Bashe anusurika kutekwa

Bashe anusurika kutekwa

hii stori mbona ipo kama imechonwa vile. muda wote ufuatiliwe halafu ushindwe kutoa taarifa polisi. ina maana Bashe hana contact za watu ambao wangeweza kujua hiyo noah wakati anaelekea kwake. maanake isije ikawa ni alibi ya kutaka huruma ya watu. lazima hii taarifa tuipokee kwa tahadhari kubwa. la mwisho kwani Bashe yeye mbaya wake si mmoja tuu na anamfahamu na alikwishamtaja kule Dodoma labda angempigia simu na kumuuliza vipi mzee.
]
Nakuunga mkono mia.
 
Sasa huyu bashe, kuendesha gari kutoka bamaga mpaka mbezi bado umeshindwa kushika numba? uemkutana nao uso kwa uso bado ukashindwa kupiga hata picha? We mwandishi wa aina gani?...Job true true....

Bashe sio mwandish wa habar!
 
Pole yake sana, hiyo ni kazi ya siasa za Tanzania kwa sasa, kazi tunayo
 
duh yaan nchi yetu inazidi kugeuka na kuwa kama MEXICO AU COLUMBIA?
eeeh MWENYEZI MUNGU IOKOE TANZANIA
 
Kama ndivyo ilivyokuwa basi inatisha, Ingawa kuna maelezo naona yanapungua hapa, Kufuatiliwa kwa zaidi ya saa nzima na ukitilia maanani sio muda mrefu kuna matukio yametokea ingetosha kumpa hofu juu ya usalama wake...Sasa je hapo glossary ndio palikuwa mahala salama zaidi kwake ? Si hata Dokta Ulimboka alitekwa akiwa glossary ? Pili...Yeye alishindwa kusoma namba na ndugu zake nao walishindwa kusoma namba ? Na si tunafahamu kuwa plate number huwa zinareflect ? kwani unahitaji taa za gari husika ndio uone namba ? Na mwisho taahadhari aliyochukua mbona haikuwa sahihi...kwa kuendelea kuingi nyumbani na kuwaacha ndugu waondoke badala ya kubaki pamoja kwani alishahisi mambo si shwari ? Nadhani ndugu yangu aweke maelezo vizuri kidogo....Ila nampa pole kwa maswahibu hayo....
 
Bashe wewe ni mpambambanaji wa kweli mungu yupo na wewe wanaoua kwa upanga nao watauwawa kwa upanga...nadhani adui yako unamfahamu..ata na yeye atashndwa mchana kweupe
 
Operesheni ng'oa kucha, meno na macho bila ganzi inaendelea. Je ni nani yuko nyuma ya matukio haya?
Sidhani kama bwana mdogo Kigwangala ana maujuzi haya.
Uraia wa Bashe nao uko mashakani licha ya kuwa Uhamiaji ilisha tusadikisha kuwa Bashe ni raia halali wa Tz

Membe huyo na TISS, Urais 2015 utatumaliza
 
Fyatu kuwa kama mtu mwenye akili alichofanya bwana bashe kwenda grosary ya jiran na nyumbani kwake 1. Kwanza anafahamika eneo husika na tayari atakuwa na watu wa karibu wa kujihami kwa lolote yeye si kichaa au ulitaka aendelee na safari ahatarishe uhai wake
 
Kwa hiyo ana hisi anafatiliwa na nani?
 
Hapo kwenye blue, labda uniambie kwamba umetoka shimoni leo hii lakini kama wewe unaishi hapa duniani utakuwa unaelewa kwamba hiki kitu kipo dunia nzima. Mimi nadhani badala ya kulalamika ungeutumia muda huu kufikiria namna ya wewe pia kuwa mtu mwenye nguvu kubwa ya kifedha na ushawishi mkubwa serikalini.

Unaendelea kupotosha ukweli kama kawaida yako; Sumu usitake kutunywesha sumu, upumbavu unao uongelea wewe huwezi kufanyika nchi yoyote ile duniani isipokuwa Tanzania tu; By ze way wewe umefika nchi gani tofauti na Bongo? au unafikiri hatukufahamu wewe?
 
Hapo kwenye blue, labda uniambie kwamba umetoka shimoni leo hii lakini kama wewe unaishi hapa duniani utakuwa unaelewa kwamba hiki kitu kipo dunia nzima. Mimi nadhani badala ya kulalamika ungeutumia muda huu kufikiria namna ya wewe pia kuwa mtu mwenye nguvu kubwa ya kifedha na ushawishi mkubwa serikalini.

Wow! wow!
 
Bashe ana hamu ya kutekwa.cha muhimu anunue dawa ya ganzi atembee nayo ndani ya gari.
Nakubaliana na hoja yako.
Ingawa hali iliopo sasa hivi walio wengi wanatembea kwa tahadhari kutokana na matukio ya kutekwa kisha kungolewa meno, macho na kucha bila ganzi, lakini tukio la huyu Bashe haliingii akilini mwangu mtu ufuatwe kitambo kirefu hivyo wakati ana nafasi ya kuwasiliana na vyombo vya usalama wafuatilie nani anamfuata kwa nyuma, na pengine angeweza kuendelea na safari hadi kuishia kitu cha polisi badala ya kwenda moja kwa moja nyumbani kama alikuwa na hakika anafuatwa. Kuna kitu hakijakaa sawa hapa.
 
Fyatu kuwa kama mtu mwenye akili alichofanya bwana bashe kwenda grosary ya jiran na nyumbani kwake 1. Kwanza anafahamika eneo husika na tayari atakuwa na watu wa karibu wa kujihami kwa lolote yeye si kichaa au ulitaka aendelee na safari ahatarishe uhai wake[/QUOTE]

Kwa historia tuliyonayo kwa matukio mawili yaliyopita Bashe hakuchukua tahadhari yoyote ya busara...Gari mbili hao wa glossary wangemlinda vipi kama kweli walikuwa ni watu wabaya ? pia hainiingii akilini kushindwa kusoma namba yeye na jamaa zake....Kwa tishio kubwa namna hiyo bado unaingia nyumbani kweli ? Na bado unawaacha jamaa waondoke wakuache hatarini ? mmmh....
 


JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

Kuna kitu kinasumbua kidogo. Nitoke Sinza mpaka Mbezi nikihisi nafuatiliwa na baada ya yaliyomtokea mwenzangu? Nina simu na nisiweze kutaarifu polis?
Haipandi unless nina uwezo wa kudhibiti lolote.
 
Polisi hawa hawa wanaong'oa watu meno bila ganzi na kunyofoa kucha kwa koleo ndo hawa hawa wanatoa RB na ni hawa hawa wanakuja kujichunguza baadae. We are finished!!!!!!!!!!!!!!

Nimeipenda mkuu!
 
hamna habari hapo. ni udaku tu wa bashe ili aendelee kuuza gazeti lake. njaa hizi balaa. kama walikutana uso kwa uso iweje asione namba za hilo gari?

Mkuu angalia details zako vizuri hapa chini; kisha utuambie kati yako na Bashe nani mwenye njaa;

Join Date : 28th March 2013

Posts : 22
Rep Power : 305
Likes Received2
Likes Given0
 
Back
Top Bottom