Bash La Mwaka NYC: Wakulu Tukutane Huko

Pengine ni muhimu kuimarisha ulinzi siku ya BASH....maana kama tangazo la mwaliko tu lishazua mshikemshike,sijui siku ya shughuli yenyewe itakuwaje......Just hinking aloud
 
Pengine ni muhimu kuimarisha ulinzi siku ya BASH....maana kama tangazo la mwaliko tu lishazua mshikemshike,sijui siku ya shughuli yenyewe itakuwaje......Just hinking aloud

- Mkuu wangu hii sio sherehe ya kwanza kufanyika, internent ndio imesadia sana kuwajua chui waliovaa ngozi ya kondoo, otherwise hakuna asiyewafahamu Police wa NY na wapo wengi sana pale Park itakapofanyikia, karibu sana mkuu labda lingine lakini sio la usalama, kwanza hao filimbi filimbi hakuna mpiganaji hata mmoja utawaona wamelowa kelele ni huku Internent tu.

Ahsante.

William
 
Waswahili bwana. Mtu una piga kelele uta fikiria ume lazimishwa kwenda kwenye hiyo sherehe. Kama shida ni details kasha sema zitaongezwa. Na nilivyoona mimi hii ni notification of invitation. Kama maelezo hayaja kutosheleza si umtuie pm W.J. akupe details zaidi? Sherehe siyo yako na hata usipo enda haki pungui kitu ila una lalamika uta dhani wame request ugharamie sherehe.
 

Heheheheheee mabingwa wa kombe la ndama hao....
 
Asante sana William kwa mwaliko. Ni wakati muafaka huu wa kukutana na watanzania wenzetu na kubadilisha mawazo.
 
wakati mwingine tuna matatizo. Mwaliko umetolewa kwa maneno ya kiungwana kabisa lakini mtu mwingine anataka ligi! Kama kuna kitu hakijaeleweka wasiliana na mtoa habari na muulize kiungwana akueleweshe; lakini hapana! the "gotcha" mentality! Unasoma kitu badala ya kujaribu kuelewa unaanza kujiuliza wapi amekosea nimuoneshe nimeona.

Kama hiyo tafrija mtu hutaki kwenda hata kukosoa ni kuchezea watu akili tu. Kama unataka kujua unamuuliza mtoa hoja akupe maelezo zaidi na kama kuna kitu anataka kusahihisha atasahihisha, huo unaitwa uungwana. Lakini kuna watu ile chembe ya uungwana haipo tena wao ni ubishi, kupinga, kukomoa, kuumbua n.k

Well... tuombeane uzima tu.. ningependa sana kuja Big Apple, sijawahi kufika huko na mimi naondoe ushamba ushamba wa kijijini.
 

Sasa hii ndo nini kama sio mwendelezo, bwa ha ha ha ha ha ha haa
 

Mwanafalsafa you always talk sense, keep it up bro.
 

- Mkuu unakaribishwa sana na hii shughuli itakuwa saafi sana yaani wananchi wengi wa miji mbali mbali kuweza kukutana na kubadilishana mawazo na ku-socialize kwa pamoja kama ndugu, ni mambo kama haya ndio huwa yanatutofautisha wa-Tanzania na watu wa nchi zingine, binafsi I will be more than happy to have you there,

Ahsante.

William.
 



Kaaa yaani tena NY?? Willy hebu fanya basi mgharimie mwana JF mmoja toka Tz awakilishe?? Najiteua mimi. Wadau mnasemaje???

Na sisi wana JF wa Tz tutakuwa na kujirusha lini??? Au tunaogopa mbwa wa Kova??? Naitamani siku hiyo nitakapomwona live wewe, yule, wale, nk. kwa nia njema tu. Tatizo ni kwamba hatuwezi kuchuja dedicated na vibaraka kwenye hilo libeneneke!!! Watakuja kusoma namba zetu za magari au kutafuta namba za taxi tutakazopanda halafu watufuatilie!!! Thubutu siku hiyo nitabadili njia na taxi kama kumi nitabadili vituoni!!! Tehe tehe!!
 


"Mguu Pande...Mguu Sawa!!!!. Paukwa Pakawa, katokea .......kijino kama kijiti.....kajenga nyumba kaakaaa....."
 

Mkuu maane heshima mbele sana bro, uliloongea ni la maana sana ila pia kwa hilo angalizo, hawa jamaa naona base yao ipo hapa hapa DSM, sasa kwa vile wako hapa watajivisha ngozi ya kondoo kisha waje waanze upekenuzi wao, si unajua hata kama sio kukusumbua kwa JF watafatilia kabiashara kako ka mtumba, ili mradi ukose 500 ya cafe kurusha mawe,,au sio mkuu!

Sijui wengine wanaonaje lakini binafsi nipo ukurasa mmoja na wewe (nikiazima maneno ya mzee FMES) kwa hili, haja ipo ila usalama wetu ndo wa kutilia mashaka!
 
- Heshima kwa wakuu wote JF, naomba kuweka tena uptodates ya the bash, ni kwamba jana tulikuwa na kikao muhimu sana cha the crew, yaani watayarishaji wa hii bash na kuusiliba msingi wa yote tutakayoyafanya kuhusiana na hii shughuli:-

1. The bash itakuwa tarehe 27, June 2009 kuanzia saa Saba mchana, itafanyika huko Wilson Woods Park, Mt Vernon New York. Hapo Park kutakuwa na kuchoma nyama, vinywaji na muziki hivi vyote vitagharamiwa na sisi watayarishaji. Na ni mwaliko wa wazi kwa yeyote yule anayejisikia kuja kushiriki nasi.

