Bashe: Ualimu ni chaka la watu waliofeli, Hakuna dira ya taifa la viwanda

Bashe: Ualimu ni chaka la watu waliofeli, Hakuna dira ya taifa la viwanda

Dhana ya mtihani ikitumika vibaya inaweza kuzalisha wahalifu kama wezi wa mitihani na majawabu yake na waghushi vyeti feki ili wafikie malengo yao mazuri kupitia uhalifu.Mtihani utoshe tu kupima uwezo wa kukumbuka maarifa uliyojifunza.Haingii akilni umuulize mtu aliyefaulu umkalishe umpe mtihani uleule au mwingine afanye uone kama atapata alama zilezile,na kwa aliyefeli hivyohivyo.Utapata matokeo mengine tu.Mtihani utumike kupima na kuona ni kwa namna gani mtu anaweza kuchanganua masuala yanayaikabili jamii yake katika sekta za uzalishaji mali na sekta ya kutoa huduma.Dhana ya mtihani kama zana imekuwa ikitumika vibaya kudunisha na kufifisha uwezo wa mtu huku mwingine akiinuliwa kuendelea mbele na masomo.Wengi wamedumaa kifikra na kimaono na wanajiona hawana uwezo wa kusaidia jamii zao hata kama walisoma kwa kuwa tu walifanya mtihani wakafeli.Huu mtazamo unaotumiwa na jamii yetu.Elimu yetu ina vizingiti vingi sana vinavyochochea uhalifu mwingi tu katika jamii.Watu wakikosa elimu ni hatari tupu.WATU WASOME.
 
Akichangia kwenye bajeti ya Elimu mwaka 2016/17 mbunge wa Nzega Hussein Bashe amesema hali ya elimu nchini ni ya kusikitisha na hatari kwa ukuaji na usalama wa taifa, dira ya nchi haiendani na elimu inayotolewa, tunaenda kujenga taifa la viwanda lakini hatuna wataalamu wa sayansi

wale wanaofeli au kupata alama za mwisho za ufaulu ndio wanaenda kufundisha, amesema hii ni hatari sana kwani ni kama kujenga nyumba huku msingi wake ukiwa dhaifu mno



Pamoja na kuwa GAMBA nimeananza kumfolow na kumkubali huyu dogo. Keep it up Bashe
 
Hongera Mh.Bashe kwa kuongea ukweli.Mimi kwa mawazo yangu wanafunzi wanapata grade za juu ndio wawe waalimu.Walipwe mishahara minono kuliko hata Wabunge.Wabunge walipwe mara mbili ya madiwani.Kitendo cha wanafunzi waliofeli kuwa walimu tumejitia kwenye kitanzi kama nchi.
Hawa watakao pata grade za juu tutawapata kutoka wapi na watafundishwa na walimu gani ili wapate alama za Juu?Maana walimu waliopo hawana alama za Juu sasa hao wanaopata alama za juu watatokea wapi?

Huenda tatizo la elimu yetu halijulikani
 
Bila shaka wewe ni product ya dr kisanga,mwituruban,kivelya,mzee wa kijuju viliage nk
Mwiturabani wa GE141(Climatology).
Kivelia wa GE142(Spatial Organization).
Vipi walikufundisha
 
Ndiyo kk,walinpiga msasa sana
Mimi sijawahi kufeli lakini nipo kundi la waliofeli,Kitendo cha kuchagua Bachelor of Arts with Education, naonekana nilifeli.
Ila tangu niajiriwe nilianza kukata tamaa juu ya kazi yangu.
Siwezi kuwa na wema wa mshumaa ni mwendo wa matangopori
 
Tatizo la elimu ya Tz ni lishe duni ya watanzania wengi hivyo vichwa vimedumaa hatuwezi kufikiri sawasawa.Hata waliofaulu darasani nao bado wamedumaa tu maana hata taaluma zao walizosomea wanashindwa kuzitumia sanasana wakakimbilia kwenye siasa ambako kigezo ni kujua kusoma na kuandika.
 
Mpaka sasa hvi wabunge wa ccm waliongea mambo ya maana wapo 2 tu. Bashe na Cosato Chumi. Wengine naona wasubiri posho tu.
 
kwahiyo rais na waziri mkuu ni watu waliofeli? kama ni hivyo anavyotaka kutuaminisha tutarajie nini kwa nchi yetu kama tunaongozwa na watu waliofeli? wakati mwingine kuwasifia watu kama hawa wanaoropoka ropoka hovyo na sisi tunajivisha joho la ujinga wao bila kujua.
yeye alifundishwa na walimu wa aina gani mpaka akafika hapo alipo ? atuambie kama yeye alifundishwa na walimu waliofaulu tu. hivi ufaulu kwake ni upi ? kupata A,B ,C au kupata threshold inayotakiwa kuweza kukwea ngazi nyingine?
anafikiri tatizo la elimu nchini limesababishwa na walimu waliofeli ? je wale waliofundishwa na standard 4 na sasa hivi ni maprofessor anaweza akawashawishi kwa kijihoja kama hiki? hajui kuwa walimu wote waliosimamia uchaguzi na waliompigia kampeni ni hao hao anaowatusi bila hata aibu?
wabunge wetu wajifunze namna ya kukosoa sera mbovu za serikali siyo kukimbilia kutafuta mchawi kwa kushambulia kada za watu. tatizo la elimu yetu ni mazingira mabovu ya kufundishia na kujifunzia.
tunawalazimisha walimu wakapigane vita wakati hawana silaha huku wakiwa na njaa tutashinda vita kwa hali hiyo?
mchango wa hovyo ever kuusikia kwa mbunge kijana tena kutoka kwetu Tabora. jinga mkubwa.
 
Alichosema Mheshimiwa Hussein Bashe kina ukweli...mm matokeo ya Form Four nilipiga Division Four nikaamua kusomea certificate ya ualimu nikaungaunga mpaka nikapata Degree kwa sasa nafundisha Midland...kiufupi sikustahili kuwa mwalimu ila maisha yamenipeleka huko...
 
Mimi sijawahi kufeli lakini nipo kundi la waliofeli,Kitendo cha kuchagua Bachelor of Arts with Education, naonekana nilifeli.
Ila tangu niajiriwe nilianza kukata tamaa juu ya kazi yangu.
Siwezi kuwa na wema wa mshumaa ni mwendo wa matangopori
Unawalisha sumu viongozi wajao wa taifa hili...lol
 
Kuna member wanamsifia bashe lakini akipewa uwaziri mtaona jinsi watu mtakavyo mponda!
 
kiujumla nakubaliana kwa 50% na mawazo ya bashe ila sikubaliani naye 100% kwamba kila aliyeko uwalimu alifeli. je mwalimu mzuri ni yule aliyepata GPA akiwa sekondari amayule aliyefaulu vizuri masomo ya ualimu? naheshimu dhana ya vyeti ingawa siafiki kwamba kila mwenye cheti kizuri ana uwezo wa kitu fulani. wako wanafunzi wana vyeti vizuri ila majibu ya mitihani walipewa siku ya mtihani. matatizo ya elimu yanachangiwa na serikali kutoweka kipaumbele kwenye elimu. kwa mfano kwenye shule zetu nyingi za kata walimu wa masomo ya hisabati na sayansi ni wa kutafuta kwa tochi. je tutapata mafanikio katika sekta mbalimbali kama madaktari, wahandisi na wengineo? je walimu wetu wanapewa updates za mambo yao na serikali? je serikali inawapa stahiki zipasazo? je mzingira ya kufundishia na kujifunzia yako vizuri huko mashuleni? je katika utungaji wa sera za elimu na mitaala ya elimu ni kiasi gani hao walimu wanashirikishwa?

Naona wewe unabishana na sera.
Sera inataka kila aliyefaulu vizuri aendelee na masomo ngazi inayofuata
Wenye ufaulu dhaifu hawezi kuendelea na masomo, bali wataenda kusoma fani fulani au kazi fulani,. Mtu akienda kusomea UALIMU maana yake kaenda kusomea kazi kwa kuwa ufaulu wake haimruhusu kuendelea.
Zamani wenye ufaulu dhaifu walisomea Upolisi, jeshi, ufundi mchundo( ujenzi,umeme,Bomba, mechanics etc). Hawa walisomea ajira direct wakati wenzao wakiendelea na masomo. Sasa hivi ajira za moja kwa moja toka chuoni hamna,, zaidi ya UALIMU.
 
Akichangia kwenye bajeti ya Elimu mwaka 2016/17 mbunge wa Nzega Hussein Bashe amesema hali ya elimu nchini ni ya kusikitisha na hatari kwa ukuaji na usalama wa taifa, dira ya nchi haiendani na elimu inayotolewa, tunaenda kujenga taifa la viwanda lakini hatuna wataalamu wa sayansi

wale wanaofeli au kupata alama za mwisho za ufaulu ndio wanaenda kufundisha, amesema hii ni hatari sana kwani ni kama kujenga nyumba huku msingi wake ukiwa dhaifu mno

 
Nadhani Bashe pia amefeli ndo maana kashindwa kutofautisha kati ya ufaulu wa chini na kufeli. Watu wanaodahiliwa kwa kozi za Ualimu hawajafeli bali walio wengi ufaulu wao ni wachini
 
Naona wewe unabishana na sera.
Sera inataka kila aliyefaulu vizuri aendelee na masomo ngazi inayofuata
Wenye ufaulu dhaifu hawezi kuendelea na masomo, bali wataenda kusoma fani fulani au kazi fulani,. Mtu akienda kusomea UALIMU maana yake kaenda kusomea kazi kwa kuwa ufaulu wake haimruhusu kuendelea.
Zamani wenye ufaulu dhaifu walisomea Upolisi, jeshi, ufundi mchundo( ujenzi,umeme,Bomba, mechanics etc). Hawa walisomea ajira direct wakati wenzao wakiendelea na masomo. Sasa hivi ajira za moja kwa moja toka chuoni hamna,, zaidi ya UALIMU.
Mimi nimefaulu hadi nimefika UDSM,nimesoma degree ya ualimu,leo hii mimi ni mwalimu,dhana ya kushindwa kuendelea ngazi nyingine inatoka wapi
 
Serikali inabidi ilitazame jambo hili walimu inabidi wawe na minimum division two na GPA ya upper second. Sio mtu ana gentlemen tu huku form six ana dv Three eti anakabidhiwa watoto awafundishe, serikali ianze kupitia sifa za walimu.
Hivi wewe form six ulisoma combination gani? Ulipata division ngapi?
 
Anatafuta cheap popularity huyu jamaa,ivi hapo mjegoni tukiwaambia kila mmoja afike na vyeti vyake vya kitaluuma hali itakuwaje humo mjengoni?.
 
Back
Top Bottom