Mkuu wangu nadhani unashindwa kumsoma Zitto vizuri kwa sababu umeshindwa kufuatia utaratibu wa posho zenyewe. Zitto hakutaka posho hizo lakini ilikuwa lazima uchukue kama utaweka sahihi daftari la mahudhulio.. Fedha zinaingizwa direct ktk account yako, hivyo kwa ushauri wa mbali kwanza Zitto alitoa ombi la fedha hizo zipelekewe moja kwa moja ktk account ya NGo ya jimbo lake.Hebu tupe ufafanuzi kwa mambo yafuatayo.
Nadhani waliowengi wamekuelewa kutokana na ufafanuzi wako. Labda kwa kuongezea hapo nitoe pia maelezo kuwa hata Mh. Mbowe alishalitolea ufafanuzi jambo hili tena kwa umahiri mkubwa sana. Katika kumbukumbu zangu Mh. Mbowe alisema, Swala si kufuta POSHO zipo zilizohalali kama Per DieM lakini siyo SITTING Allowance. Pia likazuka suala la Spika MAKINDA kukemea wabunge wote wanaokataa posho hizo kwamba watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu ni kukiuka kanuni za Bunge. Swali linakuja Nani aliyewachanganya Wabunge ni Spika au Mh. Zitto! Jambo la msingi ilikuwa ni kufuta posho zote kuanzia kwa Wabunge hadi Serikalini rejea maneno ya WAZIRI Mkuu –Posho zisizo za lazima kufutwa, swali je hayo yametekelezwa? Kwa mantiki hiyo endapo Chadema wangezikataa ina maana hata baadhi ya stahiki zao zilizo halali wangezikosa kwa sababu form za kusaini posho hizo hazikutenganishwa. Ingekuwa ni halali kwa wananchi kuwalaumu Chadema ikiwa tu form hizo zingekuwa zimetenganishwa kisha wakaamua kuzichukua zote, lakini kwa hili hatuwezi kuwatupia lawama chadema. Swali langu kwa Mh. Zitto. Unatuambia nini wananchi kuhusu Posho yako kupelekwa Jimboni kwako, je zimekwishapelekwa? Ikiwa zitapelekwa je utasaini form hizo? Sasa kutakuwa na tofautigani na Wabunge waliozichukua kisha wakaenda majimboni mwao na kuwasaidia wapigakura wao? Bado ni kizungumkuti kwani inaonekana Serikali haijawa tayari kutekeleza adhima hiyo ya kufuta posho legelege. Ni mawazo tu yenye mlengo wa kati.
Ikakataliwa na hakika nadhani Bunge linaweza chukua mfano huu kuutumia zaidi ya kuwapa wabunge fedha hizo. Yaani kila mbunge atapewa posho hii kupitia NGo ya jimbo lake kwa kila anayoweka sahihi pia ingesaidia kuyawezesha majimbo na wananchi zaidi ya kumpa Mbunge fedha mkononi kwendsa kununua viwanja na kufungua miradi yao binafsi..Kwani mwisho wa siku kila NGO nchini hutakiwa kuwakilisha mapato na matumizi yake kama NGO tofauti na fedha ambayo mbunge kapewa yeye.
Hivyo Bunge lilipokataa ombi hilo ndipo Zitto alipokataa kuweka sahihi ktk daftari la mahudhulio na inamweka yeye ktk nafasi mbaya ya kuenguliwa bungeni. katika nafasi Chadema iliposimama haiwezekani wabunge wake wote waache kuweka sahihi ktk daftari hili kwa sababu ndicho CCM na CUF wanakitaka na kwa uhakika watawaengua wabunge wote wa Chadema bila hata mshipa kuwashtuka na nafasi zao zitachukuliwa na mshindi wa pili ktk kila jimbo..
Kwa hiyo maamuzi ya Zitto kama mmoja wa viongozi wa Chadema lazima uchukuliwe kama ni mpango mzima wa mkakati wa kupinga hizi posho na sio ushindani ndani ya Chadema. Kwanza tazameni lengo la Zitto na sio ushindani baina yake na viongozi wengine wa Chadema..