Basata mnasubiri nini kumchukulia hatua Ney wa mitego

Basata mnasubiri nini kumchukulia hatua Ney wa mitego

Nay miaka yote anaimba ukweli na uwazi. Alafu napenda sana kumsikiliza, usije ukanikwaza kwa uchochezi wako!!!!...nyimbo nzuri sana hii, watanzania tuache ushamba na uoga.....hajaimba matusi, ameimba kama watu wengine walivyosema kuhusu matukio hayo....kwahiyo hakuna jipya aliloliimba Nay. Kwasisi ambao hatupendi kusikiliza watu wakizungumza huwa tunaweka haka kanyimbo ka Nay tunasikiliza huku tukitingisha kamguu kamoja na kichwa kikinesa nesa mdogo mdogo!

NB: Makonda haitwi Bashite
 
Aliyoimba yana ukweli ama hayana? Kwanini wasibadilike hao walioimbwa? Kumfungia Nay hakubadili ukweli uliosemwa. Isitoshe serikali haifuatilii mambo ya mitandao
tena vijipost safi sana,kwanza tusipangiane vina na mizani
 
akina Bashite tanzania hii hawataisha ona mwingine hyu cjui kaandika nini hapa
 
Acha ubashite we ng'ombe....badala ya kuiambia a rikali ijenge viwanda na kuchululia hatua mafisadi wew unataka anayesema kweli ndo achukuliwe hatua...
STUPIDITY
 
Haiwezekani nyimbo za kumzodoa rais zapigwe ki horera hiyo!
Tutaanza kuforwadiana kwenye magroup wanatutafutie kesi bure!

Nimeusikiliza wimbo huo mwanzo mwisho tena zaidi ya mara nne sijakisikia chochote kilicho kibaya zaidi ya kwamba msanii ametumia ubunifu wake kutunga na kuimba wimbo juu ya jambo ambalo ni hot kwa wakati huu ktk jamii....

Inawezekana wengi wenu huko serikalini na mlio karibu na Rais wenu labda hamkusoma somo la fasihi ktk shule mlizosomea mkaelewa maana ya sanaa ya lugha na fasihi....

Kazi ya sanaa ya lugha [fasihi] ni kuelimisha, kuburudisha, kukosoa, kuelekeza nk kwa njia mbalimbali kama vile nyimbo [ music ], ushairi, ngoma, hadithi, tamithilia nk

Mwanafasihi yeyote ktk fani yoyote ya fasihi haamuki na kujikuta anatunga hadithi, wimbo iilimradi ni hadithi au wimbo tu, bali huangalia jamii ina tatizo na kuhitaji nini kwa wakati uliopo na ujao pasipo kusahau maudhui ya fasihi kama nilivyotangulia kuandika hapo juu.....

Sijaona tatizo lolote ktk wimbo wa Ney wa Mitego. Kilicho wazi ni kuwa kinachosikika ktk wimbo huo, kinaakisi matendo na uchafu wa baadhi ya viongozi wetu ktk jamii tunamoishi na kwao ukiwapa nafasi ya kutoa maoni juu ya wimbo huo, automatically watakuambia wimbo umejaa uchochezi na kumzodoa huyu au yule na especially Rais Magufuli....

Na ukiona maoni ya namna hii, tambua mara moja mwanafasihi Ney wa Mitego amefanikiwa kufikisha ujumbe aliokusudia ktk jamii !!!
 
Serikali haifanyii kazi mambo ya mitandaoni, OVER!
 
Duh chadema viroba vimekatazwa lakin ndio kama vimefunguliwa. Mkiungana ufipa mnaweza kutunga bonge la wimbo wa taarabu. Maana hapa Bavicha kule gwajima mnajua kuchamba sana. Wachaga siku hzi mmechukua nafasi ya wazaramo. Maana wazaramo wapo bize na maendeleo ya viwanda nyie mmebaki maneno tu mitandaoni. Kumbe mmeminywa kila mahala aisee kwenye serikal hampo kule mlipokuwa mnakwiba pesa TRA sa hiv mnapaona kama kituo cha polisi. Hapa kazi tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom