Basata mnasubiri nini kumchukulia hatua Ney wa mitego

Basata mnasubiri nini kumchukulia hatua Ney wa mitego

Nimeusikiliza huo wimbo kiukweli hauna adabu hata kidogo
Nadhani bado hamjaelewa mwelekeo tulionao sasa
Ney alichokifanya ni utovu wa nidhamu kwa viongozi wetu na ipo haja kwa basata kutoa onyo kwa huyu kijana vinginevyo wataibuka wasanii wengine na nyimbo za aina hii na huenda ikaleta taswira mbaya kwa nchi
 
Nani a forward wakati tunaupakua wenyewe tu na kila mtu anajiburudisha kwa ubunifu wa kijana. Mnapozidi kubana ndio ubunifu unaongezeka, juu tutaandika ''uzalendo kwanza'' ila ndani sasa tunajua wenyewe.
Na mimi nasema wapoooooo

Hapa kwetu Shinyanga leo nilikuwa napita mitaani na kushuhudia zaidi ya sub - woofer 20 ktk nyumba za watu na saluni [barber shops] zikipiga huo wimbo huku vijana wa umri kati miaka 7 - 25 wakiigiza chorus yake !!

Ama kweli teknolojia imekua sana jambo lolote laweza kusambaa na kuenea haraka na muda mfupi sana kama moto ktk misitu ya Calfonia !!
 
Mtoto mdogo mshirikina,acha hayo mambo huko kwenu wazee ndo wanahayo mambo.
 
Hahaa sasa kumbe wimbo upo mtandaoni?

Nyie si mmesema hamfanyii kazi udaku wa mtandaoni?
 
Ccm saiv wanadeka wanafanya fyongo ukisema tu walicchofanya eti "uchochezi" hivi nani mchochezi kati ya mfanyanyaji ma msemaji?
Hahahaahah yani umenichekesha ulivyosema ccm saiv wanadeka duuh si wanababa yao asiyeshindwa kamweeh
 
Kama walishindwa kuufungia ule pale Kati patam ambao ulikua na sifa zote za kuufungia huu unastaili uendelee kupigwa Kwan ngoma tam sana afu Imetoka kipindi kizuri yaani huyu atakua super sub
Nadhan waliipiga marufuku video bana ndo ilikuwa mbay hata kwa watoto
 
Mods mnasubiri nn msiifute hii post ya huyu ndugu yake bashite. Nyimbo ya maadili unaijua wee?

'Kuvamia ofisi za watu nayo ni kazi'
'Viongozi wasiotaka kushauriwa'
 
Hapa kwetu Shinyanga leo nilikuwa napita mitaani na kushuhudia zaidi ya sub - woofer 20 ktk nyumba za watu na saluni [barber shops] zikipiga huo wimbo huku vijana wa umri kati miaka 7 - 25 wakiigiza chorus yake !!

Ama kweli teknolojia imekua sana jambo lolote laweza kusambaa na kuenea haraka na muda mfupi sana kama moto ktk misitu ya Calfonia !!
Kwasasa kila mtu anao na hakuna kutumiana tena, yaani labda waje wakague redio zetu majumbani na kukamata simu zote ila bad haitasaidia kwani tushaanza kuumeza, yaani wakiuzima tutauimba wenyewe kwa sauti zetu wenyewe.
 
Basata au mtaka mtumbuliwe ninyi? Kuna hii nyimbo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyoimbwa na msanii Ney wa mitego inasikika ikiwakejeli viongozi mbalimbali. Maneno yaliyotumika ni Makali sana, najua imetoka weekend mtasema hamkuwa kazini basi Jumatatu mchukue hatua na kinyume na hapo hatua zitachukuliwa dhidi yenu
Kamuimba nani kwani mbona hajataja mtu
 
Basata au mtaka mtumbuliwe ninyi? Kuna hii nyimbo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyoimbwa na msanii Ney wa mitego inasikika ikiwakejeli viongozi mbalimbali. Maneno yaliyotumika ni Makali sana, najua imetoka weekend mtasema hamkuwa kazini basi Jumatatu mchukue hatua na kinyume na hapo hatua zitachukuliwa dhidi yenu

Marehem Dr Remmy miaka ile aliimba wimbo wa mambo kwa Socks kuhamasisha condom Basata na Serikali kwa ujumla wakaufungia wimbo ule, mpaka akili zilipokuja kuwakaa vizuri wakaanza kutembea na magari barabarani kuhamasisha Condom vile vile kama alivyokuwa ameimba Remmy

Kama kuna mtu kaimbwa na Nay wa Mitego, basi ni muda wa kujichunguza na kama kuna ukweli basi ajirekebishe
 
Basata au mtaka mtumbuliwe ninyi? Kuna hii nyimbo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyoimbwa na msanii Ney wa mitego inasikika ikiwakejeli viongozi mbalimbali. Maneno yaliyotumika ni Makali sana, najua imetoka weekend mtasema hamkuwa kazini basi Jumatatu mchukue hatua na kinyume na hapo hatua zitachukuliwa dhidi yenu
Nyimbo ni wingi, katoa ngap?? Halafu fasihi ina kazi ya kukosoa, kuonya, kukejeli n.k.... Kama unapenda fasihi kweli, ipende hata inapokera matakakwa yako au niseme matakwa yenu
 
The TrueBoy is in the Building Beibeee....,Nzagamba atulie kidogo.
 
Basata hawafanyi kazi kwa kusikiliza udaku hahahaa Tanzania eehhh nchi yangu naipenda.
 
Kuna viongozi wana maamuzi ya kiseeeee , wapooo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom