Wimbo "pale kati patamu" wa Ney wa mitego wafungiwa rasmi

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,847
2,000
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na msanii Ney wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ameeleza kuwa msanii huyo amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua sekta ya sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonyesho yenye kukiuka maadili.

“Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.”

Ameeleza ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.

“Ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Katipatamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.”
1468664308779.jpg


========

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na Msanii Ney wa Mitengo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.

Msanii huyu amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonesho yenye kukiuka maadili. Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.

ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati patamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.

Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni wasio na staha na wanaojipanga kuibomoa jamii.

BASATA linapenda kueleza ya kufuatayo
• BASATA linatamka kuwa limeufungia wimbo huu rasmi kutumika kwa namna yoyote ile.

• Aidha pamoja na adhabu ya kufungia wimbo huu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapotengeneza kazi zao.

SANAA NI KAZI, TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI.
 

makilo

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
1,697
2,000
Kuzifungia nyimbo zake zisichezwe redioni hakutoshi.inatakiwa na yeye Ney afungiwe hata vi miaka vi 5 tu nadhani atashika adabu japo kiduchu.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,535
2,000
Sorry to say this but BASATA have some loads of stupidity if not negligence on them
Hiki kitengo ndio kilitakiwa kiratibu kazi zote za wasanii kabla hazijazalishwa! Uwezo huo upo sasa inakuwaje wanasuburi kazi itoke isambae kwenye jamii ilete madhara ndio wao waje na blah blah za kuifungia? Huku si kutengeneza mazingira ya rushwa?
Sorry again to say this but I can sniff some stupidity on them
 

Ze Heby

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,651
2,000
Hii haina maana.Wimbo ushasambaa mitandaoni
Ilipaswa wamfungie hata miaka miwili asifanye shoo njaa impige ndio atajifunza
Shame on you BASATA
 

warumi

R I P
May 6, 2013
16,298
2,000
Jamani nyimbo ikifungiwa ndio nn? Kila siku wanafungiwa wanarudia madudu yale yale, cha muhimu wafungwe wao tu then mtaona kama wataendelea na huo upuuzi, huyo nay angewaweka dada zake makalio nje si anajifanya hamnazo, wanawachezea watoto wa watu kwa kuwapa vi mia mbili na nyie ma dada mbwa nyie nawarudia sasa hiv
 

dexterous

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
1,784
2,000
Sorry to say this but BASATA have some loads of stupidity if not negligence on them
Hiki kitengo ndio kilitakiwa kiratibu kazi zote za wasanii kabla hazijazalishwa! Uwezo huo upo sasa inakuwaje wanasuburi kazi itoke isambae kwenye jamii ilete madhara ndio wao waje na blah blah za kuifungia? Huku si kutengeneza mazingira ya rushwa?
Sorry again to say this but I can sniff some stupidity on them

Hata mimi nimefkiria hivyo mkuu kwann nyimbo ya msanii yoyote hapa bongo isipite kwanza kwao waipitie kisha ndo iruhusiwe kwenye ma blog n vituo vngne vya burudan....Yaan unafungia kwenye Redio wakati watu kwenye simu zao ipo
 

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
53,644
2,000
Jamani nyimbo ikifungiwa ndio nn? Kila siku wanafungiwa wanarudia madudu yale yale, cha muhimu wafungwe wao tu then mtaona kama wataendelea na huo upuuzi, huyo nay angewaweka dada zake makalio nje si anajifanya hamnazo, wanawachezea watoto wa watu kwa kuwapa vi mia mbili na nyie ma dada mbwa nyie nawarudia sasa hiv
Sio dada zake angeweka hata makalio yake
 

weed

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
2,125
2,000
...kwanza mbona kabadilisha jina lake Ney wa mitego,mana hilo jina na matendo yake ya kishamba ndo vinaendana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom