Bash La Mwaka NYC: Wakulu Tukutane Huko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bash La Mwaka NYC: Wakulu Tukutane Huko

Discussion in 'Matangazo madogo' started by W. J. Malecela, Jun 2, 2009.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu wote JF, salaaam kwa wote ninaomba kuwafahamisha kwamba kwa kushirikiana na wananchi wengine kama kumi hivi, tunatayarisha bash kabambe la mwaka litakalo fanyika huko NYC, kwa maajaliwa ya Mungu itakuwa tarehe 27, June 2009.

  - Shughuli zitaanza Saa Saba mchana kwa kuchoma nyama, vinywaji baridi, na muziki mzito sana mpaka Saa Mbili Usiku, katika Park moja maarufu sana pale NYC yaani Wilson Woods, Westchester, dakika kama 15 kutoka Manhattan, halafu usiku kutakuwa na Muziki wa Disco utakaoanza Saa Nne mpaka asubuhi ya tarehe 28, June 2009 katika ukumbi maarufu sana wa Alamo ambao uko hapo hapo karibu sana na hii Park zitakapoanzia hizi shughuli.

  - Kimsingi ni Bash la kumuaga mshikaji wetu mmoja, nimeamua tu kuwapa hints mapema ili wale wa mbali tuanze kujitayarisha mapema, badala ya kuwashitukiza dakika za mwisho, na baadaye nitawafahamisha details zote muhimu mipango itakapokamilika ambayo kwa sasa bado iko kwenye duru za awali, lakini ninawaahidi wale wote wenye nia ya kufika huko kwamba kama kawaida yangu sitawaangusha tutaondoka wote tukiwa tumeridhika, tuombe Mungu tu hali ya hewa iwe kama ilivyo sasa, ninaamini kwamba itakuwa isipokuwa basi tutafahamishana any mabadiliko.

  - Kwa niaba ya wenzangu wote tunaohusika, ninawakaribisha ndugu zangu wote wa JF na wengine wote kufika huko, hatuhitaji mchango isipokuwa tunaamini kwamba utakuwa considerate na kutokuja mikono mitupu siku ya siku itakapofika.

  Ahsanteni Sana.

  Wenu

  William Malecela.
   
  Last edited: Jun 29, 2009
 2. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  William, pata uhakika wa tarehe ya tukio ndio ualike watu, sio mambo ya kiswahili ya ``panapo maajaliwa``

  Mtaje huyo tunaekuja kumuaga. Isitoshe, bash la kuaga mshikaji mmoja sio "la mwaka" la kualika nchi nzima.

  Again, William, kama tarehe ya bash wewe mwenyewe huijui, hii haiwezi kuwa notice in advance ya uhakika.
  Okay, kwa hiyo tusitume michango in advance lakini unaomba tubebe nyama mbichi tutachoma hapo hapo, ok.
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  3. na baadaye nitawafahamisha details zote muhimu mipango itakapokamilika ambayo kwa sasa bado iko kwenye duru za awali,

  - Mkuu Dilunga, kwani kilichoandikwa sio kiswahili hapo mkuu? Haya yako yote umeyatoa wapi? kweli akili ni mali na ni nywele kila mmoja ana zake, mbona hujamaliza uchunguzi wa ajali ya Mwakyembe kwanza tayari unarukia uchunguzi mwingine?

  - Sherehe yoyote inayofanyikwa nje haiwezi kusemwa kwa uhakika kwa sababu inategemea na utabiri wa wataalam wa hali ya hewa ikiwa mbaya somo linabadilika, na anayeagwa kama hapendi jina lake liwekwe humu then what unafikiri kila mwananchi anapenda kutajwa humu kama wewe?

  Hivi hapo juu haijaandikwa tarehe 27, june 2009 mkuu kweli unaona sawa sawa? uhakika wa vipi na bado kuthibitisha hali ya hewa kwanza vipi mkuu are you okay au?

  - ni wapi zimetajwa nyama na kwamba lazima ziwe mbichi , jamani kweli ukishangaa ya musa utaona ya firauni, sasa hii yako mkuu unaita nini critic au Ze-Comedy? Jifunze kuwa na subira, huko US kuna wananchi wanaofanya kazi, wanaosoma kufahamishwa mapema kunaweza kusaidia kuwapa nafasi kujitayarisha kwa kuomba likizo, ruhusa makazini, kubadili ratiba za kazi na masomo, mkuu jaribu kuwa considarate na wengine badala ya kuiona dunia ndani ya box lako tu peke yako, angalia na nje ya box lako mkuu!

  Respect.

  FMEs!

   
 4. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mtu hawezi kupanga mipango ya mahudhurio based on mwaliko wa panapo ``maajaliwa.`` Apange fixed date.

  Kama hataki kutajwa basi asipende kufanyiwa fanyiwa pati za kuagwa na watu wasiomjua.

  Inawezekana ni terror suspect amepigwa palanja la kurudi kwao na sasa anafanyiwa pati na sympathizers wake wanaoalika halaiki ya strangers kama public support ploy. Huwezi kuitisha pati ya kuaga mtu asiyejulikana.

  Amedai ni "nyama choma" na tusije "mikono mitupu." Sasa anaomba tuje na nyama mbichi, au?

  Na yeye William avute subira mpaka apate uhakika ndio aalike. Hawezi kutoa early notice halafu akasema tusubiri details!
  ``Huko U.S.``? Kwani wewe uko wapi? Kama wewe hauko huko, sherehe za mbali wewe zinakuhusu nini?

  Na kufanya kazi ni sehemu yeyote ile duniani. Sio ``huko US.`` Huyo William apate kwanza uhakika zaidi ya shughuli za Kiswahili za ``maajaliwa.`` Mialiko ya ki-biriani za vichoroni imepitwa na wakati.
   
 5. i

  isdory Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazee vipi huko Ikulu ya Dodoma kuna nini? mbona kimya nasikia kideo cha mzee kimebebwa na vibaka
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Ni wivu na chuki kwa sababu hujashirikishwa na unatakiwa uende kama wananchi wengine, sasa usiharibu sherehe ya watu kama wakati ule wa sherehe ya Mama Migiro ukajaribu sana kuiharibu lakini ukakwama nasikia ukaingia kwenye sherehe na mapovu ya hasira mwili mzima, huku watu wanabonyezana na vicheko, acha mkuu watu walishakushitukia zamani sana na matatizo ya wivu na chuki,

  - Subiri utapewa taarifa kamili, acha hizi longo longo haziwezi kuharibu sherehe kama unavyotegemea, itafanyika kama zile zingine zilizofanyika huku ukipigana sana kuziharibu, pole sana mkuu lakini nasikia matayarisho yanaendelea kama kawa, ninaapa kwa chuki ulizonazo hii shughuli huwezi kwenda, halafu pia kuna watu kule unawaogopa kukutana nao uso kwa uso kwa sababu ya matatizo yako ya chuki na wivu, sasa wamekugundua,

  - Utabakia hivyo hivyo anti-social na kuchukia watu bila sababu kumbe tatizo ni wewe mwenyewe na mawivu na machuki ya kijinga, hata ulete mtoto mdogo hapa atanga'amua kua una matatizo flani hivi yanahitaji dawa, umeanzisha chama kikafa puh! chini kisa watu hawakukuamini kwamba you are for real, sasa waachie wanaominiwa na wananchi huwezi lazimisha uongozi kwa nguvu mkuu, sasa kaa pembeni uongozwe tena na uliowakuta ukaenda macho juu sasa tizama ulipoangukia maana kama haupo vile!

