Bashe anusurika kutekwa

Bashe anusurika kutekwa

Bashe kapika SINEMA hii ili ku-draw attention ya watu.Kwanza amejuaje kama wanakuja kumteka?Je kama lengo ni kumpiga risasi na kuishia, wangempata vizuri aliposhuka hapo glossary.Ni ishara gani zilizoonyesha kwamba wanamfuata ili wamteke?
Itakuwa walikuwa wanatumia kipaza sauti
 
Matunda ya Rwakatare.
Uzuri kwa Mungu utasema kweli tu.leo utamsingizia yeyote yule.ila kwa Mungu hata kama muhusika baba yako utatuambia kweupe kuwa ni baba yangu.HAKUNA JINSI YA KUMKWEPA MUNGU.
 
JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

mmmh,jamani kwa kweli SI HUKUMU LAKINI TUWE MAKINI SANA,MAANA KUNA WATU WANAWEZA WAKAANZA KUZUSHA MAMBO KWA KUTUMIA SITOFAHAMU ILIYOPO TANZANIA SASA,napata shida sana kama muda wote huo aliozunguka na hawa jama kweli alishindwa fanya jitihada za kusoma number za magari hayo? pia mbona hajaweka wazi muda aliotoka kazini ili tuwe in a fairy position to judge,pia Bashe anajua anafuatiliwa toka Sinza mpaka mwenge,anapita tangibovu,..kweli alishindwa kupiga simu kwa jamaa zake kuwataarifu au wamfuatilie?
 
Hapo kwenye blue, labda uniambie kwamba umetoka shimoni leo hii lakini kama wewe unaishi hapa duniani utakuwa unaelewa kwamba hiki kitu kipo dunia nzima. Mimi nadhani badala ya kulalamika ungeutumia muda huu kufikiria namna ya wewe pia kuwa mtu mwenye nguvu kubwa ya kifedha na ushawishi mkubwa serikalini.

akishawaza ivo ndo iwe je sasa? Na kama duniani kote ndo kupo ivyo ndo waTz tukubaliane nalo na kulipokea na kuwa sehemu ya maisa yetu?
 
Kufuatiliwa kwa zaidi ya saa nzima kwa vyovyote alikuwa na muda wa kutosha kutoa taarifa polisi au kuomba ushauri kwa ndugu na marafiki wamwambie afanye nini, Au hata angeweza kuingia kwenye Hoteli yoyote kubwa "ya kitalii" ambazo naamini zina ulinzi wa silaha na angekaa hapo na kuomba msaada zaidi....sidhani kama haya yanahitaji elimu ya chuo kikuu kwa mtu kuchukua tahadhari ya hali unayoifahamu tayari...
 
Faida ya nchi corrapted ndo hii inakuwa shamba la walanguzi na genge la wahuni inaelekea kila sekta ya ungozi nchi hii kuanzia chini hadi juu imekaliwa na wala rushwa, wahuni, walanguzi ambao wanayafikiria matumbo yao na siyo maslahi ya Taifa
 
hii stori mbona ipo kama imechonwa vile. muda wote ufuatiliwe halafu ushindwe kutoa taarifa polisi. ina maana Bashe hana contact za watu ambao wangeweza kujua hiyo noah wakati anaelekea kwake. maanake isije ikawa ni alibi ya kutaka huruma ya watu. lazima hii taarifa tuipokee kwa tahadhari kubwa. la mwisho kwani Bashe yeye mbaya wake si mmoja tuu na anamfahamu na alikwishamtaja kule Dodoma labda angempigia simu na kumuuliza vipi mzee.
Hili nami nililifikiri kwamba angewapigia watu wa karibu hata polisi waende pale kwake waweke mtego kuona ambacho kingefuata. pengine wangemfata njiani na kutress hayo magari wakati akiendesha taratibu.
 
Bashe wewe na Boss wako Rostam si ndio mnawapangia waandishi au wahariri waandike nini!!Kama juzi badala ya kudeal na issue ambayo iko bado mbichi mnabadilisha na kuleta vitu vya kupikwa ati Zitto Zuberi Kabwe alitakiwa afe sasa naona inakula kwako kaka sasa unalo basi nakuomba sana kwa kuwa hii ndio iko new issue basi usiandike leta zile za zamani hii yako ipotezee.Acheni unafiki jamani andikeni isue ambazo ziko openly na sio kama ile ati Zito alitaka kupewa sumu hii ni kuwapoteza wananchi andikeni issue kama za kutekwa kwa DR Ulimboko,Kibanda,Kuuwawa kwa Viongozi wa kidini,matokeo mabaya ya kidato cha nne,kuchomwa kwa makanisa yaani andikeni kila siku tena kwa ukurasa wa kwanza then wale wote wenye nia mbaya nafsi itawasuta na kumrudia Mungu na kuacha kuwawinda.
 
JUMAMOSI, MACHI 30, 2013 01:07 NA MWANDISHI WETU, DAR

WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa.

Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

“Wakati niko Mbezi jirani na njia panda ya kwenda kwangu, gari moja lilinipita kwa kasi na kuendelea mbele.

“Unajua kuelekea kwangu pale kuna barabara kama tatu ambazo zote unaweza kuzitumia na zikakufikisha hadi nyumbani kwangu,” alisema Bashe na kuongeza:

“Nilichokifanya nilipita barabara ya kwanza na wao wakapita barabara ya pili na ghafla nilikutana nao uso kwa uso, wakati huo naelekea kwangu na kibaya zaidi, gari lao walizima taa kubwa na kuacha ndogo.

“Walivyona gari langu, walinipiga taa kuashiria wanakata kona, lakini cha ajabu walinifuata nyuma na hapo nikaanza kujua sasa nafuatiliwa.

“Nilichokifanya sikwenda nyumbani moja kwa moja, bali niliamua kupaki gari kwenye grosari moja iliyoko jirani na kwangu.

“Baadaye niliamua kuondoka ili niwazunguke kwa nyuma nisome namba za gari lao, lakini sikufanikiwa kwa sababu taa za nyuma zilikuwa zimezimwa,” alisema Bashe.

Kwa mujibu wa Bashe, baadaye aliingia nyumbani kwake na kuwakuta wageni ambao alikaa nao hadi saa sita usiku baada ya kuwasimulia tukio lilivyokuwa.

“Sasa basi, wakati jamaa zangu hao wanaondoka kurudi kwao, walikuta lile gari pale pale njiani, wakanipigia simu, kwamba lile gari nililowasimulia linawafuatilia.

“Nikawaambia wageuze gari lao ili wasome namba, lakini hawakufanikiwa hata kidogo kwa sababu wale jamaa walishtuka na kuamua kutimua.

“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda pale Polisi Kawe na kutoa taarifa ambapo nilipewa RB yenye namba KW/RB/2899/2013,” alisema.

Machi 6, mwaka huu, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika.

Katika tukio hilo, Kibanda alitobolewa jicho la kushoto, alipigwa kichwani na kitu chenye ncha kali na kunyofolewa kucha. Kwa sasa yuko nchini Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu

Worst scripted comedy ever
 
Huyu Bashe ni mzushi wa daraja la kwanza. Ukiangalia mwenendo wa gazeti la Mtanzania ni kama wanajaribu ku-divert attention yetu kwenye matishio ya kweli yanayowakabili WATANZANIA (na sio watu wenye uraia wenye utata, anyway). Mara ya kwanza, Bashe alidai kuna siku yeye na Kibanda walifuatiliwa na polisi, lakini habari hiyo haikuchapishwa hadi Kibanda alipotekwa na kuteswa. Why? Kisha akadai eti amara kadhaa amekuwa akiona magari ya polisi yakiwa katika mkao wa kumfuatilia. Hayo yote hayajawahi kuandikwa katika gazeti analoongoza. Sasa amekuja na episode nyingine ya kunusurika kutekwa!

Huyu mhuni wa kisiasa (political thug) anastahili kupuuzwa tu. Yeye ni mouthpiece ya Rostam, fisadi mkubwa katika historia ya nchi yetu. Na naomba nisimung'unye maneno: I will go to a pub nikisikia mmoja wa majambazi wanaoibaka nchi yetu kila kukicha (au wapambe wao) aking'olewa kucha, jicho au meno. Wakati mwingine haki inapatikana hapahapa duniani, hata kama si kwa njia za kistaarabu.

Let's just ignore this political conman
 
Kwa foleni za dar ,kutoka mwenge mpaka njia panda ya kawe hivi alishindwa hata kuomba msaada hapo lugalo jeshini?
 
Back
Top Bottom