Kosa la Michael Jackson kugombana na waliomuweka mjini

Kosa la Michael Jackson kugombana na waliomuweka mjini

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
985
Reaction score
2,387
Mwezi Agosti mwaka 1985, mfalme wa Pop, Michael Jackson, alicheza karata ya kibiashara iliyowashtua na kuwakasirisha mabosi wote wa makampuni makubwa ya muziki duniani.

Alinunua hati miliki za nyimbo zote za bendi maarufu zaidi duniani, The Beatles (pamoja na nyimbo za Elvis Presley na maelfu ya wasanii wengine), kwa kitita cha Dola Milioni 47.5!

Kitu ambacho makampuni ya muziki hayakutarajia ni kwamba, kijana mweusi aliyetoka kwenye umaskini wa mtaani Gary, Indiana, angekuwa na akili ya kibiashara ya kumiliki haki za nyimbo za magwiji wakubwa zaidi wa muziki wa Kizungu.

Mwaka 1995, kampuni ya Sony ilipogundua kuwa Michael Jackson alikuwa anashikilia utajiri mkubwa zaidi wa hakimiliki za muziki duniani, walilazimika kuungana naye na kuunda kampuni ya Sony/ATV.

Kupitia mkataba huo, Michael Jackson alikuwa anamiliki 50% ya catalog yote ya Sony/ATV!

Kila mara wimbo wa Beatles, Elvis, au msanii yeyote mkubwa ulipopigwa kwenye redio, filamu, au matangazo duniani, mabilioni ya fedha yaliingia moja kwa moja kwenye akaunti ya Michael Jackson.

Hapa ndipo vita ya hatari ilipoanzia. Katika ulimwengu wa biashara wa Marekani, msanii mweusi kuwa na nguvu ya kudhibiti utajiri wa mabosi waliomtawala ilikuwa hatua iliyoleta shinikizo kubwa kwenye sekta hiyo.

Siku zilivyozidi kwenda, tofauti kati ya Michael Jackson na uongozi wa juu wa Sony Music zilihamia kwenye mwanga wa wazi:

Kuharibu Albamu: Jackson aliituhumu Sony kwa kupunguza matangazo (promo) ya albamu yake ya Invincible (2001) ili aingie kwenye changamoto za kifedha na alazimike kuwauzia 50% ya hisa zake za Sony/ATV kwa bei ya chini.

Hotuba ya Harlem (2002): Michael Jackson alisimama jukwaani na kutoa kauli nzito kuhusu biashara hiyo: "Makampuni ya muziki yanawanyonya wasanii, yanawafanya wamalize kazi zao wakiwa hawana kitu... Mfumo huu una ushindani usio wa haki unaotaka kuniharibu."

Mara tu baada ya kuanza kuwapiga vita waziwazi mabosi hawa wa miamba ya biashara, baadhi ya vyombo vya habari vilianza kuangazia zaidi maisha yake binafsi na kuleta taswira tofauti kwa jamii.

Mwezi Juni 2009—siku chache kabla ya kuanza ziara yake ya kurejea jukwaani (This Is It) ambapo alikuwa amepanga kumaliza masuala yake ya kifedha—Michael Jackson alipoteza maisha ghafla nyumbani kwake kutokana na changamoto za matumizi ya dawa za Propofol, aliyopewa na daktari wake Conrad Murray.

Daktari wake Conrad Murray alipatikana na hatia ya uzembe wa kimatibabu, lakini familia na mashabiki wengi waliona kulikuwa na mkono wa watu wakubwa juu ya hili.

Binti yake, Paris Jackson, pamoja na wanafamilia wengine wamekuwa wakieleza kuwa Michael Jackson alihisi maisha yake yamo hatarini. Mara kadhaa kabla ya kuondoka kwake alionyesha wasiwasi mkubwa akisema: "Kuna shinikizo kubwa dhidi yangu kwa sababu ya catalog yangu ya muziki."

FB_IMG_1789149409608.jpg
 
Kwanini hawakummaliza akiwa kwenye peak hadi wamvizie uzeeni huku?
 
Back
Top Bottom