  - Sherehe ipo na itafanyika kama kawa kaa pembeni utapewa news, mahali nilipo haihusu kitu hii ni Global mkuu, tunajua na kushirki anywhere at anytime, tumeshiriki Busanda itakuwa NYC sasa usilete ya location maana hayahusu, jikasirkie mwenyewe kwa kuwekwa pembeni na wananchi usilaumu watu hapa na visingizio chunguzima mpaka unadikiri kusema maneno ya nyama mbichi, eti kutokuja mikono mitupu maana yake ni kuja na nyama mbichi, pole sana mkuu halafu unazidi kujiabisha tu na kuwahakikishia wanaokuweka pembeni kwamba hawakosei,

  - Yako huwa ninaiita the greatest melt down, ulianza kama msomi na mchambuaji makini na siku hizi umeishia kuwa mdundiko unitue na unikome halafu unajisema mwenyewe kuwa vichochoroni na biriani type, sisi tutakwenda na tutakuletea salam, kwenda huwezi maana utaishia kuzomewa tu, Bwa! ha! ha! ha! na nasikia wakulu wa taifa na international commuinity watakuwepo kama kawa, sasa suka au unyoe ila mtuzima ni aibu kuwa anti-social kwa sababu tu wananchi hawakutaki kuwaongoza!

  Respect.

  FMES!
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mtoto wa kiume anasema "unitue na unikome"? Astaghfirullah!
   
  Last edited: Jun 2, 2009
 8. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hapo una maana gani?
   
 9. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Mkuu hapo juu samahani sana kama nimekukwaza na hizo info nilizozitoa ambazo bado hazijakamilika, ukweli ni kwamba tunaoshirikiana katika matayarisho toka majuzi tumekua tukiwaarifu wananchi karibu wote walioko US, na hata nje kuhusu matayarisho haya, nia na madhumuni ni kuwapa nafasi wananchi wanaopenda kuja kushiriki nafasi ya kujipanga mapema kama vile ilivyokuwa kwenye sherehe ya kumuaga Balozi Chagula, Blalozi Mwakawago, kumuaga rais Mkapa, Kumpongeza Mzee Malecela kwa kuoa, kumkaribisha Mama Migiro njia iliyotumika ni hii hii ya kufahamishana mapema na baadye kupeana all the details, lakini cha muhimu ni kwamba itafanyika,

  - Ingawa pia kuna tofauti moja ya hii sherehe kwamba itaanzia kwenye cookout, yaani nje maana zile zingine zote zilifanyika ndani mwanzo mpaka mwisho, tunahitaji wiki mbili kabla kupata uhakika wa 85%, kwamba hali ya hewa itakuwa muswanu hiyo siku au tutabadili tarehe, otherwise matayarisho yanaendelea kwa nguvu moja na ushirikiano wa hali ya juu sana baina yetu wananchi, punguza jazba maana hii ni socialization tu baina yetu wananchi badala ya kuisubiri serikali kutufanyia tunaweza kuji-organize na kufanya wenyewe,

  - Hayo ya kupeleka nyama mbichi sijawahi kuyasikia hata siku moja, kwamba mtu akikualika kwenye cookout basi anategemea uende na nyama mbichi hayo ni mageni sana kwangu, nijuavyo watu huenda na vinywaji, vyakula vya aina mbali mbali, wengine huamua kuepeleka keki, lakini eti unategemewa kupeleka nyama mbichi au kule kwenye sherehe kuna anayesubiri upeleke nyama mbichi hayo mbona makubwa sana na ni ukuzaji wa mambo wa hali ya juu sana you must be an expert wa kutunga majungu mkuu, maana this is over the board and unheard off duh! Yaani ile shughuli ya cookout ya Columbus watu waliambiwa kwenda na nyama mbichi, I am lost na this!