- Naomba hapa nitoe shukrani zangu nzito sana kwa wale wote ambao tayari wamejitolea kwa hali na mali kutuunga mkono toka nilipotoa tangazo la kwanza, ninasema misaada yenu tumeipokea kwa mikono miwili na Mungu awazidishie, na hata hiyo siku kwa yeyote anayejisikia kuja amebeba chochote kwa nia ya consideration for the others, pia inakubaliwa na tutashukuru sana kwa moyo huo wa upendo na kuwajali zaidi wananchi wengine.

2. Shughuli hii ya Kuchoma nyama, itaisha rasmi saa moja usiku, kwa maana ya kwamba Saa Moja usiku, tutaanza rasmi kuanua vifaa vyote vitakavyotumika kwa ajili ya the bash, wanaotaka kuendelea kuwepo hapo zaidi ni ruhusa pia yaani baada ya saa moja usiku.

3. Baada ya kumalizika hapo Park, shughuli sasa zitahamia kwenye ukumbi wa Alamo Club, Mt Vernon, New York mwendo kama wa dakika tano tu kutoka hapo Park, huko kutakuwa na Muziki rasmi wa Disco lililotayarishwa na watayarishaji wa hii bash, utakaopigwa na Ma-DJ wawili maarufu sana na hakutakuwa na kiingilio mlangoni, muziki utaisha asubuhi ya tarehe 28, June 2009.

- Naomba kurudia tena ni kwamba kiingilio kitakuwa ni bure, na ninajaribu kutafuta details zote za directions, namna ya kufika sehemu zote hizi mbili na soon nikiwa nazo nitazitoa wazi kwa kila mtu.

4. Hii bash, kwanza ni kwa ajili ya kuwaaga ndugu zetu familia mbili ambao wameamua kurudi nyumbani moja kwa moja, na pia kusherekea siku ya kuzaliwa kwa baadhi members wa Community ya Wa-Tanzania New York na pia ni njia ya watayarishaji wa the bash, ambao tumekua tukishirikiana sana kwa hali na mali na kwa muda mrefu sana kutoa nafasi ya kujumuika na kubadilishana mawazo ya maendeleo binafsi na ya taifa letu na wananchi wengine wa nje na ndani ya New York, na cha msingi zaidi ni kufahamiana, maana dunia ni watu.

5. Mpaka sasa dalili zinaonyesha kwamba hali ya hewa itakuwa ni nzuri tena sana, lakini ninasema hivi no matter what of the wheather tulipofikia sasa hatuangalii nyuma, the bash itafanyika kama tulivyopanga, tayari tumejitayarisha na a back up plan. Na pia kwa sababu ninazo e-mails za wananchi wengi sana, ambao huenda sio members hapa, nitawatumia ujumbe huu kwa njia hiyo.

- Samahani kwa ujumbe mrefu, lakini I promise kwamba it won't happen again, lakini nilifikiri ni muhimu hapa kuweka msingi na kila kitu wazi, kama kuna mengine muhimu zaidi tutaendelea kuhabarishana as the days goes by kukaribia na the day.

Kwa niaba ya watayarishaji wote wa hii bash, ninaomba kuwakaribisha ndugu wananchi wote wenye uwezo wa kufika, pia niwakumbushe tu kwamba mabasi na treni yapo yanayopita karibu na hiyo sehemu ya shughuli.

Ahsanteni.

William.
 
Last edited:


Mkuu ni nani huyu mnamuaga. I am in NY too.
 
- Kuna habari za waliotutukana sana na habari za hii bash huko mwanzoni, sasa tunawasikia wakiwatafuta watayarishaji wenzangu ili wachangie kwa siri, hizo ni very encouraging news, karibuni sana wote tujumuike tu.

Ahsante.

William.
 
Haya mambo na utaratibu mzima yanaonekana yatakuwa bab kubwa.

Mimi nawatakia kila la kheri katika hafla hio.
 
Haya mambo na utaratibu mzima yanaonekana yatakuwa bab kubwa.

Mimi nawatakia kila la kheri katika hafla hio.

- Mkulu Richard, tupo pamoja sana shughuli itafanyika, ingawa tayari kuna maneno mengi sana kama kawaida yetu wabongo, ninawakumbusha wale wote mnaosema sema huko pembeni ni kwamba tunawasikia sana, kama mna maswali ni bora kutuuliza tunaohusika, badala ya kuwauliza wasiohusika na in the process kutaka kutuletea confusion kama mnavyojaribu kufanya so far huo sio uungwana, usiende kusema sema maneno mengi ya majungu huko pembeni kuhusu shuguli ambayo huijui mwanzo wala mwisho wake halafu yanaishia kuturudia and then what? Aibuu kwa mtumzima!

- Tumetuma e-mails na namba za simu tumeweka za wote tunaohusika, piga simu uliza maswali yako tutakusaidia, so far hakuna mwanamama yoyote aliyetajwa kuhusishwa na utayarishaji wa hii shughuli, sasa tusiingize wake za watu na yoyote yule ambaye hajatajwa kuhusika na utayarishaji wala kuagwa! Sasa wewe uliyewarukia kina mama hao na maneno mengi kama kasuku aliyekutuma ni nani hasa?

Na yes ni open cookout kwa wote wanaoweza kufika, sio tu wateule flani, looking forward to see you all there! Mwenye maswali check your e-mail unaweza kumpigia yoyote kati yetu watayarishaji kila kitu kimewekwa wazi, wabongo tupunguze maneno maneno.

Ahsante.

William.
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…