smart kuliko wa division four.Naomba tusitetee vihiyo!
sio kila anayepata division two kwenye mtihani wa taifa anaakiri kupita yule aliyepata division four kwenye mtihani huo huo. ushahidi ninao, kuna dogo mmoja alikuwa shule ya kata ya hapa kijijini, huyu dogo kwa mitihani ya ndani alikuwa anakimbiza sana (one na two zilikuwa kawaida sana kwake) hadi ile ya mikoa na wilaya (mock) hakuna aliyekuwa anamkamata, lkn cha ajabu NECTA dogo akagonga four ya 26 wale wenzake aliokuwa anawakimbiza wakapiga three nzuri wakaendelea mbele yule dogo akaenda kusomea ualimu wa primary kiroho safi, sasa hebu hapo tuambizane nani alifaa kuwa mwalimu kati ya dogo na hawa wenzake?. tusidanganyane kuwa ualimu hadi ufaulu, hiyo ni hapana badala yake ni kuwa kazi yoyote ili mtu aipende ni kulipwa vizuri na mazingira mazuri ya kufanyia kazi FULL STOP.
 
Mishahara ingepangwa kulingana na ufaulu ingefanya hata wanaopata div 1 wafikirie kujiunga ualimu... Mwenye div 4 alipwe kiasi kisichozidi 150,000/=

Duniani note mishahara hulipwa kulingana na uzito/umuhimu wa kazi husika;si kwa kigezo cha ufaulu.
 
Siyo kweli walimu wote walikuwa na ufaulu was chini. Tatizo ni malipo duni, mazingira duni ya kazi na kukosekana usimamizi kutoka kwa maafisa elimu na walimu wakuu. Mwalimu akithaminiwa elimu itakuwa salama; Ukimdharau mwalimu unahatarisha elimu ya mtoto wako.
 
Duniani note mishahara hulipwa kulingana na uzito/umuhimu wa kazi husika;si kwa kigezo cha ufaulu.
Nafikiri hujanipata concern yangu,
1st: nimezungumzia kwenye idara moja(ualimu)
2nd: ni vipi tunaweza vutia watu wenye ufaulu mzuri kujiunga ualimu
3rd: how to discourage failures au watu wenye ufaulu mdogo
4th: Njia za kukuza na kuendeleza kiwango cha elimu TZ

Ulichosema ni kuhusu kiwango cha mishahara(kuwa inategemea umuhimu), nakukatalia kwa hiyo point otherwise uniambie ualimu hauna umuhimu- na ktk factor zinazodetermine salary hiyo ni point ndogo kbs
 
Hivi mambo ya elimu tuwaachie wataalamu Wa elimu,, ktk viwango vya assessment pass, na ,fail inafahamika,,kwan kuna mwalimu aliye na Zero?? huwezi Fanya selection ya one ukawapeleka kufundisha,,,hao wanaandaliwa kwa level za juu,,, watu Wa kati wanaandaliwa kwa level za kati,,, Alafu huu utamaduni wa kusema ualimu ni fani ya walofeli uishe,,, kama una scientific evidence toa ,,kama kuna waalimu wenye zero mana hyo ndo "fail"
 
Nafikiri hujanipata concern yangu,
1st: nimezungumzia kwenye idara moja(ualimu)
2nd: ni vipi tunaweza vutia watu wenye ufaulu mzuri kujiunga ualimu
3rd: how to discourage failures au watu wenye ufaulu mdogo
4th: Njia za kukuza na kuendeleza kiwango cha elimu TZ

Ulichosema ni kuhusu kiwango cha mishahara(kuwa inategemea umuhimu), nakukatalia kwa hiyo point otherwise uniambie ualimu hauna umuhimu- na ktk factor zinazodetermine salary hiyo ni point ndogo kbs

Watu wanaweza kuvutiwa kujiunga na ualimu iwapo mishahara itavutia, jamii itathamini ualimu, mazingira ya kazi yataboreshwa. Hayo yakifanyika serikali inaweza kudahili waliopata ufaulu wa juu kujiunga na taaluma ya ualimu.

Ni vigezo vipi vinadetermine viwango vya mishahara zaidi ya umuhimu na uzito wa kazi aifanyayo mtu? Sijasema ualimu si kazi muhimu.
 
Watu wanaweza kuvutiwa kujiunga na ualimu iwapo mishahara itavutia, jamii itathamini ualimu, mazingira ya kazi yataboreshwa. Hayo yakifanyika serikali inaweza kudahili waliopata ufaulu wa juu kujiunga na taaluma ya ualimu.

Ni vigezo vipi vinadetermine viwango vya mishahara zaidi ya umuhimu na uzito wa kazi aifanyayo mtu? Sijasema ualimu si kazi muhimu.
Google hizo factors, ukishajielemisha unaweza kurudi hapa. Mi ni expert eneo hili
 
Miye nachekaga sana watu wenye kauli kama za bashe Kwanza ningeomba CWT wamuombe bashe aombe razi walimu kwanini nasema hivyo

Kulingana na vigezo vya ufaulu Tanzania Mwanafunzi aliyefeli ni yule aliyepata Daraja la mwisho yani sufuri

Sasa swali ikiwa serikali kupitia wizara ya elimu inayodaili wanafunzi wanaoenda kusomea ngazi ya cheti na astashahada ya uwalimu ina daili wanafunzi waliofeli wenye sufuri basi tatizo ni la serikali

Na ikiwa TCU inachukua Mwanafunzi mwenye cutt off point chini ya 4. point 5 kusomea shahada yoyote ile basi TCU ni tatizo

Nini Nachotaka kusema

Bashe atambue serikali kupitia viongozi wajanja wa janja ndio imetufikisha hapa kwani uwalimu ilikuwa ni miongoni mwa taluma ambayo uwezi Unga Unga ukafikia ngazi ya shahada ikiwa huna ufaulu wa alama C tatu kidato cha nne na ufaulu wa kidato cha sita kama ilivyo taluma nyingine ambapo

Mtu anaufaulu mbovu kidato cha nne anaanza kusoma kozi ya cheti badae anaenda diploma badae shahada na ndio wengi wanaozarau walimu kutwa mfano

Wahasibu
Wanasheria wengi tu wakiombwa walete vyeti vyao vya kidato cha nne hapa tutakataana

Walimu wengi ni watoto wa kimaskini waliokimbilia ajira ili ku punguza njaa za familia zao na wao na ndio maana leo hii ukienda tasisi mbali mbali wakuu wengi wa idara hizo taluma zao za awali walikuwa walimu ila walipoanza kuikabili njaa wakabadili taluma zao na sasa wapo katika nafasi tofauti

Tusiwabeze walimu tukifanya hivyo tunakuwa tunawatusi viongozi wa taifa hili ambao walikuwa walimu ila utendaji kazi wao tunauona
 
Back
Top Bottom