  Otherwise, kama upo hayo maeneo unakaribishwa sana, na wala usihangaike na kubeba nyama mbichi, labda huenda una experience flani ya kualikwa na kutegemwa kupeleka nyama mbichi, ninarudia tena kwamba not this one feel free kama una mpango wa kuja, na ukifika pale Wilson Woods nitafute kama unahitaji msaada nitakuwepo siku hiyo kuanzia asubuhi mpaka asubuhi tena shughuli zitakapokwisha kama zitafanyika siku hiyo kama zilivyopangwa, na wananchi wengi na viongozi wengi tayari wamethibitisha kuhudhuria hizi shughuli kama tulivyowatangazia.

  - Na mwishoni mwa wiki hii nitakuwa na matokeo ya wataalam wa hali ya hewa na nitathibitisha kuwepo hiyo siku yaani tarehe 27, June 2009 kuanzia mchana saa saba mpaka asubuhi ya tarehe 28, June 2009.

  Again samahani sana kama nimekukwaza, pole sana mkuu maana sio rahisi mtu kuandiak wka hasira kama ulivyoanza bila ya kukwazika, tusameheane ndugu yangu.

  Ahsante.

  William.
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Hapo una maana gani?

  - Kelele za mlango sherehe ipo kama ilivyopangwa, ni suala la uamuzi kusuka au kunyoa!

  Respect.

  FMES!
   
 11. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Bwa ha ha ha ha ha ha haaaaa, comedy, bwa ha ha ha ha ha ha aaa, I love JF.
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Huu ni ukumbi wa matangazo madogo madogo, ya Ikulu yapo kule kwenye siasa, au mtandao wako hauonyeshi sehemu ya siasa mkuu?

  Respect.

  FMEs!
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nasikia mi kamera kibao imeandaliwa, ova Mafia funeral fulani hivi if you catch my drift.
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkulu Bluray, ukiona mke wa mtu analiwa na mtu mwingine halafu yule anayeliwa mke anajikomba kwa anayemla mkewe, maana yake nini mkuu wangu kama sio hiyo astaghfilruah!

  - Ulifikiri ni siri au ulidhani kwamba kwa jina hili uko safe sana! unai-underestimate JF, Bwa! ha! ha! ha! karibu mkuu wangu sasa nimevua gloves maana ni muda mrefu sana sasa nimekua nikikupa heshima ya bure kwa ID hii yako, sasa karibu sana mkuu!

  Respect.

  FMEs!
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  Duh..saa nyingine huwa napata burudani kusoma tu hoja zinapotolewa hapa...uelewa wangu huu ni mwaliko, na sio hoja..wanaweza kufika waseme, wasioweza kama mimi tunaomba udhuru na kuwatakia shughuli njema!
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Ahsante Mkuu Kaizer na tupo pamoja sana hapo!

  FMEs!
   
 17. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Thread ya mwaliko wa nyama choma itafungwa.... (wa)mhusika mwenyewe kajaa matusi... hahahahahahaaa

  Haa hahahahahaaaaa

  Ulipokuja kama Wiliiam umeanza taratiiiib, kwa upole, halafu ghafla the true colors zikakurupuka toka ndani ya ngozi ya ustaarabu...hahahhahaaha... I got hand it to you William, kwa usanii.

  Mfano wako wa pati ya Ohio ni tofauti, wageni wa Ohio hawabebeshwi nyama mbichi kwa sababu wanakuwa wameshapitisha donee in advance na hela yao imeshanunua nyama.

  Wewe unasema tusichangie lakini tusije mikono mitupu kwenye nyama choma. Tuje tumebeba vi hotdog vibichi?
   
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  Jun 3, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Ndugu Kaizer ubarikiwe sana huu wako ni mfano wa kuigwa, yaani ustaarabu wa hali ya juu sana.

  Ahsante sana.

  William.
   
 19. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Naomba tuendelee kupeana updates kaka. (Itabidi nije huko)
   
 20. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #20
  Jun 3, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Hamna tatizo ndugu yangu, ukija itakuwa bomba sana maana madogo wote yaani the future leaders kama wewe watakuwepo.

  Ahsante tutaendelea kufahamishana.

  William.
   
Loading...